Hivi kujua lugha ya kiingereza ndiyo usomi Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kujua lugha ya kiingereza ndiyo usomi Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutunga M, May 5, 2010.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Katika usaili unaofanyika katika maeneo mengi unakuwa katika lugha hii ya kigeni na wale wanaoonekana kubwabwaja vizuri lugha hii ya wakoloni ndiyo huesabiwa kama bora na wakati mwingine kupata ajira.

  hata matamshi ya wananchi ni kuwa mtu anayetema vema ung'eng'e anaonekana ndiye msomi hata kama ni bongo lala

  hivi tufanye nini kuondokana na tatizo hili kama wenzetu china ambapo lugha za magharibi wanazitumia kwa utashi tu wa jambo fulani

  au bado tunatawaliwa!
   
 2. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo kubwa!
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu pole, lakini ndiyo hali halisi.
  Ni kweli watu wanaamini kuwa mtu mwenye kuongea kiingereza kizuri anaakili sana lakini hicho kitu hakina ukweli wowote.......Wako hta hapa nchini watu wenye upeo mkubwa tu lakini hwajui kiingereza na wengine wengi tu wanaoongea kingereza hawana akili kabisa hadi unajiuliza walijuaje lugha ya kigeni ilhali hawana akili kiasi hicho!
  Mfano mzuri ndugu yangu ni wakenya... wanaongea vizuri sana kiingereza kuliko waTZ lakini ukiwapima wanachoongea na kukielewa wakenye nimbumbu mno kwa waTZ! Akili ya kitumwa imewatawala kudhani kujua kiingereza ni kufanana na mzungu(mwingereza?)......
  Kukijua kama njia ya kurahisisha mawasiliano sawa, lakini kukitumia kama kigezo cha akili ni pumba.
   
 4. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,906
  Likes Received: 21,007
  Trophy Points: 280
  mheshimiwa MPOGORO,MZIZI WA MBUYU.....
  mimi naomba kuuliza swali,
  mtu unasoma kuanzia form 1 hadi university(miaka 9+ ) kwa kutumia kiingereza kwa masomo yote(kasoro ya lugha nyingine) halafu unamaliza chuo kikuu una degree hujui kiingereza katika hali ya kawaida mtamuelewa vipi huyo mtu?
  NB:huko china/russia etc hawatumii kiingereza kama sisi wanatumia lugha zao kwenye kila kitu hivyo huwezi kuhoji ukikuta watu wao hawajui kiingereza.

  kwa maoni yangu huwezi kutenganisha kiingereza na usomi tanzania hadi tutumie kiswahili kama lugha ya kufundishia hadi chuo kikuu.
   
 5. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kwa tz, ndiyo, kujua lugha ni usomi, kutojua hii lugha ni ubabaishaji. kwanini nasema hivi? kwasababu kuanzia form one hadi university tunasoma kwa kimombo, ni kama zaidi ya miaka nane 8 yote unasoma kwa kiingereza, hivyo ni wazi kabisa kuwa wewe kama haujui kuongea vizuri, basi ulikuwa hauelewi vizuri masomo uliyokuwa unasoma, hivyo wewe si msomi.

  kuna wengine hawajaenda shule lakini wako fluent kama nini, hao ni kundi lingine, wana faida sana ktk ulimwengu huu wa sayansi na teke linalokujia, kwasababu vitu viingi viko operated kwa kimombo, hao pia nitasema ni wasomi, pamoja na kwamba ni katika level ya chini. usiongelee mambo ya china, japan au india, italy na scandinavian countries kuongea lugha zao za asili madarasani na kila sehemu. wanapata shida sana wakija kwenye biashara ya kimataifa,na wengi wanaenda kusoma kimombo.
   
