Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 15,849
- 36,141
Nadhani kila mmoja anaelewa kwa Morogoro road ndiyo njia kuu ya kuingia Dsm, kwa namna yeyote mimi nilitegemea hii barabara ingewezeshwa ili iweze kupitika kwa urahisi muda wote!
Ila kituko kinaanza pale Kimara mwisho, licha ya uwekezaji mkubwa kwenye kituo cha BRT sidhan kama waliwafikiria watumiaji wengine. Kimara muda wote pana folen, na watu wanaotoka mjini wakishavuka pale folen inakuwa imeisha. Pamoja na utanuzi wa barabara wanaofanya mimi sioni kama tatizo linaenda kuisha pale (kwanza barabara yenyewe toka ilivyoanza hata haiishi, hata huo utanuzi wake ni kama wanafanya utani maana barabara bado ni finyu sana kwa pale kimara Terminal.
Kingine licha ya wakazi kutosha pande zote mbili za kimara ila huwezi vuka toka upande mmoja kwenda mwingine moja kwa moja ukiwa na gari, mtu anayetoka upande ilipo TRA na anataka kwenda uelekeo wa bunyokwa basi ni lazima aende mataa yaliyo mbele ya Korogwe ama aende Stopover. Mwanzo palikuwa na round about ambayo inatoa magari upande mmoja tu. Kwa sasa pale wamepavuruga na sijui wanakuja na design gani!
NB: Kama design za kawaida kabisa hizi za barabara zinatutoa jasho, kuna siku tutatoka kweli kwenye huu umaskini wa dunia ya tatu?