gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,305
- 3,327
Naomba kukumbushwa kwani aina hii ya magari ni miongoni mwa magari ambayo si tu ya thamani kubwa bali hata gharama za uendeshaji ni kubwa mno.Inasemekana gharama za uendeshaji wa V8 moja kwa mwaka ni zaidi ya 100ml.
Tunaambiwa vipuri vya magari haya bei yake ni kubwa mno pale inapotokea vimeharibika.
Kuna kipindi Mh Mbowe alionesha uzalendo wa hali ya juu alirudisha hili gari(KUB) lakini badae kukatokea uvumi alikata shauri nakulirudia tena kwani mwanzo alilirudisha kwa pressure kutoka kwenye chama lakini yeye alikua bado analipenda.
Wakati fulani mh Pinda nae alifurukuta kuishauri serikali iachane na matumizi ya haya Magari lakini alichemka.
Usitishwaji wa matumizi wa haya magari ni jambo la msingi sana hasa katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inanyimwa misaada na nchi wahisani.
Kwa mwenye kufaham naomba kujulishwa kwa faida yangu na wanajukwaa wengine.