Hivi kwanini ni ngumu kuacha madawa ya kulevya?

Dejavu

JF-Expert Member
May 31, 2018
1,568
3,424
Katika maisha yangu sijawahi kuona teja kaacha madawa ya kulevya kirahisi na kupona kabisa, kwanini?
 
Wapo wanaacha na kupona kabisa


Heroine ina addiction sana na inaingia ndani ya damu hivyo kuacha inakuwa vigumu sababu ikifika wakati na kama mtumiaji asipoweza kupata dawa zake basi atajisikia mchovu,kupiga miayo sana,joints kuuma,kuharisha nakadhalika.

Kuna aina 2 ya kuacha madawa

1)kupitia methadone

Hapa muathirika wa madawa hujiunga na kitengo cha rehabiliation na hapa Dar zipo Muhimbili na Mwananyamala.Muathirika atakuwa anapewa dozi ya methadone na kupunguziwa dozi kulingana na maendeleo yake mpaka kuacha kabisa

2)kupitia sober au kuacha bila ya methadone

Hapa muathirika anaamua kuacha bila ya kutumia methadone hivyo atavumilia maumivu kama kuharisha sana,kutapika,joints kuuma,kupiga miayo nk na baada ya wiki ,miezi atakuwa fresh kabisa.

Naweza kukupa mfano huku mtaani kuna jamaa alikuwa teja saizi kaacha huwa napiga naye story haswa usiku kwakuwa tupo jirani.Mateja wengi kitaa wanatumia methadone saizi na huyu jamaa alijiunga methadone ila alikaa metha miezi 3 tu na kuona uduwanzi...watu wapo mwaka wa 5,4,3 methadone kila saa tisa alfajiri wanaenda kunywa dawa sasa huyu jamaa akaona anachoka akaamua akaze na saizi yupo fresh tokea mwezi march na mwingine teja nampata kaacha miaka ya zamani alienda kumuomba mama yake elfu kumi akanunue madawa mama yake akamwambia sikupi na kuanza kulalamika jamaa akamuambia mama yake nipe kwa leo nikanunue nakuhakikishia ndio itakuwa dawa zangu za mwisho kuvuta na sitovuta tena nitaacha matha wake akampa na kweli jamaa akatia nadhiri akajikaza imepita miaka mingi na yupo fiti .
 
Katika maisha yangu sijawahi kuona teja kaacha madawa ya kulevya kirahisi na kupona kabisa, kwanini?

Salaam Dejavu

Naitwa Sam
Nimefurahi sana kwa swali lako zuri ambalo sio wewe tu ambaye umekuwa ukijiuliza sana swali hili "Kwa nini mateja sio rahisi kuacha kutumia dawa za kulevya?" Majibu ni haya

Uraibu
Kama unavyofahamika pia kama Uteja ni ugonjwa unaotokana na mabadiliko katika neva za fahamu yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevya au aina kadhaa ya kemikali au shughuli na kusababisha usugu katika urudiaji wa utumiaji wa aina ya dawa ya kulevya au shughuli husika,

Katika Ubongo wa Binadamu kuna sehemu ya inayyojulikana kama ventral Cortex inayoshughulika na ma baadhi ya matendo muhimu ya kibinadamu na huongozwa na uwasilishwaji wa visafirishi (Neuro Transmitters) ambazo huwezesha matendo mbali mbali kufanyika, mfano Neoro Transmitter inayojulikana kama Dopamine huzalishwa katika VTA kutokana na GABA (Gama Amino Beuteric Acid) na kusafirishwa kupitia kwenye Neurons Kuelekea kwenye Synapse ambapo ikifika hapo umemelishaji hufanyika (Elecrification) na kufanya negative negative na positive charges, Kitendo cha kutumia Heroin, Cocain, Bangi, Pombe, au vichangamshi na vipumbazi pamoja na baadhi ya matendo kama kufanya ngono, kazi, mazoezi yote husababisha kuzalishwa kwa Dopamine nyingi zaidi kuliko kiwango cha kibinadamu cha kawaida hivyo kusababisha mtu kujisikia raha na furaha kwa muda mrefu matokeo yake ile kemikali inapokwisha mtu huanza kujisikia vibaya na kukosa raha kabisa sawasawa na mtu anapomaliza kufanya tendo la ndoa, matokeo yake mtu hutamani kutudia kutumia au kufanya mara kwa mara na kila siku jambo ambalo baadae husababisha usugu na mtu kushindwa kuacha kutumia,

Aina za Uraibu
1 Uraibuwa wa dawa za kelevya
2 Uraibu wa Pombe
3 Uraibu wa kazi/Mazoezi/Kamari/Michezo(Ushabiki)
4 Uraibu wa Ngono
5 Uraibu wa Chakula
6 Uraibu wa Matumizi ya vifaa vya teknolojia
7 Uraibu wa Kihisia (Perfectionism)
8 Uraibu wa Kununua/ Fedha nk

Namna ya kukabiliana na Urabu
Muathirika anabhitaji kusaidiwa kujitambua kwamba tayari amesahingia kwenye mtego wa ubongo wake kutekwa na urabu wa aina fulani,
Baada ya hapo atatolewa sumu mwilini kwa kusimamiwa na madaktari wa wauguzi wataalamu
Kisha atasimimawiwa kwa kipindi cha wastani wa Wiki tatu kwa ajili ya ku controll hali za kuchanganyikiwa na mawenge (Withdrawal Syndromes management)
Atafanyiwa Utambuzi Tabia Tiba (Cognitive Behaviour Therapy)
Atapewa mwamko wa Kiimani kupitia program maalumu za hatua kumi na mbili
atafanya mazoezi ya mafunzo aliyopewa na kisha atarudi kuungana na familia yake

Sam
+255 742 550 551
tanzaniamrc@gmail.com
 
Back
Top Bottom