Hivi hawa wabunge wanajua kweli mwalimu ni yupi na yuko wapi?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
5,067
4,506
Leo ni siku ya bajeti ya wizara ya elimu. Ni muda mrefu nimekuwa nikisikitika kusikiliza mijadala ya wanasiasa kuhusu waalimu. Huwa ninachoka na uelewa wao kuhusu nani ni mwalimu na yuko wapi.

Utawasikia wakisema mwalimu ni mtu mhimu sana, kila mtu amepitia kwa mwalimu lakini mwalimu hathaminiwi - mshahara wake ni mdogo sana, anaishi kwenye mazingira duni sana, na kadhalika na kadhalika!

Utakuta maneno yote hayo kumbe wanaongelea mwalimu wa chekechea, wa shule ya msingi na wa shule ya sekondari. Kumbe kwa uelewa wao hawa ndiyo waalimu na wizara ya elimu inahusu walimu hawa pekee.

Kwao watu kama tutors kwenye vyuo mbali mbali na wahadhiri wa ngazi mbali mbali kwenye vyuo vikuu wakiwemo maprofessa kwao watu hawa siyo waalimu! Hawajui kwamba mwalimu hata wa chekechea anayo fursa ya kujiendeleza na kupanda ngazi hatua kwa hatua na kuweza kufikia hata ngazi ya uprofesa. Sasa yule ambaye amezembea kujiendeleza na hivyo kubakia kwenye ngazi hiyo ya chini ya ualimu kwa nini wanasiasa na watu wengine wapige kelele namna hiyo?

Cha mhimu ni kuwa fursa yake ya kujiendeleza isifinywe na urasimu wa kipuuzi. Huko nyuma fursa za kujiendeleza kielimu hadi ngazi za juu kabisa (PhD) zilikuwa very open kwa wote. Kulikuwa na maprofessa wengi tu, madaktari bingwa na wanataaluma wengi tu walioanzia ngazi hizi za chini. Manesi wa grade B, rural medical aids, laboratory technicians, clinical officers na wengine waliweza kufikia hata udaktari bingwa. Mafundi mchundo waliweza kufikia kuwa wahandisi n.k. Mimi chuo kikuu nilifundishwa na maprofesa ambao wengi wao walianzia ualimu wa secondary na wengine wa primary kabisa.

Kinachotokea hivi sasa ni kufinya fursa hizi za kujiendeleza. Utakuta mtu ana diploma ya uganga ya ngazi ya NTL6 (ya miaka 3) ambapo hapo awali sifa hiyo ilimruhusu na alishawishiwa kuomba kudahiliwa kwenye shahada ya udaktari akipenda (shahada hii ni ya miaka 5 na si rahisi mtu wa aina hii kushawishika kujiunga nayo). Sasa hivi amewekewa masharti magumu kwamba lazima awe pia na principal passes tatu za A level!!! Hivyo hivyo kwenye taaluma zingine. Unaambiwa ili kujiunga na kozi ya utabibu (CO) mwanafunzi wa form IV anapaswa kuwa pass si chini ya tatu za kiwango si chini ya 'C' kwenye masomo ya PCB (physics, chemistry, biology). Kiwango hichi cha ufauru ni kikubwa na kinamruhusu kujiunga na kidato cha tano kwenye A level moja kwa moja. Atakuwa aidha ni mjinga au ana matatizo mengine kama ataacha kwenda A level na badala yake aende kwenye kozi hiyo ya uganga wa vijijini. Matokeo yake ni kuwa tutaendelea kuwa na uhaba wa waganga kwenye zahanati na vituo vyetu vya afya vijijini. Huo mpango wa zahanati kila kijiji na kituo cha afya kila kata utakuwa ni ndoto kwani utakosa waganga.

Kumalizia mada hii ya waalimu ni kuwa waalimu wako kwenye kila taaluma (every profession). Mwanafunzi akimaliza masomo yake ya sekondari atakutana na waalimu wa fani ya kazi atakayosomea. Kwa mfano kama atasomea sharia atafundishwa na waalimu wa sharia, kama ni udaktari atafundishwa na waalimu wa udaktari. Hivyo kuna waalimu wa uhandisi, uhasibu, mifugo, misitu, utumishi, kilimo, mipango, utawala, usanii, uchumi, maendeleo ya jamii, nyuki, mapori, wanyamapori, ulinzi nk nk. Kwa taaluma yo yote siyo rahisi kukwepa kazi ya uaalimu kwani hiyo itakuwa ndiyo mwisho wa taaluma husika.

Kwa hiyo waalimu wako sehemu nyingi tu lakini hawatambuliwi na hawa wabunge. Masilahi yao hayana wa kuyatetea. Wao mwalimu wanaomjua ni yule wa primary na secondary tu, hawa waalimu wa tertiary na quartery hawawafahamu, sijui ni kwa sababu hawakupitia huko. Mbaya zaidi na wizara ya elimu iko kwenye mkumbo huo huo. Sasa wanafikiria hata kupendekeza kuwa wafaulu wa division I ndiyo wapelekwe kusomea ualimu wa primary na secondary badala ya kusomea ualimu wa tertiary na quartery kama ilivyo sasa!!

Tufanyeje ili kubadili mind set za hawa wanasiasa wetu?
 
Ndiyo maana watu kama Mh Mwakyembe ambaye ni mwalimu wa Tundu Lisu alipokuwa tertiary school, hawataki kujitambulisha wala kutambulishwa kama ni waalimu, na wanafunzi wao kama wakina Lisu wala hawawaheshimu kama wanavyowaheshimu waliokuwa waalimu wao kwenye primary!
 
Back
Top Bottom