Hivi huyu alikula kiapo kweli??

Black BackUp

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
685
625
Unaanzeje mtu tu from nowhere unakaa baa/kwenye kadamnasi na kujitangaza kua wewe ni Afisa usalama/Usalama wa taifa lengo lako hasa ni nini?
watu wakuogope wakuache peke yako waone mchomoa betri kaingia? Au unataka unywe uondoke bila kulipa? Kama uliapa ndugu,uliapa kitu gani? Nini maana ya kile kiapo "Mungu nisaidie" . Hebu acheni mambo yenu bwana, msitutishe.
 
Mambo ya kwenye bar sio yote unachukulia serious mengine ni pombe na sifa tu. ata wewe unaweza kujiita Afisa usalama wa familia yako mbona simple Tu
 
Siku hizi hata boss mkuu anawatambulisha hadharani... Ni mwendo wa kutishana tu.
 
We unaamini kwenye kiapo? watu wanaapa ili wapate kazi tu.
Wanakula kiapo chote hadi kinaisha kwenye sahani. Baada ya hapo hakuna kinachowatia hofu tena kwenda kinyume na hicho kiapo kwa sababu ulaji wake umekuwa ni kama formalities tu kwa walishaji na walaji wa hivyo viapo katika ngazi zote. Watazamaji tunabaki tukijifariji kwa kusema "Mungu anawaona" au"malipo ni hapa hapa duniani" huku wao wakizidi kusonga mbele.
 
Unaanzeje mtu tu from nowhere unakaa baa/kwenye kadamnasi na kujitangaza kua wewe ni Afisa usalama/Usalama wa taifa lengo lako hasa ni nini?
watu wakuogope wakuache peke yako waone mchomoa betri kaingia? Au unataka unywe uondoke bila kulipa? Kama uliapa ndugu,uliapa kitu gani? Nini maana ya kile kiapo "Mungu nisaidie" . Hebu acheni mambo yenu bwana, msitutishe.
Anaweza kuwa Afisa Usalama wa taifa la Kenya, taifa si Tanzania tu.
 
Ww pia ukilewa ukijiita afisa usalama utakuwa kweli usalama story za walevi hizo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom