Kuna wasomi wa aina mbili; walio elimika na wasio elimika. Wasomi unao waongelea wewe ni wale ambao hawaja elimika. Hawa huwa wamejaa dharau, kiburi, kujisikia, kujiona, kujidai, nk.
Aina hii ya wasomi unaweza ukawakuta wanaishi maisha ya kifahari halafu wazazi na ndugu zao huko vijijini walikotokea wakiishi kwenye dimbwi la umaskini. Kiufupi ni watu wabinafsi na walafi waliopitiliza.
Binafsi sina ujasiri wa kumdharau mtu kwa sababu tu ya umasikini wake, elimu yaje, kazi yake halali inayomuingizia kipato, umri wake, jinsia yake, nk. kwa kuwa tu eti mimi ni zaidi yake na ni msomi! Huo ndio tunaouita ULIMBUKENI! Mbaya zaidi wanaoitwa wasomi wengi wa Tanzania wanaangukia kundi hili.Wamejawa na superiority complex isiyo na tija dhidi ya makundi mengine.