Hivi kujua lugha ya kiingereza ndiyo usomi Tanzania?

Kaka wakati tunaendelea na majadiliano kasome english course ili uwe fit pale british council maana utakosa kazi kweli atiii.
Hatuna kitu, vile tulivyonavyo si vyetu wamepewa wenye lugha zao atakutaka nini tena wewe? kama ni mgodi anao yeye wewe aje kwako kufanya nini mpaka ajue english. inabidi tujifunze ili tuombe vibarua. China na ufaransa na nchi zingine hawamtegemei mtu kwenye uchumi wao.
 
na hao wachina ambao kwao wanatumia kichina kila shule sasa hivi ndio wanajaza university kubwa za uingereza,wa-russia wanaleta hadi vitoto vya primary, waarabu ndio usiseme sasa sisi ambao hatuna hata kiwanda cha calculator leo mnataka msijifunze kiingereza.
 
kila msomi lazima ajue kiingereza lakini sio kila anaejua kiingereza ni msomi

Mh, sasa kama nimesoma china na nikasoma kwa kichina tu hadi nikapata PHD.....mie si msomi? sitakiwi hata kurudi nchi kwani ntakuwa sijui kabisa kiingereza!?
 
Mh, sasa kama nimesoma china na nikasoma kwa kichina tu hadi nikapata PHD.....mie si msomi? sitakiwi hata kurudi nchi kwani ntakuwa sijui kabisa kiingereza!?

we ni msomi,kumbuka hii thread inahusu wasomi wa tanzania,nimesoma na wengi kuanzia vidudu na baadae chuo kikuu wakaenda kusoma china/russia/poland na huko wamesoma kwa hizo lugha zao,lakini hadi kufikia hatua ya kwenda hizo nchi walikuwa wanajua kiingereza.
kama umesoma china kuanzia vidudu-phd hii thread haikuhusu.
 
Kwa aliyekulia na kusoma hapa Tanzania tu kuanzia kidato cha kwanza na kuendelea usomi wake utapimwa pia kwa Kiingereza pia. Ila kama kakulia nje na kusoma huko au hata bila kusoma, Kiingereza hakiwezi kutumika kupima usomi wake.
 
Mh, sasa kama nimesoma china na nikasoma kwa kichina tu hadi nikapata PHD.....mie si msomi? sitakiwi hata kurudi nchi kwani ntakuwa sijui kabisa kiingereza!?

Ukienda kwenye li-international conference huko South Africa utafanyaje na hiyo presentation yako kwa Kichina? Utajifunza nini kutoka kwa hizo za wenzio ambazo ziko kwa Kiingereza? Utakuwa msomi uliyejitenga na wenzio!
 
Kwa aliyekulia na kusoma hapa Tanzania tu kuanzia kidato cha kwanza na kuendelea usomi wake utapimwa pia kwa Kiingereza pia. Ila kama kakulia nje na kusoma huko au hata bila kusoma, Kiingereza hakiwezi kutumika kupima usomi wake.

ur right,na hii thread sidhani kama inazungumzia waTZ waliokulia nje otherwise ingekuwa haina maana.
 
"kila msomi lazima ajue kiingereza lakini sio kila anaejua kiingereza ni msomi"
Mbebabox vipi mkuu!!hilo box lina nini unachoka hivi mkuu!?
umesema kila msomi lazima ajue kiingereza.....maana yake ni pana sana lazima ijibiwe kwa uga mpana pia. hukutakiwa kuijumlisha tu kauli yako ya kila msomi lazima ajue kiingereza!!!!!!hamna kitu kama hicho unachokitaka..
 
very simple,thread hii inahusu tanzania,nimesema hivyo kwa wasomi watanzania vinginevyo tusingejadili kwasababu ambayo iko wazi.
 
very simple,thread hii inahusu tanzania,nimesema hivyo kwa wasomi watanzania vinginevyo tusingejadili kwasababu ambayo iko wazi.

Unaogopa kukubali kuchemka kama JK? lakini bado, hata hapa TZ Si lazima kila msomi lazima ajue kiingreza, tafakari....
 
