Hivi Hizi ni Kauli za Kiongozi wa Nchi?

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Salaam wana Jamvi. Katika kuadhimisha miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM,mwekiti mtarajiwa wa CCM rais John Magufuli ametoa kauli zinazowasha masikio akiwa uwanja wa Namfua Singida zilipofanyika sherehe hizo kitaifa.Zilizonishtua sana ni hizi zifuatazo; 1.Yeye ni rais wa CCM na amechaguliwa na CCM 2.Kwamba CCM tu ndiyo yenye haki ya kutawala 3.Kwamba vyama vingine havina haki ya kutawala kwa kuwa ni vya hovyohovyo!
Hizi ni kauli za ajabu hasa kama zimetolewa na kiongozi mkuuwa nchi ambaye Watanzania wote hata wale wasimchagua wanamtegemea kuivusha Tanzania Kwenda nchi ya maziwa na asali.Nikauli hatari kwa demokrasia yetu changa.Kauli hii inaweza kufanana na kauli iliyotolewa na Mh.Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akiwa jimboni kwake Ruangwa Lindi kwamba walioshindwa kwenye uchaguzi hawastahili kufanya mikutano.Kuna dalili za udikteta zinatunyemelea!Mnasemaje?
 
Angalia mazingira aliyotoa kauli hizo, pia tutambue kuwa alikuwa kwenye sherehe za chama pasingekuwa rahisi kusema maneno yasiyoendana na siku yenyewe
kwa mtazamo wangu hayo ndo nimeelewa hivyo
 
mh mimi siwaelewi kabisa viongozi wetu ila wewe waache siku tukielevuka watakuwa mashakani
 
Ndo maana namuunga mkono Trump.. waafrica bado hatujielewi.. ni hatari kufikiria kwamba mtu mwenye mawazo tofauti na wewe ni adui.. la hasha.. Tanzania isingekuwa na upinzani imara hata kwa hicho kiwango kidogo isingefika 2015..

Mtu anayebeza upinzani au fikra mbadala kimsingi ni mtu asiye na vision.. haelewi anachotaka ni nini..

Tukirudi kwa kauli za mkuu.. hakika zinaudhi sana.. lakini kwa sababu anawafunga wote wanampinga, naachia hapa nisijefungwa mie..
 
Back
Top Bottom