Hivi hawa jamaa wanajua kuwa wanakata tawi walilolikalia?

Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
2,000

Yupi awezae kukalia kuti kavu, wakati anajua ataanguka - Maalim Gurumo.

Wamekomaa bungeni wanataka mawaziri na maraisi walioliingizia nchi hasara kwenye madini wakamatwe. Lakini hawamlaani rais Magufuli kwa kutomkamata Lowassa kwenye ishu ya Richmond.

Ina maana hawajui kuwa hakuna mahakama duniani inayoweza kumtia hatiani kiongozi kwa kufanya uzembe. Hata kama unajua kaiba au kachukua ten pasenti bila ya ushahidi hakuna kesi.

Sasa utamkamata mtu umwambie wewe ulikuta nchi inachukua asilimia kumi na tano kwenye madini ukasaini mkataba nchi ipate asilimia zero. Huo si wizi ni uzembe.

Anaweza kujitetea tulikuwa na shida sana ya uchimbaji wa kisasa tukaona tuchukue asilimia 0 madini yachimbwe ili tukusanye kodi. Case closed.

Njia pekee ya kuwaadhibu wanaofanya makosa ya hivi ni kuwafungulia kesi za uhaini. Unamuweka mtu ndani unamuambia hutoki mpaka utuambie ulichukua rushwa kiasi gani, mtandao wako ni upi tunataka mrudishe mali za uma.
 
Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,459

Wewe umekunywa balimi asubuhi hii sio bure
 
Negan The Dead

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
340
1,000
Nikajua umeandika cha maana kumbe pumba tupu.Sijui kwa nini moods wanaruhusu mabandiko ya kibashite bashite.

Kwa akili yako na rais anavyochukia Chadema unadhani Lowassa angehusika kwenye Richmond angemuacha?Kama rais ana uchungu na nchi atuonyeshe vyeti vya Bashite kwanza.Asitudanganye eti Acacia wamekubali kulipa hizo 108trillion!
 
Ngixolele Umoya

Senior Member
Mar 26, 2017
108
250
Post zingine bhana hadi unajiskia aibu kwanini umefungua kuisoma, kama lowassa ni mwizi mbona hayupo serikalini tangu 2008, na hayupo ccm tangu 2015, hana kinga ya kutokushtakiwa, mnasubiri nini kumkamata??? Mkameteni munfunge, wakubwa zako wanajua ndo maana hawamgusi, kila siku kumuobgelea utafkiri yupo serikalini....!!! Lowassa ni raia tu kawaida tu kama wewe, hana kinga ya kushtakiwa, mada za hivi zipeleke tanuru la fikra Facebook, ndo level zake kule
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,786
2,000
Maelezo yote hayo kumbe unamtafuta Lowassa, haya kamkamate umpeleke mahakamani kama una ushahidi maana hata zile ripoti mbili za makinikia hakuna iliyomtaja
 
Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,276
2,000
Wachangiaji wamehamaki kwa uzi mbovu kwa siku ya leo. Wamesahau kuwa wewe una njaa na umetumwa na polex2 kuwachafua kina Lowasa ili ujaze tumbo lako!
Laiti ungelikuwa unajitambua usingeandika ulichokiandika. Kweli ajira hakuna na zilizopo sio hizi za lumumba st!
 
BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,037
2,000
Iko wapi ile picha ya Mkapa akishishika jiwe la kilo 5? Dhahabu tupu!
 
Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
2,000
Mna uelewa mfupi. Hii posti imewabana CCM kuliko wapinzani. Lakini ndio hivyo tena. Nawapongeza walimu wa shule kwa kuwavumilia. Ni kazi ya wito na uvumilivu mkubwa.
 
Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
2,000
Ni hivi wakikamatwa hao jamaa na Lowassa akamatwe. Lakini hata wote wakikamatwa mwisho wa siku hawatakuwa na kesi kwa sababu wizi wa namna hii hauachi kidhibiti nyuma.

Kusaini mikataba mibovu sio wizi. Trump yuko mbioni kuvunja mikataba ya biashara iliyosababisha Marekani iingie hasara kibiashara na mataifa mengine hasa China na Mexico. Mikataba hiyo imesainiwa na marais kina Obama na Clinton.

Lakini tunajua kuwa hawa jamaa zetu wamechukua kitu kidogo (kikubwa in this case) kwa hiyo kesi ya wizi hatutawapata. Wapewe kesi ya uhujumu wa uchumi ambayo haihitaji ushahidi. Ni kubinywa korodani tu mpaka useme kila kitu na urudishe mali za uma.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634

..kwani nani amewazuia CCM kuwakamata Lowassa na Sumaye?

..serikali dola mahakama zote ni za CCM, sasa nini kimewapa kigugumizi cha kuwaburuza Sumaye na Lowassa mahakamani?
 
Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
2,000
Bado huelewi wizi wa hivi hauna ushahidi wa kusimama mahakamani. Hizi ni kesi za kuwekwa ndani tu kama za ugaidi mpaka mtuhumiwa aseme ukweli.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom