Hivi JamiiForums tunge-expose real ID zetu tungeondoka wangapi?

Kinachotusadia ni kwamba hakuna anayenijua jina langu halisi na wengi siwajui.

Hivi kila mmoja wetu angekuwa analazimika kuonekana ID yaani jina lake halisi na mahala unapokaa, hivi tungebaki salama kweli?

Au yangekuwa ndiyo yaleyale ya kuitwa na polisi watatu halafu unatokomoea kusikojulikana na kesho yake unakutwa mtaroni kama ilivyotokea kwa Robert Ouko kule Kenya.


CCM inaiga utawala wa kinyama wa KANU; kuwaletea askari na Upotea Unaokotwa Vichakani
 
acheni woga, huna impact yoyote kwa harakati za kwenye keyboard, go out there and do something real ndio uanze kuhofia usalama wako. Kuficha id ni woga wa kijinga, kwa teknolojia hii watu wakitaka kukutafuta wanakupata tena haraka mno.

Kwani Kubenea aliyeponea chupuchupu kupofuliwa anakwenda mtaani? Si anatandika article zake kwenye keyboard kama sisi, au wewe unaelewaje?
 
ah ah mdau hujatumia jina lako sema kwe registration umeweka email yako unayotumia hadi ofisin kwahiyo wakitaka kukuhack ni sekunde tu...cha umuhimu ni kujiamini na kusimama katika ukweli kwani itakuweka huru
 
wangetumaliza walahi,serikali ya kidikteta huwa haipendi kuambiwa ukweli wala kusahihishwa,wangetumaliza

kweli? Ya kidikteta ingeshindwa kukusaka kwa id hiyo ya massai? Kumbe uhuru nao unalevya ee?
 
Last edited by a moderator:
kinachotusadia ni kwamba hakuna anayenijua jina langu halisi na wengi siwajui.

Hivi kila mmoja wetu angekuwa analazimika kuonekana id yaani jina lake halisi na mahala unapokaa, hivi tungebaki salama kweli?

Au yangekuwa ndiyo yaleyale ya kuitwa na polisi watatu halafu unatokomoea kusikojulikana na kesho yake unakutwa mtaroni kama ilivyotokea kwa robert ouko kule kenya.

hivi ndivyo unavyojidanganya kuwa hujulikani kwa id yako mkuu?!!! Usijidanganye ndg yangu unajulikana sana! Cha maana kama 'bold spirits' wa humu ndani walivyochangia uzi huu hakikisha unakua sure and or innocent na kauli zako tu! Maana believe me mecenaries are @ work!
 
ah ah mdau hujatumia jina lako sema kwe registration umeweka email yako unayotumia hadi ofisin kwahiyo wakitaka kukuhack ni sekunde tu...cha umuhimu ni kujiamini na kusimama katika ukweli kwani itakuweka huru

Aisee, wengine michezo ya email tulianza zamani kabla hata Jamii Forum haijazaliwa. Kamwe sitoi real identity yangu na hivyo email yangu halisi sitoi.

Ninachofanya ninatunga email ya ajabuajabu na kamwe hawataijua na hata hivyo siangalizii mails au JF mahala pamoja.
 
Wangetumaliza walahi,serikali ya kidikteta huwa haipendi kuambiwa ukweli wala kusahihishwa,wangetumaliza
yaani mkuuu hata kwa majina yetu haya bado napata wasiwasi maana sikumbuki wakati najisajili niliandika nini labda nipate uhakika wa usalama kutoka kwa mods
 
Wacheni kujidanganya ! system ikiwataka ni kupepesa jicho! tunajua location zenu zote kupitia network ya internet! endeleyeni na matusi uchochezi dharau na uwongo uso kipimo lkn hii ndio demokrasia!
 
hizi fake ID zetu zinaiumiza kichwa sana taasisi ya UWT ya magamba.na kama tungeji-expose kwa majina yetu halisi kama tufanyavyo kule FB na twitter tungeshapotea.JF fake ID forever...
 
Kinachotusadia ni kwamba hakuna anayenijua jina langu halisi na wengi siwajui.

Hivi kila mmoja wetu angekuwa analazimika kuonekana ID yaani jina lake halisi na mahala unapokaa, hivi tungebaki salama kweli?

Au yangekuwa ndiyo yaleyale ya kuitwa na polisi watatu halafu unatokomoea kusikojulikana na kesho yake unakutwa mtaroni kama ilivyotokea kwa Robert Ouko kule Kenya.

Hawana shida na watu wanaorusha madongo tu na kuishia hapo,wanashida na watu wanaowalaza macho kama kina Ulimboka.

Ingekuwa wana shida na jf wasinge hangaika na wachangiaji wange deal na Wamiliki/Waanzilishi wa jf na ,sio member mmoja mmoja.
 
Wangetumaliza walahi,serikali ya kidikteta huwa haipendi kuambiwa ukweli wala kusahihishwa,wangetumaliza
Mimi naitwa POWER GEORGE naishi Msoga kijijini - nyumba ya tano toka nyumbani kwao DHAIFU na picha yangu ndiyo hiyo hapo juu. Mwenye kutaka kuni-Ulimboka namkaribisha, niko tayari.
 
Kusingekuwa na kuuliwa wala nini, sema uoga ndio unasumbua wengi, bali kwangu mimi uoga ni mwiko, kiongozi akikosea anakosolewa tu bila kujali cheo chake maana
Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu, bali wenye haki ni wajasiri kama simba.
 
eleweni kuwa kitendo cha kuingia mtandaoni tu tayari wewe si salama.huwezi kwepa hili hata kama unatumia fake ID.
Kuna kitu kinaitwa IP ADDRESS na IP TRACER & IP TRACKER wanaweza kupata LOCATION na kwa kutumia ramani za google ndio kabisa huwezi kuruka
 
Ni kweli ndg zangu, hata sisi tunaotumia ID na majina yetu, hatujui ni lini tutaokotwa, tuombeeni sana, huwa ninajiuliza hawa jamaa ni lini wataichomoa roho yangu? kisha najipa moyo bado bado. Tunaelewa kuwa tunamshika simba sharubu wakati yy yu macho. OOh..God be with us.

Waambie vijana waache uoga mbona watu tunatumia majina halisi miaka yote pamoja na picha halisi na maelezo yetu yote yapo wazi kabisa kule FB lakini bado tunapeta tu.
 
Back
Top Bottom