Hivi kwa kauli ya Magufuli, ukweli unaweza kujidhihirisha?

Ksuley

JF-Expert Member
Dec 18, 2015
1,166
445
Habari ya asubuhi wanajukwaa,

Jana wakati namsikiliza Mh. Magufuli katika hotuba yake ya kuzindua mwaka mpya wa mahakama! Ilikuwa ni yenye mguso mkubwa, hasa nimevutiwa na kipande alichosema kuwa wakati anaingia madarakani kwa mwezi wake kwanza, "Hazina kulikuwa hakuna pesa ya kulipa hata mishahara "Sasa ndio nikapata swali, je, kumbe viongozi wa serikali wanaotoa matamko ya kukanusha taarifa zinazohusu serikali, ambazo utolewa na vyombo vya habari, huwa wanakurupuka tu, bila ya kufanya uchunguzi wa kina!

Maana habari ya serikali kukosa pesa ziliwahi kuandikwa na baadhi ya magazeti ya hapa nchini!Kuwa "Hazina imekaushwa" kwa kukombwa pesa kipindi cha kampeni! Serikali ilivyokuwa ikimaliza muda wake na watendaji wake wakikanusha! Sasa kwa maneno ya Mh. Magufuli, nani wakweli wale waandishi wa habari walioandika zile habari au wale watendaji wa serikali waliokanusha hizo habari.
 
Tunaambiwa kuwa matumizi ya serikali yanatokana na makusanyo yanayopatikana kila mwezi. Sasa kama aliingia ofisini na fedha hazijakusanywa unategemea nini?
 
Back
Top Bottom