TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Habari za muda huu wanajamvi? Mie kama kawaida leo najisogeza uwanjani na hivi vipindi na matangazo ya luninga zetu ambayo kwa nyanja moja au nyingine yanatuharibia watoto wetu.
Mwanzo nilipolisikia hili tangazo nilidhani masikio yangu mabovu kwamba nimesikia vibaya ikanibidi nilivutie ukasi na kulitega mpaka nikalisikia tena. Kwa ufupi lina maneno ya kihuni na matusi juu, simainishi ile kauli ya kisoka ya "kampa kampa tena" la hasha bali ukilisikiliza vizuri kuna mahali wanasema nasikia utamu kisha.......(tusi) kama hamuamini livizieni hilo tangazo mlisikilize kwa makini mtasikia tusi la waziwazi bila chenga?! Napata maswali lukuki kichwani kwa hiki chombo cha habari.
1) Wanaandaa kizazi cha namna gani kama mambo hayafichiki siku hizi?!
2) TCRA kazi yao husika ni ipi hapa Tanzania iwapo mambo kama hata yanatokea?!
3) Mkurugenzi wa vipindi, Meneja masoko na mhariri walikuwa wapi kuruhusu tangazo hili likaenda hewani?!
4) Ni mahaba ya soka yamewazidi mpaka wamekuwa wahuni au imetokea bahati mbaya? Iwapo ni bahati mbaya kwanini wasiliondoe haraka?!
Dunia imeharibika kwa kweli, nimekaa zangu sebuleni na mke wangu na binti yangu mdogo Mwanzo sikuona tatizo ila nilishangaa mke wangu akibadili Channel haraka kisha akapiga kimya nilivyododosa akaniambia ila nikalitafuta na kuangalia ndipo nikajua masikio yangu mabovu ila mara ya tatu nikajiridhisha ni kweli.
Hivi watanzania tunaelekea wapi na mambo haya, utandawazi unatuharibu kiasi hiki?!
Pasi Shaka TCRA watafanyia kazi au Chanel husika kusitisha kurusha hilo tangazo.
Na Chanel zingine rekebisheni matangazo na namna ya utangazaji kwani mnatuharibia watoto na vijana wetu mitaani huku.
Asanteni na ninawasilisha