 6. T

  Tall JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Kujua kiingereza sio usomi,hiyo ni lugha tu kama kizaramo vile.lakini kujua kiingereza ni dalili nzuri kuwa angalau ulienda shule.maana somo hili hufundishwa huko mashuleni.shule gani kuna somo la kizaramo?kinyakyusa je?
  Ni vema sana ukatumia lugha ya kiswahili,hii inasaidia sana kufikisha ujumbe ulioutarajia.
  Tatizo ni kuwa,kiswahili kina maneno machache kuliko kiingereza.wakati mwingine unakosa neno zuri la kiswahili,lakini tazama, kuna neno zuri sana la kiingereza lipo ambalo ukilitumia,basi ujumbe unafika pasipo shaka sasa?kwa nini nisilitumie? Makosa makubwa tunayofanya ni kutumia kiingereza wakati hao tunaowasiliana nao wengine hawakijui. Samahani labda niseme hivi mfano: Unaongea kihaya mbele ya watu wakati baadhi yao hawakijui.
  Kwa hiyo jamani tuwe makini tunapotumia lugha hii ya kigeni.
   
 7. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  mie nimemaliza chuo kikuu na bado sijui kiingereza...na nimefaulu vizuri sanaaaa masomo yangu nilosomea....NDIOOO...kwa sababu sikusomea degree ya lugha ya kiingereza....yesss..najivunia kumaliza chuo kikuu bila kujua kiingereza.

  turudi mitaani tunakoishi na kukutana na watu 40m...wanaojua kiingereza hawafiki 1m...wewe unayejua kiingereza bila hiyo lugha ya watu 39m unajisikiaje??

  Huu utumwa wa serikali yetu kungangania kiingereza mpaka inafikia hatua tunaingia mikataba ya kiingereza tunauza nchi kisa hatujui hiyo lugha NI UJINGA DARAJA LA KWANZA.
   
 8. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wewe sio msomi, ila ni mzuri kwa kukariri n a kuandika ulishokariri bila kuelewa. haiwezekani ukawa haujui kimombo ukaelewa masomo yanayofundishwa kwa kimombo. ndio watu wengi sana tunao hapa bongo, na ndio mojawapo ya uwoga unaofanya watz wawaogope wakenya, wafeli interviews, wawe inferior kwa mataifa mengine, kwasababu hawajiamini wanaopongea, kimombo kimewapita. wewe ni mfano mzuri sana wa wabongo wengi tulionao madarakani na kwenye maofisi. mambo wanayoyafanya huko kwenye docs maofisini ni n madudu, and they are not competitive kulinganisha na mataifa mengine.
   
 9. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Mkuu huyo mtu alipataje degree huku akijibu maswali kwa kiswahili...sijui unanielewa! ninamaana hakuna mtu nchi hii aliemaliza chuo kikuuuasiejua kiingereza niongo, kinachotokea ni kuwa hawezi kuzungumza kiingereza moja kwa moja sababu hakitumii katika mazingira yake yote....lakini kusema akisemes kwa kiingereza hataelewa sikubali....
  Kingereza siyo usomi! kuna ndugu yangu mmoja anajua sana kiingereza hata sijui alijifunzaje! lakini ameishia darasa la sabatu...akija ofosini kwangu mapokezi anaongea kiingrereza tu watu wa nmheshimu mno wanadhani kasoma sana!!! lakini amini usiamini hakuna kazi anayoifanya zaidi ya kuombaomba!
   
 10. G

  GodHaveMercy Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisikia 'kutawaliwa kifikra' ndio huku. Sijui wabongo tukoje...!? Ndivyo ilivyo hata huku mtaani kwetu, ukipiga maneno mawili matatu ya kimombo, basi macho yote kwako. Wanakuona ndio msooomi. Kujua lugha flani ni sehemu tu ya ujuzi na si kila kitu. Ni kweli kuwa Englsh iko juu sana na ni muhimu hasa ktk hiki kipindi cha utandawazi, lakini si kivile kama tunavyochukulia sisi. Maana imekua kama 'tunaitukuza' hiyo lugha kiasi cha kuwashusha wenzetu ambao lugha hii imewapa kisogo.

  "KINYAMWEZI IS LIKE DELICIOUS FOOD TO MY TONGUE!"
   
