Hivi hizi ndondi zitaisha lini?

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,585
3,179
Ndugu zangu,

HIVI HIZI NDONDI ZITAISHA LINI?

Maana mnyukano unaendelea takriban miezi mitatu sasa, kwa kumbu kumbu zangu NDONDI kama hizi sijawahi kushuhudia hapo kabla, wananchi mzuka na Mori ndio vinazidi kupanda, kule kina mweupe ndo kwanza wanatupa mashati wanasema liwalo na liwe anatafutwa mshindi mhhh yetu macho.

Tuliona "Waamuzi wazee wa baraza" wakasema isiwe nongwa malizeni wenyewe sisi tumefungwa mikono,ni kweli nyama imeoza baadhi ya sehemu lakini si yote Ila kuleni hivyohivyo hatuwezi kumwingilia mpishi kwani na yeye kule jikoni ana uhuru wake.

Duh,kusikia hivyo walala hoi wakasema haiwezekani aslan, lazima kazi iendelee,wengine wakasema mdundiko lazima uchezwe nchi nzima,wengine tunaenda kubinuka sarakasi Pele viwanja vya jumba kuu, 😂😂😂 Manyota akasema salakasi jumba jeupe?

Hamnijui njoni huku kwani mneno mliyonena ni Maneno yenye makufuru, tanzi linawahusu. Walala pu kuona hivyo walipiga yowe hiyo sijawahi sikia mwangwi Kama huo maisha yangu yote, majirani wote wakanyanyua shingo na vichwa vyao toka kwenye usingizi wa pono "kunani Tena jiraniiiiiiii" mmh washika pembe wakaona hii noma sasa hata majirani watajua tunapigana tukiwa uchi!

Mara chatu katema mzigo, hhee kilicho nitia simanzi kabla hata windo halijafika home likanena Maneno makuu.

"heli nife nikiwa shujaa kuliko niishi duniani nikiwa dhalili mpambano lazima yaendelee" walala pu "aminaaaaa" kule Nako Hali kadhalika.

Baadae kidogo wazee wa majoho yaliyobarikiwa wakanena baada ya tafakuli na sala ya muda mrefu na hapo ndipo nilijifunza kuwa watu huwa hatujifunzi kutoka kwenye yaliyo tuumiza Jana, ili mradi tu Kuna kipolo baada ya kazi. Kipindi chatu yupo kwenye harakati za kutaka kumeza Yale mawindo wapo watu walishangilia Sana "na wasurubiwe, wauwawe wengine wakilaumu chatu alikuwa amechelewa na Maneno mengine dahari huku wakirukaluka kwa shangwe na ndelemo, ghafla chatu katema windo kweli ningekuwa Mimi ningeona aibu Sana Ila sio hao!

Na sasa wamewavaa Hawa wazee wa majoho yaliyo barikiwa nongwa Nini? hawazipendi zile karatasi pendwa.

Mi niseme tu kuwa ifike wakati sasa tumalize ugonvi huu tutauwana Bure na sisi ni ndugu.

Leo nikamshukiru Mungu, mama wa kaya kanena acha tugombane Ila tukumbuke jambo moja tu tukimaliza ugonvi atakuwa ameivisha biriani la kutosha tutakaa tutakula pamoja na hapo ndo tutajua sisi ni ndugu hamna wa kututenganisha.

Mbarikiwe Sana.
 
Watanzania hawajaridhika na mkataba wa Bandari yake Salama. Serikali isione aibu kuachana na Waarabu.

Tunaposema Bandari Imegawiwa, maana yake Imegawiwa, tena bure. Wadau wanaodai kuwa kuna rushwa zinanuka kwa kugawiwa Bandari zetu kwa wajomba, maana yake Rushwa inanuka.

Hivi vijisababu na hoja mbovu mbovu walizozitoa na wanazoendelea kuzitoa baada ya kushurutishwa kuhusu mkataba huu, havina maana yeyote ile. Ni uwongo kutaka kuhalilisha Udhalimu na Ufisadi unaotumika kumleta Mwarabu kuja kututawala.

Pinga udhalimu, maangamizo, Ukoloni mamboleo na ufisadi unaofanywa dhidi ya Watanzania,Watanganyika na Wamasai wa Taifa hili kwa nguvu zako zote. Wakemee Vibaraka wote wa Waarabu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom