Hivi Dr Ulimboka amenywea au amelishwa kitu au kaishia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Dr Ulimboka amenywea au amelishwa kitu au kaishia wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Father of All, Oct 6, 2012.

 1. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nikikumbua JF ilivyompigia debe na kumuunga mkono Dr Ulimboka baada ya kufanyiwa kitu mbaya na serikali, najisikia vibaya kuona alivyotoweka. Je kunani au amelishwa kitu, kugwaya, au kaishia wapi jamaa huyu? Maana sisikii mgomo wa madaktari tena ukiachia mbali wenzao waliomo kwenye mazoezi kuwasaliti na kuramba masaburi Kikwete. What's up?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  ....Siri ya mtungi aijuaye ni kata...Kimya kingi...Kwa jinsi siku zinavyozid kuyoyoma sijui kama tutamsikia Dr Ulimboka akisema chochote kuhusu yale yaliyomsibu katika lile pori la mauaji kwa jina maarufu la mabwepande.
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu umesahau dr mwakyembe nae ametoka huko huko alikotoka dr ulimboka? Baada ya dr mwakyembe kupewa uwaziri kilichofuata ni kusema watu wasifuatilie afya yake nafikiri na dr ulimboka ni hivyo hivyo hawa jamaa hawana mapenzi na hii nchi Wana njaa tuu
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,799
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Mimi nahisi vitu vitatu

  1.Ametishwa sana akatishika

  2.Amepewa pesa nyingi sana ili asiiache serikali uchi

  3. Tukio la kutekwa kwake na kuteswa halina uhusiano na mgomo, labda ilikuwa analipiziwa kisasi kwa kutembea na mke wa mtu, au kudhulumu!!
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Mhhhh! Hayo mawili ya kwanza yana uzito zaidi kuliko hilo la tatu hasa ukitilia maanani maelezo ya Dr aliyoyatoa wakati yuko mahututi yaliyotutaarifu kwamba aliyehusika kumteka ni mtu ambaye anamfahamu na aliwahi kumuona Ikulu katika mgomo wa kwanza kama sikosei ulikuwa kati ya December 2011 na January 2012.

  Halafu ukiunganisha na ile artile iliyoandikwa na Mwanahalisi na kusababisha gazeti lile kufungiwa kuhusu mchoro mzima wa kutekwa kwa Dr basi hayo mawili ya kwanza ndiyo yanazidi kuwa na uzito zaidi.
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Wonders shall never cease. Na amejikalia mbali na media kabisa. Ila angejitokeza kuna maswali ambayo.angeshindwa kuyajibu. Muache tu apotelee. Wenzao wakenya wamegoma kiutu uzima na madai yao kutekelezwa. Ubinafsi ndio uliotufikisha hapa tulipo to start with.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  .. Best serikali yao inawajali ndio maana ikaona umuhimu wa kuyatekeleza madai ya o na yale ya walimu mara moja bila kusuasua...sie kwetu serikali ikaja na ngojera zake, "Serikali haina uwezo" na kuanza kutumia vitisho vya kuwafukuza kazi madaktari na walimu, lakini cha kustaajabisha Serikali hii isiyo na uwezo iliweza kupata uwezo wa kuongeza mishahara na marupurupu ya Wabunge kwa kiwango cha hali ya juu!!!

  Wenzetu miaka michache iliyopita Waziri Mkuu wao Raila Odinga alipasuliwa kichwa na madaktari wazalendo kwa kuwa viongozi wao wanaamini wana vifaa vya kileo na madaktari mabingwa, kamwe huwezi kusikia Pinda/Kikwete akubali kupasuliwa kichwa nchini lazima wataenda majuu maana wanajua sera za magamba zimefanya hospitali zetu ziwe hoi bin taabani zikiendelea kusuasua na vifaa vya mwaka 47!!! Waache Wakenya wawe juu.


   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Best, hata wao mwanzoni walisumbuana na waalimu sana. Lakini kila ofa waliyotoa waalimu waligoma hadi ilipofika 300% waliyoinuia. Madaktari serikali yao haikuwaacha kwa kitambo coz walijua madhara yake. Hawa wa kwetu ni kuwa divided then ruled. Uli na kudhalilishwa kote lakini amerudi amenyamaza. Which now is the trend ya migomo. Hata SA nao wakikomaa kugoma ni hadi kieleweke. Unajua naamini watu wanakutreat the way unawaruhusu kukutreat.
   
 9. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  kuwa mbali na media? Mie naamini tu kuwa hili nalo litapita kama yalivyopita mengine mengi kabla na baada ya uhuru. Watanzania tumekuwa kama watu ndani ya club ya disco,ambapo dj huwatesa wachezaji kupitia udhaifu wao ni dj tu ndie huwa mtu wa kwanza kugundua kuwa sasa wachezaji wamechoka,pamoja na kuchoka dj huwawekea cd/tape ingine kali zaidi,hapo hapo watu huanza tena kucheza wakiwa wamesahau uchovu wote uliopita,
   
 10. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  1) Ngoja upepo upite, jamaa anapelekwa nje kufanya MPH everythings is pay off by TISS. (speculation)
  2) JK amempromise Ubalozi au Cheo ndani ya serikali baada ya Afya yake kutengemaa. (speculation)
  3) Kesi ya Kova's movie ipo mahakamani, kafungwa mdomo kujadili jambo lililo mahakamani (Intellectual guess)
  4) Baba na family yake wamemtisha baada ya kutishiwa usalama wao na TISS, Its not worth (guess)
  5) Dr. Ulimboka katishiwa usalama wake au kufunguliwa kesi hivyo kaufyata (guess)
   
 11. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kuna mtu alileta uzi hapa kwamba watanzania ni wanafiki. Unataka Ulimboka aseme lipi jipya wakati alishasema kila kitu, tena akiwa katika maumivu makali? Mwanahalisi ilipoleta data za uchunguzi kwa kuanzia pale Ulimboka alipoishia na kisha kufungiwa ati kwa uchochezi, wewe umefanya nini? Sasa unataka Ulimboka afunguke zaidi ili uchukue hatua gani? Ninyi ndio wanafiki wakubwa.
   
