Yupi awezae kukalia kuti kavu, wakati anajua ataanguka - Maalim Gurumo.
Wamekomaa bungeni wanataka mawaziri na maraisi walioliingizia nchi hasara kwenye madini wakamatwe. Lakini hawamlaani rais Magufuli kwa kutomkamata Lowassa kwenye ishu ya Richmond.
Ina maana hawajui kuwa hakuna mahakama duniani inayoweza kumtia hatiani kiongozi kwa kufanya uzembe. Hata kama unajua kaiba au kachukua ten pasenti bila ya ushahidi hakuna kesi.
Sasa utamkamata mtu umwambie wewe ulikuta nchi inachukua asilimia kumi na tano kwenye madini ukasaini mkataba nchi ipate asilimia zero. Huo si wizi ni uzembe.
Anaweza kujitetea tulikuwa na shida sana ya uchimbaji wa kisasa tukaona tuchukue asilimia 0 madini yachimbwe ili tukusanye kodi. Case closed.
Njia pekee ya kuwaadhibu wanaofanya makosa ya hivi ni kuwafungulia kesi za uhaini. Unamuweka mtu ndani unamuambia hutoki mpaka utuambie ulichukua rushwa kiasi gani, mtandao wako ni upi tunataka mrudishe mali za uma.