Hivi kweli hata "toothpick" tunaagiza kutoka China?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,068
151,315
Nchi ya amani lakini tunashindwa kuwa hata na kiwanda cha kutengeneza toothpick?!Hivi hii amani tunayojivunia imetusaidia vipi ukilinganisha na nchi zenye machafuko?

Tuna amani,tuna misitu,tuna ardhi na tuna wasomi lakini eti bado tumeshindwa kuwa na hata kiwanda cha aina hii kweli?!

Hivi tulikuwa na sababu gani ya kudai uhuru?Kwanini tusingewaacha wakoloni watujengee kwanza viwanda kama walivyotujengea reli na kisha ndio tuwatimue?

Hivi kwenye hii dunia mchango wetu mkubwa ulikuwa ni kusaidia nchi zingine zipate uhuru na kuhifadhi wakimbizi kutoka mataifa ya wenzetu?Je,hili ndio lilikuwa kusudio la mungu juu ya uwepo wa nchi inayoitwa Tanzania?Kama siyo,sasa sisi tuna faida au mchango gani katika hii dunia?Kichwa kinauma!!

Kilichonisukuma kuandika haya ni baada ya kukuta toothpick zilizoandikwa "made in China" katika mgahawa mmoja maarufu hapa Dodoma mjini unaojulikana kwa jina la "Wimpy Kiosk".
 
Ccm imesababisha haya yote unayolalamikia mkuu , pamoja na nchi hii kuwa miongoni mwa nchi za mwanzo mwanzo kupata mainjinia lakini inashindwa kutengeneza hata cotton buds ! Poor my country !
 
Ccm imesababisha haya yote unayolalamikia mkuu , pamoja na nchi hii kuwa miongoni mwa nchi za mwanzo mwanzo kupata mainjinia lakini inashindwa kutengeneza hata cotton buds ! Poor my country !

Alafu bila aibu kila baada ya miaka 5 wanaomba waaminiwe na warudi madarakani!! Hii ni laana!
 
mkuu tafuta mtaji ujenge kiwanda cha hiyo bidhaa ni fursa hiyo.

muda wa kulalamika umeisha,kwa sababu jukumu la kujenga viwanda ni la kila mtu si la kikundi fulani cha watu.

Watanzania tutumie fursa zilizopo tuache kulalamika,tupigane tujenge viwanda hata kama ni viwanda vidogo vidogo.
 
Kwa sasa kulalamika inatosha, naomba tuanze kujadiliana namna ya kujenga viwanda vilivyo ndani ya uwezo wetu, kikiwemo hicho, kasha tuiambie serikali kwamba azuie bidhaa hiyo kwa kuwa tunaweza kuzalisha wenyewe.

Nimenunua kiwanja mahali, nikijiandaa kuwa na kiwanda cha FENICHA, Magufuli kasema, FENICHA za serikali zitoke ndani ya nchi yetu.

TUje na suluhisho la changamoto sasa.
 
mkuu tafuta mtaji ujenge kiwanda cha hiyo bidhaa ni fursa hiyo.

muda wa kulalamika umeisha,kwa sababu jukumu la kujenga viwanda ni la kila mtu si la kikundi fulani cha watu.

Watanzania tutumie fursa zilizopo tuache kulalamika,tupigane tujenge viwanda hata kama ni viwanda vidogo vidogo.
Hata umeme wa uhakika kuvutia wawekezaji nao umewashinda.!!Mmeingia mikata mibovu shirika linaangamia!Hivi kuna jibu kubwa zaidi ya CCM nchi hii?
 
mkuu tafuta mtaji ujenge kiwanda cha hiyo bidhaa ni fursa hiyo.

muda wa kulalamika umeisha,kwa sababu jukumu la kujenga viwanda ni la kila mtu si la kikundi fulani cha watu.

Watanzania tutumie fursa zilizopo tuache kulalamika,tupigane tujenge viwanda hata kama ni viwanda vidogo vidogo.

ebwanawe ndo nchi yetu bhana..labda huyu naye tumpe mda mana naye bado anaangaika na majipu ya mkwere...
 
Shida yetu watanzania kila kitu tunailaumu serikali, kuna matajiri kibao tanzania wenye uwezo wa kuinvest katika viwanda hapahapa tanzania lakin wengi wao wanaenda kuwekeza nje, mifano hai ipo. we should play our part first before we blame the gvt
 
Jiulize kwanini wana-invest nje ya nchi ndio utajua ni kwanini serikali haiwezi kukwepa lawama katika hili.
 
Nakubaliana na wewe
 
Hata Wewe Unaweza Kuwekeza Katika Utengenezaji Wa Hizo Toothpick Pia Naomba Unitoe Katika Hizo Lawama Za Pamoja Kama Nchi, Aidha Mimi Binafsi Napendelea Uwekezaji Wa Mazao Ya Misitu Uboreshwe Zaidi Kuliko Hata Hizo Toothpick Zako
 
tatizo letu ni kulalamika tu.
wakati wa Nyerere tumelalamika.
Mwinyi tumelalamika.
Mkapa tumelalamika.
Kikwete tumelalamika.
Magufuli tunalalamika.

wanachama 100 wa JF wakiungana pamoja kila mtu akitoa mtaji wa milioni moja wanaweza kujenga kiwanda kidogo cha hiyo bidhaa.

tatizo ni ubinafsi,kulalamika na hatuchukui hatua.
 
ubarikiwe sana mkuu kitulo kwa huu mchango maridhawa
 
Vitu vya kufanya vipo vingi sana ila serikali yetu hawajakaa chini kuwa moyo wa thati kabisa haya mambo hayatekelezeki kwa kusema kisiasa lazima wakubwa wakae chini watuoneshe njia nikianzisha mimi siku mbili tu shida zitaanza
atakuja afisa mali asili
atakuja afisa mazingira
atakuja tra
Atakuja fire
watakuja kila aina ya watu mpaka mwenyekiti wa ccm kutaka pesa kwako..
Mwisho kabisa hata umeme na maji kwetu ni shida gharama yake ni kubwa sana
 
ukawa wanalia lia tu, babu yao kaanza kuonesha mfano kwa kuchunga ng'ombe.
 
Jiulize kwanini wana-invest nje ya nchi ndio utajua ni kwanini serikali haiwezi kukwepa lawama katika hili.
kwasababu hawana akili ya kuona fursa hapa nchini kwetu. sidhan kama naweza kuilaumu serikali kwa ufinyu wa akili wa matajiri wetu
 
Shida yetu watanzania kila kitu tunailaumu serikali, kuna matajiri kibao tanzania wenye uwezo wa kuinvest katika viwanda hapahapa tanzania lakin wengi wao wanaenda kuwekeza nje, mifano hai ipo. we should play our part first before we blame the gvt
Nakubaliana na wewe. Wengine wametorosha mabilioni ya pesa kwenda kuziweka nje ya nchi badala ya kuwekeza hapa hapa nchini. Pesa hizo zinanufaisha nchi zilikowekwa kwa wananchi wake kuzikopa na kuendeleza miji yao!
 
Back
Top Bottom