Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,887
Pamoja na kuwa swala la Tume Huru ya Uchaguzi kuwa ni swala la kikatiba zaidi,je haiwezekani kutumia vifungu vya katiba hii ya sasa na sheria ya uchaguzi pamoja,sheria ya Tume ya Uchaguzi na sheria ya nyingine kujenga hoja Mahakamani ya kudai uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi?
Hoja yangu hapa ni kuwa,kwa kutumia katiba hii inayotambua uwepo wa vyama vingi,sheria ya uchaguzi pamoja na sheria ya tume ya uchaguzi haiwezekani kujenga hoja kuwa sheria hizi mbili yaani sheria ya uchaguzi na sheria iliyounda Tume ya Uchaguzi vinakinzani na katiba inayotambua uwepo wa vyama vingi kwa hoja kuwa sheria hizi mbili hazitoi fursa sawa kwa vyama vya upinzani kushindana kwa usawa na chama tawala?
Kwa mfano,haiwezekani kujenga hoja kuwa katiba inatambua uwepo wa vyama vingi,lakini sheria ya uchaguzi bado inawatambua Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ni wateule wa Raisi(kada wa chama) kama wasimamizi wa uchaguzi,sheria ambayo katika mfumo wa vyama vingi haifa na kwamba sheria hii ilifaa wakati wa mfumo wa chama kimoja na si sasa na hivyo sheria hii inakwenda kinyume na katiba ya nchi inayotambua mfumo wa vyama vingi?
Hoja nyingine haiwezi kujengwa kwa kutazama sheria ya uchaguzi inayopinga matokeo ya uraisi kuhojiwa Mahakani wakati kutafuta haki Mahakamani ni haki ya kikatiba na Mahakama zipo kwa mujjibu wa katiba?
Hoja nyingine ya kujenga mahakani haiwezi kuwa ni katika mfumo wa vyama vingi ni kutotenda haki kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzj kuteuliwa na Raisi anaetokana na chama kimojawapo cha siasa na hivyo sheria hii haifai katika mfumo wa sasa wa vyama vingi unaotambuliwa na katiba?
Ukiacha swala la Tume Huru ya Uchaguzi, mchakato wa kuendelea na kura ya maoni nao hauwezi kudaiwa kupitia mahakamani?
Kwa hapa tulipofika kama nchi,ni bora tuende kwenye kura ya maoni ili tupate katiba mpya inayotambua uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi alafu tukifanikiwa kushinda uchaguzi na tukaingia madarakani basi tunaweza kubadili vipengele vya katiba ambayo vinakwenda kinyume na maoni ya wananchi waliyoyatoa kupitia Tume ya mzee Warioba tofauti na hapo tunajidanganya.
Mimi si mwanasheria wala mtaalamu wa mambo ya katiba ila sidhani kukosa sifa hizo kunaniondolea uhalali wa kutoa maoni haya hivyo naomba wataalamu watusaidie.
Ya Dodoma tuwaachie wenyewe sisi tu-focus ni namna gani tunaweza kuchukua nchi kupitia sanduku la kura vinginevyo tunapoteza muda tu.