Unaogopa kukubali kuchemka kama JK? lakini bado, hata hapa TZ Si lazima kila msomi lazima ajue kiingreza, tafakari....

LOL,niogope nini mkuu,nobody is perfect,huwezi kutumia kiingereza kuanzia form1 hadi chuo kikuu then uwe hujui kiingereza au labda maana yako ya kujua kiingereza na ya kwangu ni tofauti.
 
LOL,niogope nini mkuu,nobody is perfect,huwezi kutumia kiingereza kuanzia form1 hadi chuo kikuu then uwe hujui kiingereza au labda maana yako ya kujua kiingereza na ya kwangu ni tofauti.

Naona namimi kuna kitu hatuelewani hapa ngoja......tutaendelea siku nyingine.
Leo tuendelee kumpompoa mawe JK wee na ubabe wake wa ajabu kwa wanachi ....
 
Mpende msipende kiingereza ni cha muhimu sana ukisoma nje ya nchi ndo utajua umuhimu wa lugha ya kiingereza, lasivyo utashinda umejifungia chumbani kwako kwa kuogopa kuongea na watu. Kama unawatoto jitahidi sana uwape msingi mzuri wa kiingereza ndugu yangu la sivyo watakulaumu.
 
Hapa kwenye lugha ni tatizo kubwa Tz. Si kiswahili wala kiingereza vyote tumeegesha tu! Labda tunaweza zaidi 'kiswa-kinge'!
 
Lugha Kingereza limeenea sehemu kubwa duniani kwa sababu ya ukoloni tu hii ina maana kwamba Uingereza ilikuwa na makoloni mengi duniani kuliko mataifa mengine ya Ulaya,hilo la kwanza,la pili ni kwamba Uingereza lilikuwa Taifa la kwanza kuwa Industrialized,kwa maana nyingine lilikuwa ni Taifa lililotawala dunia kwa upande wa Uchumi na kisiasa na mambo mengine mengi.

Hizo ni sababu tu zilizoifanya Kiingreza ichukue nafasi kubwa sana duniani na ndo maana kwetu huku Tanzania,masomo mengi kuanzia Form 1 hadi Chuo chimbuko lake la baadhi ya masomo mfano Biashara,Sheria ,Sayansi na Hisabati au hesabu(Mathematics) chanzo au chimbuko ni Uingereza ambalo liliandaliwa kwa kutumia Lugha ya Kingereza.

Sasa unaposema mtu ni msomi, inawezekana Lugha ya Kiingereza anaifahamu vizuri kuanzia kwenye Vocabularies hadi grammar na kumalizia kwenye pronaunciation,yeyote anayepapata vizuri hayo maeneo ni mjuzi mzuri wa kiingereza katika kuitumia. Usomi unakuja wapi? Usomi unakuja pale katika mafunzo yote aliyoipata/alizopata mtu huko nyuma na kuitumia vizuri na akazalisha matunda mazuri katika kazi zake na kwingineko,huyo ndo msomi.

Usomi wowote ule ambao mtu anaitumia usomi lakini matunda yake si mazuri,huyo si msomi.Kwish ney!!!
 
Katika Tanzania kupasi mara nyingi si lazima ujuwe kitu,unaweza kuibilizia majibu ukawa fasi darasani na ukapata cheti cha daraja la juu.Samahani sidhani kama wewe ndiye huyo.
Hata hivyo ni kweli kuwa unaweza kujua lugha ya kiengereza vyema na ukawa sifuri kichwani.Sitomsahau mwanafunzi wangu ambaye aliletwa shule kama kupunguza ghasia nyumbani,ni taahira kabisa lakini kwa kimombo hata mimi akinipa tabu kwa tense zake.Hesabu ya 2+2 hakuwahi kujuwa jawabu yake.Hata ukimkaririsha mara ngapi akirudi kwenye mtihani kama hajawahi kuisikia.
 
Kwa mtazamo wako huo kuna siku hata choraa wa kenya au uganda akawa anatuongoza kisa anajua kiingereza! jamani poleni wtz
 
Kwa hiyo? maana hujamalizia upo wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…