King Shebby
Member
- Apr 21, 2016
- 12
- 3
....Natumai kuna wadau mbalimbali mlishiriki usaili wa mchujo wa nafasi mbalimbali zilizotolewa na DART pale DUCE jumamosi ya tarehe 21.05.2016.
Hoja yangu hapa ni mbili hivi;-
1. Kutudanganya kuwa majina ya watakao faulu usaili ule yangebandikwa pale DUCE, kuwekwa kwenye website yao na pia kutumiwa ujumbe mfupi (SMS) kwenye namba ambazo kila msailiwa ataaandika kwenye zile register zao. (Kesho yake tayri wangekuwa wametoa majina yaani - Jumapili jioni tarehe 22.05.16
Lakini hadi leo hii sijapata taarifa kutoka kwenye tovuti yao kuhusu watu walifanikiwa kuitwa hatua inayofuata ya usaili wa mahojiano c kkwenye simu au tovuti (sijajua DUCE ka wamebandika majina kule).
Kwa mwendo huu ni bora ingewekwa wazi tuu kuwa walikuwa na majina ya watu mifukoni na wengine waliitwa kukamilisha ratiba tuuu, na usaili wa namna hiii unawapotezea watu muda wa kufanya shughuli zao za msingi huku mkijua kuna watu wameandaliwa kupewa hizo nafasi.
2. Kwa nini mtu atoe taarifa ambazo hazitekelezeki??
Kuwaambia watu kuwa kesho mnatoa majina kwenye tovuti yenu, mtabandika kwenye mbao za matangazo DUCE au kuwatumia ujumbe mfupi kwenye simu harafu mwisho wa siku hakuna utekelezaji ni Uongo na kuwakosea heshima Wahusika.
Mamlaka zenye nguvu juu ya hawa watu wachukue hatua ili waache mtindo wa kufanya vitu kwa mazoea kama ilivyo zoeleka.
Kasoro zilizojitokeza siku yenyewe ya usaili:-
1. Majina ya watu kutoka kwenye gazeti lakini kutokuwepo kwenye orodha yao
Hii ni aibu ya mwaka kwa kumuita mtu wewe mwenyewe lakini anakuta hakuna jina lake siku ya usaili
2. Kuandika majina yetu halisi kwenye karatasi za majibu
katika hali ya kushangaza na kustajaabisha ni pale wasailiwa walipo ambiwa watumie majina yao halisi kwenye karatasi za kujibu maswali husika.
Hapa ni rahisi sana kupanga matokeo ya wasailiwa na kupeana nafasi kwa kujuana, kwa nini wasitumie mfumo kama wa Utumishi walau unapunguza hofu ya kupeana fursa kwa kujuana ( Japo sio lazima kusema hakuna kujuana utumishi). Lakini kidogo inapunguza makali
3. Kukosea Jinsia za wasailiwa
Hiki ni kituko kingine unakuta msailiwa ni Mwanaume lakini amewekewa "F" ina maana hata CV za watu walikuwa hawazisomi kwa ufasaha??
USHAURI!!!
Kwa siku za usoni tunaomba muwaachie UTUMISHI wafanye kazi yao tuuu wao watawapatia idadi ya watu mnaowataka. Lakini kulazimisha vitu ambavyo hamna uzoefu navyo ni tatizo na kikwazo. Hapo nimeweka kasoro muhimu tuuu lakini kulikuwa na kasoro zaidi ya hizo.