Yudatade Edesi Shayo
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 2,903
- 4,306
mimi nilikuwa moja ya watanzania,waliokuwa na furaha baada ya ripoti mbili za prof Mruma na prof Osoro.niliona dhamira ya dhati ya mh raisi kulinda na kutete maslahi yetu.ila thatha,juzi serekali imepeleka miswada 3 bungeni,nakuazimia kuipitisha kwa hati ya dharura!!nimejiuliza kwa upeo wangu mdogo,je tunarudi 1997 kwenye hati ya dharura ya madini au 2015 mswada wa mafuta na gas tulipokuwa tunaipitisha utadhani tunakimbizwa?? hivi kweli jamani tukipata muda tukajadili kwa uangalifu,umakini,kitaalamu zaidi,itakuwa dhambi???? Mt kilimanjaro itahama? Serengeti itafutika yani sielewi haraka ya nn,mali zetu wenyewe.au hiyo miswada nikana kwamba tunaenda vitani?tukichelewa adui atatumaliza??tuache masihara na maigizo kwenye maslahi ya taifa hili.tusije mpongeza raisi mwingine atakaye unda tume ya kuchunguza hii mikataba inayo pitishwa wakati hu, kana kwamba kuna ugomvi. huko mbeleni..