VIJIMAMBOJR
New Member
- Jul 18, 2022
- 1
- 0
LUGHA NI NINI?
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokubalika na jamii ya watu fulani ili zitumike katika kuleta mawasiliano. Tunaposema sauti za nasibu tunamaanisha nini? Ukweli ni kwamba hakukuwa na kikao maalumu kilichokaliwa na watu na kuteua sauti ambazo ni lugha hivyo basi ni sauti za nasibu kwa sababu zilitokea kwa bahati tu na watu wa jamii husika wakaamua kuzifanya ndiyo njia zitakazoweza kuwaletea mawasiliano baina yao. Jamii ya watu fulani inamaanisha nini? Tunaposema jamii ya watu fulani tunamaanisha ni kikundi cha watu kilichokusanyika pamoja na kinachofanya shughuli zake kwa pamona na kwa ushirikiano, mfano; Kabila au taifa.
CHANZO CHA MATUMIZI YA LUGHA YA KIINGEREZA KATIKA MFUMO WA ELIMU TANZANIA.
Ni vema ikakumbukwa kuwa Tanganyika ilipata uhuru 09/12/1961 kutoka kwa mwingereza chini ya utawala wa Malkia Elizaberth. Ilipofika mwaka 1962 Tanganyika ikawa jamhuri na ikaongozwa na waziri mkuu Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye ndiye aliyekuja kuwa Rais wa kwanza wa taifa hili (Tanzania). Wakati huu wote Tanzania ililazimika kuchukua mifumo mingi ikiwemo ya kiutawala na hata ya elimu kutoka kwa mwingereza na hii ililazimika hata lugha ya kufundishia na kujifunzia iwe kiingereza katika ngazi mbalimbali za elimu.
FAIDA ZA MATUMIZI YA LUGHA YA KIINGEREZA KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA.
Katika jamii ya sasa kumekuwa na mijadala mbalimbali inayohusu lugha ya kufundishia na kujifunzia katika mfumo wa elimu Tanzania. Mjadala umejikita zaidi katika kuachana na kuendelea kutumia kiingereza na badala yake itumike lugha ya Kiswahili katika mfumo wetu wa elimu yaani katika kufundishia na kujifunzia kwa upande wa wanafunzi. Zifuatazo ni faida za kwa nini kiingereza kiendelee kutumika katika mfumo wetu wa elimu;
1. KIBIASHARA
Taifa Tanzania kama mataifa mengine haliwezi kujitenga kibiashara, ili uingie katika biashara za kimataifa lazima ujue lugha zaidi ya moja ili uweze kufanya biashara na watu wa mataifa mengine. Katika Dunia ya sasa lugha ya biashara ni kiingereza kwani ndiyo lugha inayozungumzwa katika mataifa mengi ulimwenguni, hivyo kuijua lugha ya kiingereza kunatoa fulsa kwa muhitimu kuingia moja kwa moja katika soko.
2. KIMSAMIATI
Kama nilivyosema hapo awali kuwa Tanzania ilichukua mifumo mingi kutoka kwa koloni mama (colonial master) mwingereza hivyo basi misamiati mingi tuliyoiingiza katika mfumo wetu wa elimu ni ile inayotokana na lugha ya kiingereza kitu ambacho ni kigumu kwa sasa (itachukua muda) kubadilisha na kuiweka katika lugha ya kiswahili. Mfano, Bunsen Burner tutaiitaje kwa kiswahili? Vipi kuhusu Archemides Principle? Na Zinjanthropus je? Hii ni baadhi tu ya mifano.
3. KIUTAWALA
Mfumo wa elimu ndiyo unaozalisha wasomi ambao wanategemewa kuwa viongozi wa baadaye. Matumizi ya kiingereza katika mfumo wetu wa elimu ndiyo unaozalisha wasomi ambao leo hii wanakwenda mataifa mbalimbali katika kutafuta fulsa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi. Mfano mzuri ziara za Rais wetu mpendwa MH. Mama Samia Suluhu Hassan (mama wa taifa) katika nchi mbalimbali kwenda kutafuta fulsa ambazo zinalifanya taifa lisonge mbele. Kufika kwake huku na kufanya mazungumzo kwa urahisi kumechagizwa na umahili wake katika kuijua lugha ya kiingereza kama lugha ya kimataifa. Hivyo endapo tutatumia lugha ya kiswahili tutazalisha watawala ambao watashindwa kutoka nje kwenda kutafuta fulsa au kwenda lakini kushindwa kutafuta fulsa stahiki kwa kushindwa kuelewa lugha zilizomo kwenye mikataba husika.
4. UMAHILI
Ni fahari kwa binadamu kuwa mahili wa lugha zaidi ya moja. Wote ni mashahidi kuwa kiswahili ni lugha inayotumika kwa kiwango kikubwa sana katika jamii ya watanzania. Ni vema kiingereza kikaendelea kutumika kama lugha ya kufundishia na kujifunzia ili kuifanya jamii (wasomi) wawe mahili katika lugha hii ya kiingereza na si kubaki kukimidu kiswahili pekee. Endapo kiingereza kitabaki kuwa kama somo basi tutazalisha jamii ambayo mahili katika lugha moja tu ambayo ni kiswahili. Hii itatokana na kuwa tuna jamii ya watu wachache wenye uwezo ambao watakitafuta kiingereza nje ya mfumo wetu wa elimu.
CHANGAMOTO ZA KUTUMIA LUGHA YA KIINGEREZA KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA.
Zipo changamoto mbalimbali ambazo ndiyo zinapelekea ugumu katika matumizi ya lugha ya kiingereza katika mfumo wetu wa elimu (Tanzania).
1. MWAMKO
Upo mwamko mdogo kwa wanafunzi katika kujifunza lugha ya kiingereza na hii ipo hasa kwa wale waliopo shule za vijijini za kutwa. Sababu kubwa ni kwamba hawaoni wapi wanaweza kukitumia kiingereza kama lugha ya mawasiliano mbali na shuleni peke yake. Hii inapelekea kuona kwamba kiingereza hakina faida yoyote mbali na shuleni hivyo kutokuweka juhudi za kutosha katika kuimudu lugha hiyo. Matokeo ya hili ni kumfanya mwalimu achanganye lugha wakati wa kutoa maudhui ya somo ili kuwawezesha wanafunzi kuelewa maudhui hayo.
2. MFUMO WA ELIMU
Mfumo wa elimu Tanzania pia umekuwa changamoto, wapo wanaosoma kwa lugha ya kiingereza kuanzia primary hadi elimu ya juu na wapo wanaojifunza kwa lugha ya kiingereza kuanzia shule za upili (secondary). Hii inazalisha tabaka mbili tofauti ambazo zinazoona kiingereza kjna manufaa kikitumika kama lugha ya kujifunzia na kufundishia na tabaka linaloona ni vema kikatumika kiswahili. Vivo hivyo kwa walimu, mwalimu ambaye amekulia maisha ya English medium ni tofauti na yule aliyekulia miasha ya shule za kawaida (St. Kayumba/kidumu na mfagio).
Hakuna lugha iliyo bora kuliko lugha nyingine. Kila lugha ni bora katika jamii husika. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba sisi kama watanzania lazima tuangalie faida iliyopo hasa katika ulimwengu huu wa utandawazi na ni ulimwengu wa kimataifa zaidi na si kitaifa katika lugha ipi inafaa zaidi katika mfumo wetu wa elimu. Tusiwe watu wa kuwaza kwa haraka na kufanya maamuzi. Tuangalie ni kwa kiasi gani mabadiliko ya lugha katika mfumo wetu wa elimu yanaweza kuleta athari.