Hivi haya ni mapenzi au kamati?

manSniper

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
814
679
Nina rafiki yangu wa karibu sana ni wa 90 ni chili wa Arusha ila kizali akahamia Dar na amejenga mjengo wa maana tunaishi sehemu moja mimi kitambo nikihamia apa nimehamia na mke.

Jamaa alikuwa bachela tuliishi vizuri sana kwa heshima sana last year akawa na msichana huyo msichana akaja kudata akahamia msichana ni wa 1987 jamaa ni wa 90 shule ni kawaida sana std7 msichana kapiga education ni ticha wa sec.

Sasa msichana acha ammiliki maela kachukua mkopo kapiga mjengo rangi alafu kampa jamaa akalipe mahari fasta tumeendelea msichana anambana msela juzi kufanya mshikaji kagombana na rafiki yake wa karibu sana.

Dada yake tumbo moja hawasemeshani na nduguye wala mwanamke baada ya kufuatilia tabia za mwanamke alikotoka kumbe msichana alishaishi na mwanaume mhaya akawa anamliki mwanaume jamaa akachomoa.

Sasa hii imekuwa kali jamaa kanieleza wanataka funga ndoa mwezi wa tano hakuna vikao wala nini, leo amekuja mama wa mwanamke wanaenda kutafuta ukumbi wa harusi wanaratibu kila kitu upande wa mwanamke imenishitua sana huyu msichana ana mapenzi ya kweli au ni kamati ya ufundi? Au ni huo mjengo na kiwanja kimemchanganya? Je nimshitue huyu mshikaji au nitaonekana mwanga? Au nikae kimya? Haya ni mapenzi kweli?
 
Hapo ukimwacha huyo jamaa ako ukija kushtuka Unaona manyoya.....keshaliwa mshitue hata ndg mmoja ili ajue halafu yy atazungumza na ndg yake we harusi gan ya upande mmoja cku ya harus Baba wa bwana harusi atatoka wapi?
Hapo kunakekundu bro but take care...
 
Imeeleweka vizuri tu si umeskia ni chali wa Ara,na ni mchizi wa90 pia dem wa 87,hapo ni kwamba hyo ndoa itagongwa expire date na kwa kuwa mchizi ni zober nyumba anaipoteza ndani ya mwaka huu hu baada ya ndoa.Mshauri aoe tu.
 
Nilijua labda ni mimi sielewi uandishi wa huyu jamaa da anauandishi wa kitoto sana.
 
Uandishi wako ni kama mmekaa watoto wavulana kijiweni mnapeana story za uongo na kweli
 
Nina rafiki yangu wa karibu sana ni wa 90 ni chili wa Arusha ila kizali akahamia Dar na amejenga mjengo wa maana tunaishi sehemu moja mimi kitambo nikihamia apa nimehamia na mke.

Jamaa alikuwa bachela tuliishi vizuri sana kwa heshima sana last year akawa na msichana huyo msichana akaja kudata akahamia msichana ni wa 1987 jamaa ni wa 90 shule ni kawaida sana std7 msichana kapiga education ni ticha wa sec.

Sasa msichana acha ammiliki maela kachukua mkopo kapiga mjengo rangi alafu kampa jamaa akalipe mahari fasta tumeendelea msichana anambana msela juzi kufanya mshikaji kagombana na rafiki yake wa karibu sana.

Dada yake tumbo moja hawasemeshani na nduguye wala mwanamke baada ya kufuatilia tabia za mwanamke alikotoka kumbe msichana alishaishi na mwanaume mhaya akawa anamliki mwanaume jamaa akachomoa.

Sasa hii imekuwa kali jamaa kanieleza wanataka funga ndoa mwezi wa tano hakuna vikao wala nini, leo amekuja mama wa mwanamke wanaenda kutafuta ukumbi wa harusi wanaratibu kila kitu upande wa mwanamke imenishitua sana huyu msichana ana mapenzi ya kweli au ni kamati ya ufundi? Au ni huo mjengo na kiwanja kimemchanganya? Je nimshitue huyu mshikaji au nitaonekana mwanga? Au nikae kimya? Haya ni mapenzi kweli?
duu huyo demu umesema kasoma standad 7, afu mwalimu wa sec... ha ha ha we dont fu*k wit u
 
Back
Top Bottom