Hivi kwanini wadada kupiga simu na kutuma SMS ni nadra sana kwao

mzee wa misele

JF-Expert Member
May 17, 2015
366
46
Habarini wakuu nimekuwa nikichunguza mahusiano ya kirafiki au wapenzi imenishangaza sana kwa nini wadada wengi huwa wanakuwa wazito sana kutuma SMS au kupigia simu wenzi wao au Rafiki zao ,mara unakuta mpigaji simu ni mwanaume zaidi kuliko mdada , hivi hizi tabia ni wadada wote wanazo au ni baadhi yao tu ninaokutana nao
 
Nitarudi hapa
 
Sasa we mpaka uambiwe hutakiwi live ndio uelewe?mbona ni simple logic tu hapo kuwa huyo gash hakutaki.
 
Huwa nashindwa kuwaelewa wadada kupiga simu labda wawe na shida sana

Hata mimi kwa mwanaume mshenzishenzi simpigii wala msg simtumii
Lakini kama nimekuridhia moyoni na hatujakosana, hakuna tatizo lolote nitakupigia kukujulia hali, kukueleza mapenzi na mahaba yote
 
kama ni mpenz niliempenda ntampigia sim mpaka anakereka nata sms kw kila mida kumjulia khali ila mimi wa kunijali hiv sijawah kumpata
 
Wewe unazungumzia wadada gani?
Hawa ambao hushinda na simu kutwa kucha wakichati na kuongea na simu 24/7?

Labda hawakupigii wewe tu, mimi ninakazi kubwa ya kutojibu meseji na kuchunia simu zao, simu yangu nimeweka silent kwa sababu hiyo.
 
Hata mimi kwa mwanaume mshenzishenzi simpigii wala msg simtumii
Lakini kama nimekuridhia moyoni na hatujakosana, hakuna tatizo lolote nitakupigia kukujulia hali, kukueleza mapenzi na mahaba yote

Sawa.....
 
kaka hapo changanya na zako kuutambua vizuri huo uhusiano ulionao nahuyo mdada
 
Ukiona we unachuniwa kuna mwingine anaepigiwa simu na kutumiwa msg tena kila sekunde
 
Simu na sms huwa ni reserved hadi umtumie mpesa tigopesa nk utapiwa weewee utatumiwa sms weweee
 
Yaani mimi nikipigiwa au kutumiwa meseji ujue anaomba helaa,ukituma hela anakwandikia tafadhali nipigie ukipiga anakushukru kwa kumpa hela,
 
Back
Top Bottom