Hivi kwa nini mababu/mabibi zetu walikuwa wachoyo sana kutoa siri za dawa/ujuzi wao...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,209
2,000
Nilikaa na babu mmoja akaniambia yeye anakachupa kadogo ka dawa ikitokea akawekewa sumu kwenye chakula anakunywa faster anapona...

Kuna bibi mmoja jirani yeye alikuwa na dawa ya uzazi, Kuna watu walioshindikana hospitalini sijui michango, mara mimba haitungi pale ni komesha, miti shamba tu Mungu anafanya uumbaji...
Bibi akafa na ujuzi wake...

Wote hawa na aina zao, source ya ujuzi wao au raw materials za hizo dawa hawawezi kusema hata kama ni mpapai tu. Hadi leo sijui kwa nini inakuwa hivyo na wengine wanakufa Bila kumwambia mtu.


Kuna mzee mmoja wa kichaga, nikaenda kumuona (Kuna ujuzi wa kicarpentry) nilitaka kujua kutoka kwake ili badala ya kununua baadhi ya samani ndogondogo nichonge mwenyewe kama sehemu ya Burudani tu hasa nikiwa sehemu za vijijini. Mzee yule kafunguka Kila kitu, kaniletea manuals, kanipa Kila ujuzi niliouhitaji. Nilishangaa nilijua ananicharge akasema ujuzi kapata bure atatoa bure...

Tabia hizi za kizee zikashuka hadi mashuleni. Unakuta jamaa anakapamphlet kadogo kana majibu almost yote, au Kuna mbinu za kutegua mitego yote iwe ni maswali ya sayansi, hesabu, biashara lkn hutakaa ukaone hadi siku ya kumaliza mitihani....


Inabidi ninunue baadhi ya products zake kumuunga mkono....

Uchoyo, ubinafsi, usiriusiri kwenye mambo ya muhimu yenye faida unaturudisha nyuma sana watanganyika(wazanzibari Siwezi kuwasemea maana siwajui vzr). Kuna uwezekano tabia hizi za kijima tunarithishana kutoka kwa mababu zetu...
Kuna watu wakijua kakitu hata kwa kuwalipa fee kidogo, hawako tayari....


Je hili limewahi kukukuta?
.....
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
52,322
2,000
Wanasema "information is power" "mwenye taarifa au ujuzi ndiyo mtawala"

Kwa hiyo siyo rahisi mtu akuambie siri za jambo ambalo kwanza wengi hawalijui alafu linafaida kubwa...


Coca cola mwenyewe mpaka leo hajatoa siri zake...


Cc: mahondaw
 

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,440
2,000
Walikuwa wanamiliki na kujua mambo makubwa mno,walikuwa wanashindwa kumuamini wa kumuachia,mpaka wampime imani kwamba hatavuruga jamii,

Fikiria mwanamalundi alikuwa na uwezo wa kunyoosha kidole miti yote mbele yake ikakauka pamoja na mifugo,watu,hii kitu ukiwapa ccm chadema watabaki?
 

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,440
2,000
Pia walikuwa wanafanya maombi mpaka mvua inanyesha,tena kwa eneo wanalotaka,may be ni Mungu ndiye alizuia wasirithishe,walikuwa wqnatembea wanapita porini,simba,nyoka wala chui hamgusi,akimkaribia mnyama huyo anapisha njia!
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,136
2,000
SIDHANI KAMA WALIKUWA WACHOYO,ILA KULIKUWA NA WALENGWA WAO WA KUPEWA TECHNOLOGY HIYO
 

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,209
2,000
Wanasema "information is power" "mwenye taarifa au ujuzi ndiyo mtawala"

Kwa hiyo siyo rahisi mtu akuambie siri za jambo ambalo kwanza wengi hawalijui alafu linafaida kubwa...


Coca cola mwenyewe mpaka leo hajatoa siri zake...


Cc: mahondaw
Tatizo linakuja kama hilo jambo lingewekwa wazi watu Wengi ktk jamii wangepata faida/manufaa (benefits) sio faida (profits) kama formula za koke. Tatizo kubwa zaidi hawa hasa wazee wanakufa na siri hizi kunatokea discontinuity ya ujuzi mkuu
 

baba glory

JF-Expert Member
Jan 22, 2016
294
250
Hapana Sema na sie wa digital hatuamini hizi mambo mie nikiwa kijijini kabla bibi hajafariki nilikuwa najua dawa kibao ila sasa duh!? Hakuna kitu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom