Hivi inakuwaje mtu anagawa namba ya mtu bila ridhaa ya mhusika?

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
59,410
119,112
Habari wanaJf
Kichwa kinajieleza, hivi hii tabia ina maana gani? Kwa kweli haipendezi hata kidogo, dada yangu Karucee huwa amezoea kusema 'Jf is a jungle, tread carefully'... Kwamba ni lazima uwe makini, si lazima kila anayetaka kujuana na wewe unampa access, lazima uwe selective hata kama imetokea umeinteract na mtu ambae si mwema iwe ni kwa bahati mbaya na sio Jf tu hata katika maisha ya kawaida.

Siku za nyuma kidogo nilipokea messages kutoka kwa watu nisiowajua lakini baada ya kuhojiana nao niligundua ni wanajf wenzangu, katika kumuuliza mmoja mmoja namba yangu mmepata wapi nikatajiwa watu ambao mimi sijawahi kuwapa namba yangu kwa kweli nilishangaa halafu nilikwazwa...naomba nieleweke kwamba kilichonikwaza si wale watu kuwa na namba yangu maana ni watu wema tu wenye heshima zao kwa nje, kuhusu utu wao wa ndani siwezi kujua.

Kilichonishangaza ni mtu kutoa tu namba ya mtu kama vile ya kwake . hum ndani bwana ni kichaka huwezi kujua nani na nani wana uhusiano gani,wengine wapenzi,wengine ma ex, wengine wakewenza, wengine wachawi n.k kwa hiyo unapokuwa unatoa mawasiliano ya mtu hujui yule unayempa ana nia gani na huyo mhusika.

Mtu anapoamua kukupa mawasiliano amekuamini wewe na hata kama ameamua kujilipua amejilipua kwako kwa sababu anazojua yeye na anaona kuwa ni za msingi kwa hiyo please naomba tuheshimu privacy za watu. Kama kwako wewe mawasiliano ni suala jepesi tu sio kwa kila mtu lakini nadhani hata kwenu ipo hivyo maana sijawahi kuona mtu anaweka ovyo ovyo namba kwenye thread.
Ni hayo tu kwa leo
#nohardfeelings
 
Daah ila ni hatari sana.
Nawaza tuu.. Mtu ampe mtu namba yangu ...kumbe anayempatia ni Mume au mtu ambaye tunajuana nje ya jf...namaanisha anayo namba yangu kwenye contact Yake.
Nikimaliza kuwaza nitarudi.
 
Ni ushamba tuu...kama ulivyosema wengine humu vigagula yani wanga si kidogo wanaroga kweupe na halikadhalika wema wapo wa kutosha vilevile humu..lakini si busara hata kidogo kueneza privacy ya mtu,.bora mwema anaweza kukuombea kheri na fanaka,.kigagula sasa woiii utaota unakimbizwa kama mwehu kila siku... (kidding)
#nohardfeelings#
 
Haha hatari sana aisee
Ni ushamba tuu...kama ulivyosema wengine humu vigagula yani wanga si kidogo wanaroga kweupe na halikadhalika wema wapo wa kutosha vilevile humu..lakini si busara hata kidogo kueneza privacy ya mtu,.bora mwema anaweza kukuombea kheri na fanaka,.kigagula sasa woiii utaota unakimbizwa kama mwehu kila siku... (kidding)
#nohardfeelings#
 
Back
Top Bottom