Kumekuwepo na hoja humu jamvini juu ya uhalali wa muungano wetu, mwenendo wake na ushiriki wa wananchi toka pande zote!
Ndugu zetu wa upande wa visiwani inaonekana kama vile tunawalazimisha kukubali/kurejea makubaliano ya uwepo wa taifa letu hili.
Licha ya mapungufu na kero za muungano kama tuzishuhudiazo ukweli utabakia kuwa waasisi wa nchi hzi mbili walifanja jambo lile kwa nia njema!
Ndugu zetu wazanzibari hawataki kuitwa WATANZANIA na wanafanya juu chini kuukwepa utanzania huu. Kwao UZANZIBAR ndio kipaumbele chao, wanaamini pasipo TANZANIA (Bara) wangekua mbali kimaendeleo.
Well, mimi asilia yangu ni TANGANYIKA na huu UTANZANIA ni jina tu tuliojipa kwa nia njema kwa lengo la kuonyesha Umoja wetu, bt kwa kua wao ni WAZANZIBAR nadhani niwakati sasa kwa mimi kuutukuza UTANGANYIKA WANGU.
MIMI NI MTANGANYIKA, UTANZANIA WANGU WA SASA NI JINA LA MPITO TU!