Hivi inawezekana kuomba kupunguziwa mahari.?

Kitchetche

Member
Apr 2, 2017
71
77
Kwa wale waliopitia haya mambo na wote mnaojua.
1. Je inawezekana kuomba mahari ipunguzwe!?
2. Usipotoa mahari inakuaje, japo ulisha ahidi utatoa.
Naomba kujuzwa tafadhali, maana nipo kwenye mipango hiyo ila hali ngumu kiuchumi.
 
Kwa wale waliopitia haya mambo na wote mnaojua.
1. Je inawezekana kuomba mahari ipunguzwe!?
2. Usipotoa mahari inakuaje, japo ulisha ahidi utatoa.
Naomba kujuzwa tafadhali, maana nipo kwenye mipango hiyo ila hali ngumu kiuchumi.

1..... Mahari kwa wachaga hawapunguzi kwa kigezo ya kwamba yale sio manunuzi... kigezo cha pil ni kwamba unaweza kulipa kidogodogo


2... lazima ulipe Mahari usipotoa baada ya kuhaidi kutoa ni watakususia mtoto wao
 
Minadaiwa pesa chini ya elf 50 ila sitalipa.
Nimetoka nyingisana mweee..
 
Dogo nadhani umenielewa....Sasa Acha kulia lia njaa. Kama nyapu ina thamani utailipia kiasi kilichokuwa proposed
 
Kila kitu kinawezekana tu, japo itategemeana na utamaduni wao na familia yenyewe,
Wakisha taja Mali mnanafasi ya kuomba kupunguziwa kulingana na mlivyojipanga na hali halisi.
To a kiasi cha Mali unachoweza pia kulingana na taratibu zao angalia je ni kipi cha kuanza nacho, siku hizi watu hawamalizi kulipa mali.
 
ndugu mahari huwa hailipwi yote hata wakisema billioni ni we kubari ila muelewane utalipa kidogo kidogo, wanasema eti kulipa mahari yote kwa pamoja hata kama unauwezo ni dharau kwa wakwe, tatizo huwa linakuja pale mke anapofariki kuna jamii zingine wanagoma kuzika hadi umalizie mahari yao!
 
Kwa wale waliopitia haya mambo na wote mnaojua.
1. Je inawezekana kuomba mahari ipunguzwe!?
2. Usipotoa mahari inakuaje, japo ulisha ahidi utatoa.
Naomba kujuzwa tafadhali, maana nipo kwenye mipango hiyo ila hali ngumu kiuchumi.
Huwezi kuacha kutoa mahari ikiwa unahitaji kuoa kwa utaratibu mzuri unaoutaka.

Suala la kupunguza mahari huwezi kwenda kumwambia Baba mkwe wako mtarajiwa ila unaweza ukaongea vizuri na unayetaka kumuoa/kuoana naye halafu akatafuta namna ya kukutetea kwa wazazi wake.

NB: Huwa nasikia watu wakisema kuwa mahari huwa haiishi as long as unaishi na binti wa watu.
 
Nataka nikushauri maana naona wengi wanaokushauri eidha hajalipa mahar wala hawajawahi kwenda hata kumlipia mtu mahar..

Mahar kwanza unajua maana yake?? Nibmalipo ambayo yanalipwa kwa binti ambae anakaribia kufunga ndoaNi utamaduni ulioanza zaman sana toka enzi za mitume na manabii...

Je ni halali kulipa? Ndio ila inategemeana na sehem unayolipa au aina ya malipo unayolipa maada tamadun za makabila ytu zmetofautiana..

Kwanza kabsa kwa mtoto anaeoa,,,hawez kwenda kuongelea mahari kwenye nyumba anayokwenda kuoa,muoaji sio muhusika wa kupatana mahari na wazaz wa binti,,kijana wa kiume anaweza chagua mzaz,mjomba au ndugu wa karibu anaejua tamadun ya sehem husika kwa ajili ya kwenda kuongelea mahar wanayotaka kulipa kuhusu binti yao,lakin wanaokuambia hapa kua unaenda kuongea nao wakupunguzie wanakosea kwa maana ya kwamba wewe sio jukumu lako kwenda kupanga nao bei... Wakubwa zako au wazaz ndio wenye jukumu hilo,,sasa unataka kwenda kama we nani?? Wale wanakuletea taarifa bwana mdogo wamesema milion na wewe unaweza kuwaomba waombe ukwen kwako wapunguze aidha mpka laki moja mbili au tatu ndio uwezo wako na wana haki ya kukubali au kukataa vile vile,wakikubali sawa unaweza kutanguliza kias kidogo kingine ukadaiwa inaruhusiwa..kama unayo unalipa yte hakuna sheria au taratibu inayozuia kulipa yte kama upo vzr.

Nakuambia sababu wengine wanahitaji aidha mnyama au hela cash,,na wenzetu waisilam nasikia wao mwanamke ndio anatamka mahar sijajua kama ni hivyo kwel au lah. Na kuna makabila mengine hata wazaz wa mwanamke hawana ruhusa ya kutamka mahar zaid ya wajokba na mashangazi wa binti ila ni baada ya kushauriana familia yte kwanza....

So usiogope kijana,ni heshima tu na taratibu ambazo zipo miaka na miaka so tunazifuata na inakujengea heshima kuliko kumchukua tu huko mnapokutana na kuanza kuishi nae.. Pia inakupa heshima kwa mkeo kwamba ulinifata home,ukanilipia mahar na umenioa...

Wengi wanaozinguaga ni wale walioamua kuishi tu ilimrad ambapo hata ugomv ukitokea kati yenu inakuwa ngumu kwenda kwa washenga kushtaki maana umeokotana huko mlikokutana... Poa dogo baadae kapambanie utamu wako mapema na mvua hizi bas unagegeda tu kila siku ..
 
1..... Mahari kwa wachaga hawapunguzi kwa kigezo ya kwamba yale sio manunuzi... kigezo cha pil ni kwamba unaweza kulipa kidogodogo


2... lazima ulipe Mahari usipotoa baada ya kuhaidi kutoa ni watakususia mtoto wao
Si kweli mahari inapunguzwa,tumetoka machame juzi tu ,tumebargain kila list yao.Mpaka mbege tumepunguza *****
 
Weweeee Tanzania hakuna kitu kinachoshindkana, Hata liwe kabila Gan ilimrad liwe Tanzania, Watakubali tuu, We wape hata nusu kwanza Hio nyingne unaweza watumia hata Kwa TIGO PESA its Possible ONLY IN TANZANIA
 
Back
Top Bottom