 12. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  ozzie we kweli nyani. unafiki unaujua au unachachawa. si ajabu we ni mmojawapo waliomtesa Ulimboka. Kwa vile nawe ni mtanzania basi mnafiki. shame on you sob and bugger.
   
 13. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mimi sijui ila naamini Dr. Ulimboka will die silently before coming election. Wabaya wake hawawezia amini kuwa one day hat
   
 14. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,681
  Likes Received: 870
  Trophy Points: 280
  Mwacheni apumzike jamani, mwajua kung'olewa kucha na meno bila ganzi nyie??!!
   
 15. Bosco Ntaganda

  Bosco Ntaganda JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 551
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mwacheni apumzike jamani, amenusurika kifo
   
 16. U

  Uriria JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 744
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 45
  Kushney
   
 17. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Na kuminywa korodani!
   
 18. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  Nia thabiti isiyo na mawaa, msimamo usiotetereka, ni moja ya nguzo muhimu pindi kundi moja linapotangaza mgogoro au mgomo dhidi ya serikali.
  Ni wazi kabisa kuwa madai ya madaktari katika mgomo wao yalikuwa ya msingi na vipo vipengele vya madai hayo vilivyokuwa na manufaa kwa umma wa watanzania, maadaktari wenyewe na hata serikali.
  Kitendo cha madaktari kugoma kilipingwa vikali sana na serikali ikisaidiwa na kundi chache la madaktari hao hao pamoja na watanzania.
  Kila kundi lilikua na sababu zake ambazo kwao walizona zina msingi.
  Binafsi naamini wananchi na madaktari wachache walikuwa kinyume na maadhimio ya mgomo walitawaliwa na WOGA na HOFU ikichagizwa na sintofahamu ya itakuwaje. Nadiriki kusema kundi hili la watu ndio sehemu kubwa ya Watanzania ambao UOGA huwatawala hata wanapopewa fursa ya kuchagua mgombea mwenye maslahi mema kwa Taifa hili, hakuna mwenye moyo wa kuthubutu.
  Kwa upandr wa serikali sote tunajua historia ya migomo na hatma zake. Mara zote huwa nahisi, labda Serikali ya Tanzania itakua sikivu pindi Wahisani wakigoma kuisaidia kifedha au Waumini wa dini wakigoma kushinikiza jambo fulani.
  Kwa kutambua hayo, msitegemee hata siku moja watu kama kina Dk. Ulimboka, Dk. Mwakyembe au hata Prof. Mwandosya kubainisha yale yaliyowasibu hata kama watakuwa wanayo haki hiyo kimsingi. Kama mlishindwa kuwaunga mkono katika ile nia njema walioianzisha, mtawezaje kuwaunga mkono kwa taarifa tu watakazotoa? Wahenga husema matendo huongea zaidi ya maneno, lakini kwa Watanzania maneno ni muhimu kuliko matendo, wanajua kabisa mtu kuna hatari kubwa inayomkabili yule anayeshiriki kutenda kuliko yule atayesikia sababu za Dk. Ulimboka na kuzifanya stori za siku kijiweni.

  Dk. Ulimboka, ni vyema akaachwa aamue mwenyewe na asilaumiwe kwa lolote atakaloamua, wacha sisi Watanzania wanafki tuendelee kuonja tabu na shida za sekta ya afya maana ipo siku zitaisha bila kupigiwa kelele.
   
 19. c

  chama JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Precise pangolin;
  Ulimboka ana familia inamtegemea; wewe hutaki kuwa shujaa?

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 20. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,315
  Trophy Points: 280
  Watanzania tunataka mno kuchulia kila kitu kama sinema... tukae tunapiga soga huku tukiangalia wenzetu wanavyotenda. Matatizo yaliyompata Dr Ulimboka ingekuwa nchi nyingine serikali ''ingeanguka''. Hii ni kwa sababu uma wote ungeungana bila kujali dini, rangi, kabila, siasa wala aina ya kazi na kulaani vikali (kwa matendo) tukio la kihuni na kipumbavu kama lile. Kungekuwa na maandamano mpaka rais angeiona ikulu ya moto. Lakini wapi.. angalia tumekaa kwenye keyboard zetu tukijifanya eti tulimuunga mkono kwa kumpigia debe na bado tuna hamu ya kuona sinema ikiendelea.... Huu ndio unaitwa unyumbu wa nyumbu wa Manyara national park. Jana alikuwa Ulimboka, leo alikuwa Mwangosi je kesho atakuwa nani? Hatujui.. lakini bado tunaendelea kufurahia maisha.
   
Loading...