scofield_PRISON
Member
- Dec 11, 2016
- 88
- 46
Picha: EFM yazoa tuzo nne kwenye Tanzania Leadership Awards
Ni furaha tu kwenye makao makuu ya EFM jijini Dar es Salaam. Kituo hicho cha redio kimejinyakulia tuzo nne katika tuzo za Tanzania Leadership Awards, TLA2016.
Baadhi ya wafanyakazi wa EFM wakiwa wameshikilia tuzo zao za TLA 2016
Vipengele ilivyoshinda ni pamoja na redio bora ya mwaka, kampuni bora kwa ubunifu, kampuni inayokuwa kwa kasi pamoja na tuzo ya mwandishi bora ya mwaka ambayo imekwenda kwa mtangazaji wa kipindi cha Uhondo katika redio hiyo Dina Marios.
Mtangazaji wa kipindi cha Uhondo, Dina Marious alishinda tuzo ya mtangazaji wa redio wa mwaka
Hafla ya ugawaji tuzo hizo ilifanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa Hyatt Regency Hotel – Posta jijini Dar es Salaam, ambapo redio hiyo iliwapatia heshima kubwa wasikilizaji wake kwa kuondoka na tuzo hizo.
Ni mwaka wa pili mfululizo kwa redio hiyo kuchukua tuzo za Tanzania Leadership Awards ambapo tuzo ya kwanza waliipata mwaka jana kwa kipengele cha redio bora ya mwaka.
Ni takribani miaka mitatu sasa tangu redio hiyo ianzishwe na imejipatia umaarufu mkubwa kwa kuutangaza muziki wa Singeli, na kujihusisha na mambo mbalimbali ya kijamii kupitia matamasha,vipindi na kampeni mbalimbali kama vile kupanda miti (mti wangu), kuanzisha vikundi vya mazoezi (EFM Jogging club), kampeni za afya, kuhamasisha jamii kujikita katika shughuli za ujasiriamali, pia kutatua matatizo katika jamii kwa lengo la kujiweka karibu na jamii nzima.
SOURCE:BONGO 5