Hivi hawa TCRA wamefanya tathmini ya kutosha kuhusu uzimaji wa Simu bandia!?

Musoma

Senior Member
Oct 12, 2010
137
221
Kwanza naomba nieleweke kuwa sipingi uzimaji wa simu za bandia unaoelezwa na TCRA ! Mashaka yangu ni umakini wa TCRA na kama wanajua uzito na ukubwa wa jambo wanalolizungumzia! Sijui kama TCRA wameshajiuliza maswali ya msingi kuhusu zoezi hili!

Je TCRA wanajua ni Watanzania wangapi wanatumia simu feki mpaka sasa!? Je TCRA wanajua idadi ya wenye simu feki kwa kila mtandao wa mawasiliano!? Je wamefanya projection ya namna gani mapato ya makampuni ya simu yatashuka wakizima simu feki hizo?! Je wanajua Serikali itapoteza mapato (kodi) kiasi gani kutokana na kuzimwa kwa simu feki hizo!?

Je watu wa TCRA hawawezi kupata "program" ya kisasa inayoweza kuzi-phase out simu feki zote kwa kipindi fulani maalum hata kama wauzaji wataendelea kuziuza kwa wateja!? Ukimsikiliza kwa makini Ndg Mungi ambaye ni msemaji wa TCRA kuhusu kuzima hizi simu huoni mtu mwenye "Business mind"!anachukulia suala la kuzima simu hizi feki kama vile ni kuwakomoa tu wafanyabiashara wa simu pale Kariakoo!

Hazungumzii suala hili kama jambo kubwa lenye "multiply effect" kwa Nchi nzima! Na hili sasa ni tatizo kubwa sana kwa wanaojiita wataalam wa Nchi hii! Sampuli ya wataalam hawa ndo wanamshauri Mhe.Rais na Serikali yake kutafuta Sukari kwenye Magodown ya Wafanyabiasha!

Sasa sijui Sukari hiyo wanayodai imefichwa kwenye magodown ikiisha watamshauri afanye nini tena!
 
Acha wazuie cm fake, makampuni ya cm yakapoyeze asilimia kubwa ya wateja, wapunguze wafanyakazi, watu wakae nyumbani wakisubiri viwanda vianze kazi wakafanye kazi huko, sikuona sababu ya kuzima cm fake bali wangezuia uingizwaji wa cm fake, kwa nini wako busy kuzuia bidhaa za majjumbani haswa vyakula na vipodozi fake kuingizwa nchini na kuviteketeza ila ukaguzi wa cm haufanyiki wakati bidhaa ina ingizwa? Cm fake zinakufa baada ya muda mfupi ni wazi wenye nazo watazitupa baada ya kufa na kutafuta hizo origional wasinge zifungia wangeacha zife zenyewe zipotee nchini, hapa ni muendelezo wa kumuonea mnyonge kwa makosa ya wakubwa.
 
Back
Top Bottom