Hivi hawa viongozi wa dini uwepo wao kiuongozi Mungu anawatambua?

Euphransia

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
937
778
Wadau,

Nimekuwa nawafuatilia sana viongozi wetu wa dini zote. Nimekuwa nafuatilia uwepo wao katika nafasi zao za uongozi, nimekuwa nafuatilia maisha yao ya kila siku, nimekuwa nafuatilia mahusiano yao na mamlaka nyingine hasa serikali zao Na nimekuwa nataka kujua kuwa Mungu amewatuma wake kuwa viongozi.

Najiuliza iwapo Mungu anatambua vyeo vyao kutokana na baadhi ya matendo Na misimamo yao haiendani na Biblia au Kuruani.Mifano ni mingi ila nitaisema baadhi tu.

Padre au Mchungaji au Shehe kuwa na mahusiano na mke wa mtu
Viongozi wa dini kuziogopa serikali zao kuziambia ukweli pale zinapokosea kama Haki inapoporwa Na serikali viongozi hao wa dini husita kuidai kwa kuiambia Serikali.

Amani inapochechewa vivyo hivyo, viongozi wa nchi wanapoenda kinyume na katiba zao viongozi wa dini husita kukemea, wananchi wanaponyimwa haki na vyombo vya kutoa haki viongozi wa dini wako kimya.Je kama kweli Mungu anatambua uwepo wao kwanini ni waoga?

Au wamejipa uongozi bila kumhusisha Mungu?
 
vipi kuhusu viongozi Kama daudi bashite waliopata division Zero na kufoji vyeti
 
Back
Top Bottom