 11. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,906
  Likes Received: 21,007
  Trophy Points: 280
  nafikiri unakubaliana na mimi kimsingi,unatumia kiingereza kusoma halafu uwe hujui kiingereza!utasoma vipi?umesema hakuna anaemaliza chuo asijue kiingereza,tuko pamoja.
  namimi nimesema HUWEZI KUTENGANISHA KIINGEREZA NA USOMI MPAKA TUTUMIE KISWAHILI KUFUNDISHIA HADI CHUO KIKUU.
  nikisema hivyo sina maana kila anayejua kiingereza ni msomi bali kila msomi lazima ajue kiingereza.
   
 12. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,906
  Likes Received: 21,007
  Trophy Points: 280
  kila msomi lazima ajue kiingereza lakini sio kila anaejua kiingereza ni msomi
   
 13. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,906
  Likes Received: 21,007
  Trophy Points: 280
  no comment.
   
 14. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ...yadda yadda yadda...
   
 15. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ninakubaliana na wewe mmbebabox.

  Msomi anawejuwa kiingereza lakini hakitumii kama mmoja wetu hapo juu alivyochangia. Ni utumiaji tu ndio unaotofautia. Mtu amemaliza chuo kikuu na amefaulu vizuri tu lakini hawezi kuongea kiingereza katika kupiga story.

  bana Ni wengi tu tumemaliza chuo kikuu lakini kiingereza chetu ni cha hapa na pale. Maisha yanaenda maana mtaani tunapiga kiswahili kwa kwenda mbele.....
   
 16. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mkienda kwenye interview siku hiyo neno zeeee zeeee zeee ndo linachukua hatamu.
   
 17. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Ukubali ukatae bila kujua kingereza (Ngeli) unakuwa tatizo kubwa mno, fanya ufanyavyo ndugu yangu kama una watoto jikamue waanze kujua lugha hii mapema. just imagine hawa maafisa masoko wa makampuni makubwa unafikiri wana shule za ajabu basi - longolongo tu za kingereza wengi wao wamesomea huko huko wakaja kuchukua postions sababu wanaweza kuwakilisha kinachotakiwa na waajiri wao kwa lugha zote (Swahili na Kiingeleza). Matumizi ya Kiingeleza bado yapo juu sana 80% naweza kusema.


  Binafsi huwa naingia kwenye interview panel, mtu anakuja na Masters toka Mlimani - kujieleza anashindwa ukizingatia panel inaongozwa na wamarekani basi m-bongo anabakia kuchanganyikiwa - kuna siku nilijaribu hata kuongea nao nikawaambia wasi panic wajieleze vizuri tu kwa kiingeleza fasaha lakini inakuwa kigugumizi kitupu sasa kampuni ya kimataifa itakuchukuaje wewe hata kujieleza huwezi? option inakuwa wachukue hata mkenya mwenye degree ya kwanza ila longo longo kibao.

  Wabongo hii lugha inatuadhibu -inatunyima fulsa nyingi sana za soko la ajira.
   
 18. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sasa kama hata walimu wenyewe kingereza wanababaisha utaacha kufaulu?
   
 19. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kiingereza ni njia ya mawasliano tu na haipimi usomi au ukipanga wa mtu. Wasomi wa Tz wanapaswa kusoma through Kiingereza hivyo inabidi afanye mawasiliano ya kisomi kwa lugha hiyo. Iwapo mtu kasoma hadi University kwa kutumia hiyo lugha na leo hii hawezi kujieleza au kuwasilian kwa media hiyo tunamwaona kama hiyo shule yake ilikuwa ya kubabaisha au ni hesabu tupu. Huwezi kufaulu economics , Law , biology etc kama hiyo lugha inayotumika huiwezi. Ndio maana utaonekana kama sio msomi vile. There is a very close relationship between your proffession and the language you used to get it . Ni vigumu kwa mchina kufaulu masomo ya kiingereza kama hajui kiingereza lakini akifaulu ujue ataongea kiingereza balaa.
   
 20. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2010
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 615
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 35
  kwanza tujue usomi ni nini?ili kuepuka mkanganyiko wa maana ya usomi tuchukulie katika hali ta wepesi maana ya usomi hapo tutatambua kwamba kwa tanzania kiingereza ni kipimo cha usomi ikiiambatana na sifa zingine..thats why hata katika nafasi nyingi za kazi wanahitaji mtu aliye fluent in both english and kiswahili.
   
Loading...