Hivi kuna haja ya kuwa na kumbukumbu ya matukio yakutudoofisha na kutuumiza?

eerua

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
373
204
Habari wakuu,

Najiuliza kwa muda sasa hivi kuna haja ya kutunza kumbukumbu za matukio ya aina zote kati ya mabaya na mazuri?

Kwanini mtu unaempenda kwa dhati akitangulia mbele za haki(kufariki)watu wachukue filamu na picha za mgando tena wengine wanaenda mbali zaidi kama mpendwa wao alipata ajali utakuta wameanzia huko, wakienda mortuary wanachukua picha pia hadi kuzika.

Waungwana nadhani Mungu alituumba akijua kuna siku kati yangu na wewe lazima mmoja wetu ataona maiti ya mwenzie vilevile katupa kusahau pia kwa kuendekeza hayo mambo yanchelewesha sana watu kusahau na kuendelea na maisha.

Kwa mfano kinachofanywa na Radio flani sidhani kama ni kuomboleza kwa mtizamo wangi bali pia kinaumiza sana mtu unaenda kumrekodi mfiwa analia then unamuweka hewani watanzania wote walie pamoja, inauna sana tujitahidi kusaidia walioumia mioyo yao japo machungu ya pungue.

Mungu ni mwema sana.

R.I.P wanangu wa Arusha.
 
Watu wanachukua historia zitakazodumu hata vizazi vijavyo.

Kuna watoto wamezaliwa baada ya kifo cha Nyerere, lakini wanaweza kuona siku ilivyokuwa bila kutegemea maandishi kwa sababu ya video.

Hiyo redio si lazimausikilize, kama unaona haikufai unaweza kuzima au kubadili stesheni.
 
Tangu nimeanza kuangalia TV sijawahi kuona marudio ya mazishi ya baba wa taifa. Kuchukua mikanda kwenye mazishi ni ulimbukeni hakuna mtu huwa anakuja kuangalia mikanda hiyo. Tuwakumbuke watu kwa matendo yao wakati wakiwa hai, sio tukumbuke walivyolala kwenye jeneza.
 
Watu wanachukua historia zitakazodumu hata vizazi vijavyo.

Kuna watoto wamezaliwa baada ya kifo cha Nyerere, lakini wanaweza kuona siku ilivyokuwa bila kutegemea maandishi kwa sababu ya video.

Hiyo redio si lazimausikilize, kama unaona haikufai unaweza kuzima au kubadili stesheni.
Mkuu soma uzi kwa kutulia utaelewa tu..
 
Mkuu soma uzi kwa kutulia utaelewa tu..
Kwa nini unafikiri sijasoma uzi kwa kutulia?

I take offense to that statement.

Unaweza kunionyesha kivipi umejiridhisha kwamba sijasoma uzi kwa kutulia?

Kama mimi nina mtoto, bibi yake amefariki kabla mtoto hajazaliwa, na siku ya msiba ilikusanya watu wengi sana kuliko siku nyingine yoyote katika maisha ya huyo bibi, na huyu mjukuu anafanya research ya familia kuandika "family tree", hana pa kuanzia, ila kuna video ya huo msiba iliyowakamata ndugu wengi sana ambao wangeweza kusahaulika, huoni kwamba huyo mjukuu atapata resource nzuri ya kuandika hiyo "family tree"?

Acheni upumbavu wa kujificha chini ya mawe kama watu ambao hawajaelimika.

Huu ni ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
 
Back
Top Bottom