Hivi kumkosoa mdada/mama aliyepika hovyo ni kosa?

Hivi kumkosoa mdada/mama aliyepika hovyo ni kosa?

Na wewe umezidi. Ungeongea nae kirafiki. Hujatumia maneno mazuri. Unamwambiaje "chumvi imewekwa na meneja wa uvinza". Halafu siku nyingine mwite pembeni.
 
Kupika najua tu, ila naendelea kujifunza. Wife kama ananisikia au kunisoma ajipange. Sio aje kunipikia uji wa korie au sijui viazi mbatata na ubuyu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Teh teh teh. Ila kwako huyo mkeo kazi anayo. Mana pale atakapokupikia visivyoelewaka hutamchelewesha kumpa makavu.
 
Wife yupo poa kwenye issue ya misotojo ila ameambiwa asifanye kazi for a certain time mpaka atakaporudi tena hospital kwa ajili ya clinic ya mtoto.
Pole kaka. Mpe pole pia shem. Mungu atamfanyia wepesi.

Hapo hata mie ningevumilia while seing namna ya kurudisha furaha ya chakula nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0a85ff547db1e36cd51ccf3d4d89263e.jpg
 
Teh teh teh. Ila kwako huyo mkeo kazi anayo. Mana pale atakapokupikia visivyoelewaka hutamchelewesha kumpa makavu.
[emoji12] [emoji12] naweza kukosa mke eeeh! Nipo poa tu, na wife will enjoy my run!! Ila ajue kupika aisee. Akikosea nitamwambia, akipata tatizo nitamsaidia pia...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukhuty ipo hivi mshikaji alikuwa ameleta Mke wake mkoani, sasa kwa kuwa ni marafiki akatupa mualiko usio rasmi.

Wali choroko ukaletwa, kupiga kijiko cha kwanza nikahisi kama natafuna kokoto

Nikadhani ni mimi mwenyewe ndio nimesikia, kumbe hata yule rafiki yangu niliyeenda naye alikuwa ananipimia na nilipomcheki akawa anatabasamu tukapeana signal .. Shemeji akaanza mbona hamli kitapoa au niwaletee na chai, tukamwambia asihofu kwani hatuna haraka..

Cha kushangaza mwenyeji wetu yeye wala hawazi anapiga kama kawaida na alikuwa anakaribia kumaliza sahani, sie ndo kwanza aibu kuacha hatuwezi na kukimalizia ukawa mtihani mgumu hadi pale mpishi alipokiri kuwa hajui kupika wali choroko ndo tukapata upenyo wa kutokea.,

FUNZO: Pamoja na kuwa yule mwanamke hakuwa anajua kupika, historia yake ilikuwa wazi kwani maisha yake yote yalikuwa yanategemea zaidi kufanyiwa kila kitu na mfanyakazi wa nyumbani kwao, hivyo hilo likamlemaza kwa kiasi kikubwa.
 
Hukumkosoa ulimchamba
hahahaha kweli alimchamba na hana kifua...na watu hawafundishwi kwa njia hii..
Binafsi mwanamke asiyejua kupika namuoanaga kama kilema kabisa na hii huchanguiwa sana na malezi maana wanawake hukuzwa na tabia za nyumbani kwao....
Huyu alipaswa kula hata kidogo na kuondoka....nyumba huficha mengi ukialikwa unayo yakuta unayaacha pale na kuyamezea...hata kama mtu mlizoeana vipi kuna vitu ukimwambia na mazingira fulani huwa si kumfunza bali ni kumdhalilisha maana ni wazi huo ndio uwezo wake wa kupika ulipofikia....

Lakini hili linafundisha sana wazazi kuwakuza vyema watoto wa kike na wakiume..mapishi ni muhimu sana kwa mwanamke...
 
hahahaha kweli alimchamba na hana kifua...na watu hawafundishwi kwa njia hii..
Binafsi mwanamke asiyejua kupika namuoanaga kama kilema kabisa na hii uchanguiwa sana na malezi maana wanawake hukuzwa na tabia za nyumbani kwao....
Huyu alipaswa kula hata kidogo na kuondoka....nyumba huficha mengi ukialikwa unayo yakuta unayaacha pale na kuyamezea...hata kama mtu mlizoeana vipi kuna vitu ukimwambia na mazingira fulani huwa si kumfunza bali ni kumdhalilisha maana ni wazi huo ndio uwezo wake wa kupika ulipofikia....

Lakini hili linafundisha sana wazazi kuwakuza vyema watoto wa kike na wakiume..mapishi ni muhimu sana kwa mwanamke...
Nimekupata kaka!! Najua aliumia japo mpk sasa bado nawasiliana nae na anadai kaimprove....

Siku nikimtembelea nitaleta mrejesho.

Kuna wa kurekebisha kwa carrot na wengine sticks....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli kaka, hili ni tatizo sana maana wanawake wengi hawajui kupika, unakuta tangu kindergaten yuko school bus akija home msosi upo, primary boarding akirudi home tour serengeti,secondary ivo ivo adi chuo, akija kuolewa nambie mziki wake. hajuiiii kitu. nin cha kufanya??? ni kuwaaambia ukweli ili kuondoa aibu ambayo inaweza tokea mbele kwa kupuuza makosa ya sasa.
 
Yes, mficha uchi hazai...ukweli unatuweka huru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi ningekumaindi saaana, huwezi nisaidia kukosoa mke wangu.
 
Mkuu, humu MMU unatamba kuwa Ulimchana , ila nikupe angalizo, hakikisha unapotoa somo mpe mhusika mwenyewe.

Pia niseme usipotumia mdomo wako vizuri maisha yako yanaweza yakachanwa dakika yo-yote ile Kwa sababu ya maneno yako yasiyo kuwa na staha.

Huwezi ukaelewa, mke na mume wameongea nini juu yako baada ya we apo kuondoka.
Tena, huwezi tambua mke wake atakapokuita baada ya mwezi mmoja ni kitu gani atakiandaa kama chakula.

Kwa hiyo, jiangalie sana.
 
Back
Top Bottom