Hivi Dar ya 2017 inatofautianaje na ya 2015?

Hivi Dar ya 2017 inatofautianaje na ya 2015?

Zero Hours

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
12,942
Reaction score
18,692
Wakuu naomba msaada hapa,

Nashindwa kupata jibu kuwa inakuwaje mkuu wa mkoa wa Dar awe mfano kwa wakuu wa mikoa wote. Naomba tuangalie vitu ambavyo vipo vinaonekana Dar ya leo na tulinganishe ile ya 2015?

Kama ni ile vita vya wauzaji wa sukari je sukari ilishuka kufika bei elekezi? Kama ni vita ya madawa ya kulevya, je ni kweli haya madawa yameisha. Mbona biashara inaendelea tu as usual?

Kama ni vita ya watu kunywa pombe muda wa kazi, je wameacha? Je ile vita ya watu kulala gest muda wa kazi nayo imeisha? Kama ni kupanda miti, iyo miti iliyopandwa ipo wapi hivi sasa?

Kama ni usafi mbona jiji bado chafu tu?
 
Dar ya sasa ina miti barabara ya morocco mwenge ambayo itang'olewa muda sio mrefu kupisha upanuzi wa barabara.
 
Dar ya 2015 ilikuwa na hsc - Home Shopping Centre - Dar ya 2017 haina kitu kama hicho.
 
Dar ya leo vyuma vimekaza sana na grisi hakuna, nyumba nyingi sana zimevunjwa morogoro road
 
Dar ya leo 2017 kuna Wafanyakazi waoga na wasiojiamini zaidi katika ofisi za serikali, kuliko ilivyokuwa 2015. Mifano nenda Bandarini, Airport, Hospital, hata katika ofisi za Halmashauri. Wakimuona mtu wasiyemjua wanaogopa !!!
 
Back
Top Bottom