Hivi hii barabara ya kuelekea Rusumo na Kabanga boda hamuioni?

Ksuley

JF-Expert Member
Dec 18, 2015
1,166
445
Habari ya asubuhi wanajamvi!

Jamani hali ya barabara hii ya kuelekea Rusumo na Kabanga boda, hali ni mbaya mno! Imejaa mahandaki tupu.. Yaani kuanzia Nyakanazi njia ya Kigoma kwenda Mzani wa Nyakahura kuelekea njia panda ya Ngara - Kabanga na Benako hadi Rusumo Boda, haifai kwa matumizi ya magari kabisa, ni hatari mno!

Magari yanaanguka hovyo kutokana na mahandaki yaliopo barabarani. Wafadhili wametujengea ofisi nzuri mno pale Rusumo Boda, lkn barabara inayoingia hapo mahandaki tupu!

Je, wahusika hawaioni hii barabara? Je, kwa hali hii ndio tunahitaji ufanisi kwa bandari yetu, ikiwa gharama za kusafirisha mizigo au magari (it) ni kubwa kutokana na ubovu huo!?

Wahusika wawajibike kwa barabara hii ni hatari!
 
Kwan ule ujenzi wa hiyo barabara kuanzia uliishia wapi?Mara ya mwisho nimepita huko ujenzi ulikua unakaribia nyakanazi.
 
Ni kweli mkuu mimi wiki jana nimepita huko nikiwa naelekea bukoba, hadi nikauriza mbona tunatumia njia ya mchepuko kwa muda mrefu hivi?wakanishangaa,kumbe tupo njia kuu!!!ile barabara haifai kabisa.
 
Mkuu mie nimeshiriki kujenga hiyo njia ila tumeishia Nyakanazi,afu hapo nyuma kuna kipande kilirukwa tokea Sehemu moja inaitwa Runzewe(shamba la bibi) hadi Nyakanazi,ila kuanzia hapo nyakanazi rusahunga nakuendelea hadi Rusumo haifai mkuu
 
Uko Sahihi Kabisa Mkuu!!
 
Mkuu mie nimeshiriki kujenga hiyo njia ila tumeishia Nyakanazi,afu hapo nyuma kuna kipande kilirukwa tokea Sehemu moja inaitwa Runzewe(shamba la bibi) hadi Nyakanazi,ila kuanzia hapo nyakanazi rusahunga nakuendelea hadi Rusumo haifai mkuu[/
Ni kweli mkuu,niliona kutoka nyakanazi mpk lusaunga Kuna mashimo ya hatari,makubwa balaa,gari zinayumba ile mbaya.nadhani magufuli alipita huko wakati wa kampeni,ataifanyia kazi.
 
Nyie wakimbizi pelekeni hiyo post kwa kagame
Lakini kiuchumi inatusaidia kupata faranga zao ikiwezekana tuifanyie mambo ili iweze kuleta mapato zaidi... Tunaihitaji kila senti ya Kagame inayoweza kuingia kibindoni mwetu
 
Ili iweje kama kodi yenyewe wanakwenda kugawana bank kwa mabox na rumbesa na wanasema sio za umma
Lakini kiuchumi inatusaidia kupata faranga zao ikiwezekana tuifanyie mambo ili iweze kuleta mapato zaidi... Tunaihitaji kila senti ya Kagame inayoweza kuingia kibindoni mwetu
 
Mkuu mie nimeshiriki kujenga hiyo njia ila tumeishia Nyakanazi,afu hapo nyuma kuna kipande kilirukwa tokea Sehemu moja inaitwa Runzewe(shamba la bibi) hadi Nyakanazi,ila kuanzia hapo nyakanazi rusahunga nakuendelea hadi Rusumo haifai mkuu
Sasa mbona hujatoa sababu ya msingi kwanini iko vile?Zaidi umerudia kuandika yaleyale!!
 
Mkuu mie nimeshiriki kujenga hiyo njia ila tumeishia Nyakanazi,afu hapo nyuma kuna kipande kilirukwa tokea Sehemu moja inaitwa Runzewe(shamba la bibi) hadi Nyakanazi,ila kuanzia hapo nyakanazi rusahunga nakuendelea hadi Rusumo haifai mkuu
Shamba la nini?kuhusu barabara wanajaribu ku repair naona kama ndo wanaharibu kabsaa.
 
Habari ya asubuhi wanajamvi!

