Hivi furaha ya Fid Q ni kutuacha njia panda?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF na wadau wa Hip Hop na muziki kwa ujumla.

Fid Q.jpg


Ni muda sasa nimekuwa mfuatiliaji wa muziki wa kizazi kipya hususani mwahip hop Fareed Kubanda. Jamaa ni mwanafasihi aliyetukuka hapa nchini kwetu, kila akitoa wimbo lazima kuna mistari inakuwa mitihani kwa wasikilizaji kuelewa alimaanisha nini na pia uandishi wake ni kivutio kwa wadau wanaopenda kufikirisha bongo zao.

Nimeona ni vema nikaweka baadhi ya mistari konde (Punch Line) ya Fid Q ili tuijadili kwa pamoja yawezekana kuna wengine wakapata uelewa na pia wadau mnaweza kutiririsha mistari mingine ya huyu mwamba ikiwezekana na namna mnavyoielewa.

1- Wimbo: SIRI YA MCHEZO.

Hii ni baadhi ya mstari katika wimbo huu ambayo huwatatiza wadau mbali mbali:

“Pole MAPROSOO uhujumu uchumi umefanya umetubu,
WAZEE ni wahuni hadi soo way back before SUGU,
Taifa la kondoo, huendeshwa na serikali ya Dubu,
na MBWA MWITU wenye siri, li bepari umuabudu,
Kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu,
huo ni utumwa pia,
Unafanya vijana wanaumia,
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia,”

2- Wimbo: Ielewe Mitaa.

Pia huu wimbo unamistari mingi amabayo imefichwa sana kwa upande wa maana nitaweka michache:

“Naeza lala na bundi na ukaamka mwenye bahati
usilale fofofo, ruzuku itakwisha,
utatembea hovyo ka kuku aliyekatwa kichwa,
maisha yako fast na yana speed ya light,
unaeza freeze kama ice ndani ya fridge ice,
ukienda mbio, na muda mtapishana,
mafanikio, huja kwa kupenda ninachokifanya,”

“Niletee mabumunda, mjeshi nikiwa vitani,
nikikuta mnaabudu punda, nitawapelekea majani,
wangapi huji'stress, hujitia mapozi na hawajielewi,
msiache nutcase, inaeza ka divorce ya hail mary,
funny huh?, sijui serious yuko wapi,
i make cred gos in the front row forward left,”

“Badili mwendo mkwepe skendo, mwache aende zake,
au muonyeshe upendo, tembo hachoshwi na pembe zake,”

3- Wimbo: I am a professional.

Pia humu kuna mistari kibao ya kuvutia na huwaacha watu njia panda pia:

“siniite brief kama nike just do it, just do it,
sikupaki matope kwenye hii dunia ya nguruwe,
wala si stop nikiona red, natafuta daily bread,
sasa im fully paid cause, I am a professional,
mi ni zaidi ya bling bling magari pesa,
kile ambacho hakiuzwi kwa bei ya chini and, I am a professional,”

4-Kuna wimbo ulitengenezwa na wasanii kadhaa ulikuwa kama Cypher ya Fiesta Fid Q alipata kuflow mistari ifuatayo:

“Usijiulize mimi ni yupi mimi ni nux zaid ya shaka,
Ninabonge la mkuki ndani ya chupi hii ni boxer,
Maisha ni menu na muhudumu ni muda,
Fasta unganisha order zenu kisha hukumu itakuja,
Me ni mbishi zaidi ya nyota uzionazo mchana wajua kali,
Siishi kwa kukopa naogopa lofa utanitosa mbali,
Utanidondosha ngosha itakuwa hatari..”

Hiyo ni baadhi wadau mnaweza kuongeza, mingine na sio tu mistari migumu kueleweka bali hata ile inayofurahisha na kuelimisha.
 
Jamaa ana punchlines ambazo unaweza kuisikiliza ngoma yake muda mrefu sana ndo uje kuelewq anachomaanisha
 
1. Home nina Stock ya mistari kama mji mkuu wa Sweden
( mji mkuu wa sweden unaitwa Stokholm ila unatamkika stockhome)
 
2. Je mnatamani nishuke chini kama mademu wa marubani
3. wanataka ni Rap tu kama Moi
( rais wa awamu ya pili Kenya anaitwa Arap Moi)
3. Nimeamua kuwa vegeterian sijui lolote kuhusu beef
 
2. Je mnatamani nishuke chini kama mademu wa marubani
3. wanataka ni Rap tu kama Moi
( rais wa awamu ya pili Kenya anaitwa Arap Moi)
3. Nimeamua kuwa vegetarian sijui lolote kuhusu beef
Yah ukiwa vegetarian ni kama Rastafarian so huli nyama ila jamaa alikuwa na maana mbili hapo
 
Naona vitu vigumu ila sijajua maana yake ....isije ikawa lengo ni kuweka maneno pasipo maana
 
ni mzuri tu wa vina lakini kwenye beats anachemka vibaya
mwanzo na mwisho nilimuelewaga kwenye fid q.com na propaganda
 
Fid ni jeshi la mtu mmoja, na sikopeshi kwa nguvu ya hoja
Niko mbio zaidi ya less, na ujio siyo wa verse moja.
 
Wimbo wa kwanza kumtambulisha FID Q ni ule wa - Huyu na yule, huyu faida yule bure!

Kuna mistari kama

- Huyu madem yule sabuni
- Yule ni mtu wa kugeza yule anabundi
- Huyu kazi anaililia yule ameichoka
 
Wangapi huji-stress kujitia mapozi na hawajielewi/ In such a nut case, naeza nikawa DIVORCED and REMARRIED/ Funny huh? Sijui serious yupo wapi/
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom