Alianza kwa kuimba kabla ya kuwaandikia na wimbo wake ulikuwa mzuri na bado nyimbo zake ni nzuri sana.
Kuandika nyimbo Tanzania hakulipi ebu fikiria kama Nandy na Aslay walikuwa wamewapatia Tshs 300,000 waimbaji wa wimbo wa Subakheri ili waurudie na kuptia huo wimbo wao wakapiga show kibao wakapata deals za ubarozi na makampuni kibao si unyonyaji huo. Japo baadae kundi liliwageuka kuwa ule wimbo ni wa kundi si wa waimbaji inasemkana waliongeza mzigo ukafika milion na point lakini bado ni ndogo.
kama watayarishaji mziki wanatengeneza hits lakini bado hawana ela ebu fikiria mtu kama Esto keys sijui nimepatia jina, nilishangaa anasema studio yake ya mziki aliyoifungua kajibana sana ametumia ela nyingi sana kakusanya sana kiasi cha milion8, nikajiuliza huyu mtu katengeneza hits kibao yani ukisikiliza ngoma 10 ambazo ni hit kwa sasa hukosi nyimbo zake 5-6 inabidi awe na ela nyingi tu.
Waandishi hawapewi ela unakuta wanaandika tu kishikaji au bure kabisa, Marioo juzi ndipo kasema ameacha kuandika ila tu kwa makubariano kama mtu anataka amwandikie mfano wakubariane huu wimbo utakula show na kwingine mimi niachie ela ya caller tune na vitu kama hivyo lakini wasanii hawataki kusikia hizo habari.
Wasanii wanalalamika wananyonywa ila nao wanawanyonywa ma producer na waandishi. Marehemu Pancho alisema B-hits iliacha kuhit baada ya wasanii kutangaziwa kuwa kwasasa itabidi walipe hawafanyi tena nyimbo kishikaji.