Jamani hali ya barabara hii ya kuelekea Rusumo na Kabanga boda, hali ni mbaya mno! Imejaa mahandaki tupu.. Yaani kuanzia Nyakanazi njia ya Kigoma kwenda Mzani wa Nyakahura kuelekea njia panda ya Ngara - Kabanga na Benako hadi Rusumo Boda, haifai kwa matumizi ya magari kabisa, ni hatari mno!

Magari yanaanguka hovyo kutokana na mahandaki yaliopo barabarani. Wafadhili wametujengea ofisi nzuri mno pale Rusumo Boda, lkn barabara inayoingia hapo mahandaki tupu!

Je, wahusika hawaioni hii barabara? Je, kwa hali hii ndio tunahitaji ufanisi kwa bandari yetu, ikiwa gharama za kusafirisha mizigo au magari (it) ni kubwa kutokana na ubovu huo!?

Wahusika wawajibike kwa barabara hii ni hatari!
Ile barabara ni mbovu hakuna mfano!Kuna kipindi nilikuwa naangalia kipindi cha top gear kilichokuwa kinarushwa na BBC,jamaa mmoja aliye kuwa anaendesha gari akasema :ukiondoa jicho lako barabarani unasababisha ajali.
-Ile barabara unakwepa shimo kwa kuingia kwenye shimo,muda mwingine unaweza ukakosa hata sehemu ya kukwepea ukalazimika kuingia kwenye mashimo.
-Serikali inabidi waiangalie hii barabara maana ni muhimu kwa uchumi wa taifa hili.
 
Uko Sahihi Mkuu, Sasa Hivi Hali Ni Mbaya Mno, Nilipita Njia Hiyo 7Jan.16 Na RUSUMO 8 Jan 16 Nikavuka Kuingia Rwanda!!! Na Nimerudi 11 Jan 16 Na Kuingia Tanzania!! Ilibidi Nilale Nyakahura, Coz Ilikuwa Jioni Na Road Ni Mbovu Mno, Especially Night, Nafuu Mchana, Kwani Mahandaki Yamekuwa Balaa Mno!!! Kwa Kweli SERIKALI ICHUKULIWE Hii Barabara Kama Ni DHARULA, Maana Hali Ni Mbaya Mno, Na MAENEO Ambayo Imeharibika Mno Ndio Utekaji Wa Magari Utokea Mara Kwa Mara!! Na Mengine Ni Milimani, Kama Ilivyo NYABUGOMBE 2!!! Alafu WATANZANIA TUNAJADILI Issues Zetu Za Msingi MSUKULE 1 ANAJITOKEZA Toka Darini, Eti " WAKIMBIZI HIYO POST IPELEKENI KWA KAGAME " Uchoko Mtupu, Nadhani Hata NCHI Inyojadiliwa Haijui, Basi Tu Anapayuka Hovyo!! KAGAME Kidume, Hana Mchezo Kabisa, Barabara Kuu Nyingi Amemaliza Kazi, Now Anapiga Zile Za Michepuko!! Roads Safiii Mno, Lami Kila Kona, ALAFU Msukule ANAJARIBU Kumtolea Mf. Kama Analijua Jiji La Kigali Na Viunga Vyake!!!
 
Habari ya asubuhi wanajamvi!

Jamani hali ya barabara hii ya kuelekea Rusumo na Kabanga boda, hali ni mbaya mno! Imejaa mahandaki tupu.. Yaani kuanzia Nyakanazi njia ya Kigoma kwenda Mzani wa Nyakahura kuelekea njia panda ya Ngara - Kabanga na Benako hadi Rusumo Boda, haifai kwa matumizi ya magari kabisa, ni hatari mno!

Magari yanaanguka hovyo kutokana na mahandaki yaliopo barabarani. Wafadhili wametujengea ofisi nzuri mno pale Rusumo Boda, lkn barabara inayoingia hapo mahandaki tupu!

Je, wahusika hawaioni hii barabara? Je, kwa hali hii ndio tunahitaji ufanisi kwa bandari yetu, ikiwa gharama za kusafirisha mizigo au magari (it) ni kubwa kutokana na ubovu huo!?

Wahusika wawajibike kwa barabara hii ni hatari!
WEka Picha watu waone, ni moja kati ya barbara mbovu zaid hapa tanzania, ni kama vile hakuna mamlaka za kuishighurikia. aibu
 
Labda barabara hiyo haipo Tanzania.. maana zinazojengwa na kukarabatiwa ni za Dar tuu !!!
 
Back
Top Bottom