GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Unajua kabisa tena fika kuwa umeondoka kwenu kuja kuungana na Mimi ili tuendeleze Ukoo na tupate faraja lakini matokeo yake sasa umekuja kuishi na Mimi ni Karaha tupu.
Hasira nilizonazo naomba hata Mungu hii Mimba ya Mke wangu iharibike hata sasa hivi ili nipumzike na haya mateso.
Mke wangu ana ujauzito sasa wa mwezi mmoja tu lakini naona ikifika mwezi wa tatu ( 3 ) nitabaki kama chelewa kwa kukondeana.
Ifuatayo ni orodha ya Kero zake za Kimatukio kwangu:
Humu kuna Wanaume wenzangu wenye Wapenzi wenu jamani naomba kuwaulizeni hivi na nyie mnapata " majaribu " haya kutoka kwa Wapenzi wenu pindi " mnapowajaza " mimba? Yaani sijui nini kilinifanya nimtongoze na nimpe ujauzito huyu Mwanamke kwani ni Kero na amenikera mno na naomba mnisaidie tu niitoe hii mimba yake ili nipumzike au nivumilie tu na haya Mazoezi ya Kijeshi ya Uvumilivu yasiyo na Cheti cha kutunikiwa?
Msaada tafadhali.

- Jumatatu iliyopita kanituma Mayai ya Kwale nimeyatafuta hadi karibu na Chalinze na kurudi usiku wa Saa 5 nafika nyumbani ananiambia hayataki ( Mwanaume nikamvumilia )
- Jumanne iliyopita kanituma nimtafutie Gazeti la Udaku ambalo lilikuwa na Stori ya kimbea mbea ambayo aliitaka kuijua na ikabidi nidanganye Ofisini ili nilitafute ambapo nakumbuka nilitembea karibu jiji zima nikalikosa hivyo ikabidi nisafiri hadi Mkoani Morogoro kulitafuta mchana na kurudi nalo jioni na kunipandisha Hasira nimerudi nalo huku nimechoka ananikunjia uso na anasema halitaki tena na badala yake nimtafutie sasa Gazeti la Tanzania Daima ili asome habari ya Lugumi ( Nisiwafiche hapa alichezea Vibao viwili vitatu na akaishia tu kulala na pengine huyo Lugumi wake alimsoma kwa kumuota ndotoni )
- Jana Jumapili kaniambia twende site Mapinga nikamkubalia ambapo baada ya kupanda Gari la Bagamoyo vizuri tu kutoka Makumbusho tulipofika tu Tegeta kaniambia tushuke nikamuuliza kwanini akasema anajisikia kutapika hivyo nikaogopa asije kuchafua hali ya hewa mule garini na kushuka nae na baada ya kushuka nikidhani kuwa atatapika kama alivyosema kauli aliyoitoa ndiyo iliniumiza na hadi sasa imesababisha nimfanyie nilichomfanya. Namnukuu alichoniambia jana " Mume wangu najisikia kutembea kwa miguu hapa mpaka Mapinga kisha turudi tena na miguu kutoka Mapinga hadi nyumbani kwetu Mbagala Kizuiani ili huyu Mwanao tumboni apate mazoezi mazuri na ya kutosha na kama hutaki Wewe nenda tu niache na nitatembea mwenyewe " mwisho wa kumnukuu.