Hivi kweli kuna watu wanapiga hela online? Mimi naona kama uzushi tu!

So far mtandao km fiverr una watumiaji zaidi ya million 3 na wote hawa wanafanya kazi online ....hii ina maana kuwa watu wote hao million 3 ni wehu we ndie Una akili
Mimi mmoja wao, nilisoma thread humu JF zinazohusiana na Freelancer, nikala ma-tutorial Youtube, nikapata baadhi ya skills, namshukuru mungu nshaanza kupata order kutoka Fiverr japo ni pesa ya kawaida nayoipata kwa sasa ila inanisaidia kidogo kukidhi mahitaji yangu ya chuo

Pesa online ipo, kikubwa Ujuzi na taarifa sahihi, alafu Kingine kinachotukwamisha wabongo ni kukosa taarifa sahihi na watu sahihi, mfano hapa chuo marafiki zangu hakuna anayejua haya mambo ya Freelancer ukimwambia anakushangaa,

Mtu ana PC amejaza Movies, Games etc weekend anaamkia na kushindia movie, sisemi ni vibaya kucheck movie, make ata Mimi huwa nacheck ila baada ya kufanya mambo yangu ya Online.

Sahivi YouTube ni darasa tosha unaweza kuingia kule ukajifunza kila kitu ambacho unakitamani then unatumia ule Ujuzi uliojifunza kujiongezea kipato.
 
inawezekana kweli maana kwa mazingira niliyopo sioni watu smart wana dili na mambo hayo.
Smart people ndio watu wa namna gani hao? Siyo kila mtu anayefanya online business anatangaza. In fact, most of successful online traders hawana huo muda wa kujitangaza na hata akimamua kijitangaza ni kwamba hiyo ni mbinu yake ya kutafuta soko lake zaidi lakini siyo kwa kutafuta ufahari.
 
kweli. Ukiona kelele nyingi ujue hamna kitu
 
Naungana na wewe mkuu
 
Hongera sana chief! Umeanza mapema sana utafika mbali, mi nimeanza iv karibuni nikiwa nina almost 34 years huwa najilaumu sana nilivyochezea muda in my twenties...ni km unavyowasema hao jamaa zako mi pia nilikuwa mtu wa movie aaubuhi mpaka enzi hizo za series za prison break

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mm nauza chorok0. Vp kuna wateja apo kwako nikuletee ili tule faida?
 
Kweli eti, afu hawa washikaji wangu mfano weekend nikiamka saa 3 au 4 asubuhi wanasema Mimi mwanaume gani nalala hadi saa 3 hawajui kwamba sometimes mtu unalala saa 9 au 10 usiku ukifanya Kaz ya client.
 
Yaan ww jamaa ilibid uulize jinsi ya kupata pesa kwenye online investment. Sio unakuja kutuambia eti huwezi tajiri, nakuhakikishia mkuu ww huna Elimu yoyote juu ya hizi issue trust me Kuna watu wanatengeneza Hadi Million 2 per day via fx. Ni vile tu watu hawana Elimu juu ya sehem sahihi ya kuinvest ndomaana wanapigwa. Lakn Kuna wanaume hawali kwa jasho kabisaa kisa hizi business.
 
Fanya unachokiamini na unachoona saihihi kwa muono wake,usitumie ubongo wa mwenzio kufikiri hatma yako, ukiwa na 1000$ kuingiza 10$perday ni kama kupiga mswaki ila angalau uwe na expiriance ya angalau miaka miwili ktk soko

 
duniani kote hakuna hela nyepesi na ukiona ubongo umekwambia kunahela nyepesi sehemu ujue basi we ndo mwepesi kupigwa pesaa. Kikubwa kilamtu na ajikite pale alipo na elimu yake ili kesho tupeane lifti. Hata wale wa korokoro la mchina nao wanaamini wataja jenga kupitia zile miambili mbili wanazokula za simba na twiga. pia na mchina nae anapiga hela hapo hapo sasa sijui nani anakula na nani analiwaTufanye kazi kwa jitihada zetu zote ili tuwe na mafanikio ya kuweza kupata milo tuitakayo, matibab u yatufaayo na sehemu nzuri ya kupumzika
 
Wacha kuletapolojo weka miamala umeyopiga kwa mwezi huko online ...

Weka miamala kama salary slip kwa mwezi mbona simple ...

Nyie watu wa online mna maneno tu ila kiuhalisia hakuna mnalopata zaidi ya vipigo ...

Forex ..

you cant win hii things easly ,lazina upoteza sanaa ili ule...!
 
Asee
anyway Baki na unachoamini bro'. Lakini naomba uwe unafuatilia Mambo ndo unaconclude public hivi. Eti huwezi kutajirika online Nani kakudanganya wewe kijana.
 
Baki na ubishi wako watu wanapiga hela..

Huyu anaitwa kileo cheki profiti yake ya leo
 
Afadhali umeongea mkuu labda ataamini Sasa Jamaa Hana exposure yoyote kuhusu hizi issue af mbishi Tena.
Watz wanafikri kila mtu anatumia mitandao kubishania siasa na kuangalia umbeya!

Hawaoni hata kijana wetu diamond ambae ni form four tu lakini hela nyingi anazipata kupitia mtandao.

Hawa watakumbuka shuka kumekucha baada ya miaka 5 ijayo
 
Well said bro'
Watz wanafikri kila mtu anatumia mitandao kubishania siasa na kuangalia umbeya!

Hawaoni hata kijana wetu diamond ambae ni form four tu lakini hela nyingi anazipata kupitia mtandao.

Hawa watakumbuka shuka kumekucha baada ya miaka 5 ijayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…