Hivi hata bustani zimetushinda?

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,345
Reaction score
15,852
Taarifa ya BBC pia imeeleza kama nilivyoweka link hapo.

Ni ukweli usiopingika huwezi kuifananisha Dar na miji mingine mikubwa ya East Africa kama Nairobi kwa mpangilio wake hasa kwenye bustani za wazi watu kupumzika katikati ya jiji. Hii inaifanya Dar ionekane kama kichochoro ikizidiwa hata na Tanga, Arusha na hata Sumbawanga (bustani ya mandela).

Cha ajabu kampeni za ajabuajabu tu ndio utaziskia mara tezi dume mara ushoga mara makahaba. Yaani kampeni zote zinalenga kwa vitu visivyo na tija utasema viongozi wetu hawafikirii au hawajawahi kutembea nje ya mipaka yetu.

Kuna haja sasa kufanya kitu kwenye hili maana hata bustani zilizopo zilishatelekezwa na hazitumiki kwa makusudi hayo.

Kwa washauri wa yule jamaa mzee wa kampeni wampe na hii kama kweli anataka kuacha legacy hapa mujini.

Kwa nini watanzania hawapendelei kukaa katika bustani za wazi?
 
Maeneo ya wazi yalikuwepo baadaye yalibadilishwa matumizi
 
Dar ipo overrated sana. Ukienda tuu hapo Nairobi utaelewa.
 
Ile bustani iliyopo pale posta ya zamani " Aisee watu wananyonyana sana ndimi usiku ''' ukikaa peke yako pale lazima ujihisi upweke

nikirejea kwenye mada " mkuu usemacho ni kweli kabisa bustani nyingi mnoo zilizopo awali kwa sasa zimeshakufa mfano hai upo pale magomeni " "... palikuwa na bustani nzuri sana miaka ya nyuma watu walikuwa wanapumzika pale " kabla ya kuvamiwa na wahuni waliokuwa wanashinda pale na kuipoteza mvuto wake " na mpaka mamlaka husika hivi sasa wameamua kuiua kabisa " na hivyo sasa haipo tena kama ilivyokuwa awali
 
Dar ipo overrated sana. Ukienda tuu hapo Nairobi utaelewa.
Dar siasa za kiboya zimetamalaki...na ujingaujinga mwingi. Angalau mwendokasi inatupa heshima kuwa ni kitu cha tofauti ambacho wanaweza kuja kushangaa
 
Na ndio kuna mkuu wa mkoa mchapakaz....uuuuwiii
 
Na ndio kuna mkuu wa mkoa mchapakaz....uuuuwiii
zamani ilikuwa garden poa kabisa waliwekwa mpaka walinzi wakulinda mazingira ilikuwa ikifika usiku haupaswi kupita lile eneo "... na ukikutwa na mpenzi wako kwenye vile viunga vya bustani mida mibovu basi unatozwa faini
 
Wameamua kujenga ofisi kabisa! Magomeni kulikuwa na garden zenye mabembea na vivutio vingine vya watoto zaidi ya tano sasa hivi zote zimegeuka gereji bubu.
 
Ilikuwa na geti kuingilia na kutokea.
 
Wameamua kujenga ofisi kabisa! Magomeni kulikuwa na garden zenye mabembea na vivutio vingine vya watoto zaidi ya tano sasa hivi zote zimegeuka gereji bubu.
Aisee inasikitisha sana,mi nilidhani maeneo ndio hayakutengwa kumbe yapo wakayatelekeza!
 
Aisee inasikitisha sana,mi nilidhani maeneo ndio hayakutengwa kumbe yapo wakayatelekeza!
Yapo kinondoni,ilala,temeke. Watu hawajali, hawana akili ya kuwaonesha kuwa hivyo vitu ni muhimu ndio maana maeneo kama hayo wanajenga magorofa.
 
Wameamua kujenga ofisi kabisa! Magomeni kulikuwa na garden zenye mabembea na vivutio vingine vya watoto zaidi ya tano sasa hivi zote zimegeuka gereji bubu.
Aisee ..
 
Sehem gani magomen mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…