Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
CCM tuna mambo mengi ya kuwaambia wananchi. Si kuwaambia tu bali wanaona kwa macho yao. Hakuna blaa blaa bali bampa to bampa.
1. Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka umeanza kazi na wana Darisalama wananufaika. Huo ni mtaji wetu
2. Shirika la Ndege ATCL limeanza kusimama kwa miguu yake na limeweza kutengeneza faida ya bilioni 7
3. Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa hadi 2020 ujenzi utakuwa umekamilika hadi Morogoro. Na kabla ya kuanza kampeni, treni zitakuwa zimeanza ambapo umbali wa Dar Morogoro ni saa 1:30
4. Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Tanga utakuwa umekamilika. Tanzania tutakuwa Exporter wa mafuta kwenda nchi jirani.
5. Usambazaji wa umeme vijijini unapamba kasi kwa sasa. Hadi 2020, Asilimia kubwa ya vijiji vyetu vitakuwa na umeme wa uhakika na wa bai nafuu
6. Mradi wa kusambaza maji vijijini unaendelea kwa kasi. Hali hii imepunguza magonjwa ya kuambukiza kama kipindipindu. Kwa utawala wa Magufuli, Kipindupindu hakikubaliki
7. Milioni 50 kwa kila kijiji si ndoto tena. Mchakato wa kugawa fedha hizo unaendelea. Na wananchi wanaendelea kuhamasishwa kujiunga kwenye vikundi.
8. Hadi 2020, mikoa yote Tanzania itakuwa imeunganishwa kwa barabara za lami.
9. Hadi 2020, wananchi wengi watakuwa wameajiriwa kwenye sekta ya viwanda iliyoanza kupaa kwa kasi
10. Ifikapo 2020, ubabe wa Rais Magufuli utakuwa umezika kabisa tatizo la ufisadi, uzembe na uhujumu uchumi nchini.
11. Mwaka 2020 tutashuhudia Tanzania ikiongoza nchi zote za Afrika Mashariki katika kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
12. Uchaguzi Mkuu wa 2020 utafanyika kipindi ambacho Sekta ya Afrika itakuwa imeimarika na vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 5 vitakuwa vimepungua.
13. Hadi 2020, mazao ya biashara ya pamba, korosho, ufita, tumbaku, kahawa na alizeti yatakuwa na thamani kubwa kutokana na ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao hayo kujengwa kwa wingi hapa nchini.
Kwa kweli mambo ni mengi sana na nikiamua kuyaorodhesha yote, nitatumia zaidi ya siku mbili kuyamaliza.
Sasa tuje upande wa pili wa shilingi, vyama vya upinzani. Kick zao zote wanazotumia kuishambulia Serikali ni za msimu. Ni kama nyanya vile ambayo huwezi kuiweka ghalani.
1. Ile kick ya UKUTA imeishia wapi?
2. Kick ya Bunge Live imeota mbawa na sasa hakuna anayeiongelea tena. Watanzania wameanza kuuona ukweli.
3. Vipi kuhusu bei ya sukari? Hoja hiyo bado ina value kwa wapinzani? Nani anaiongelea?
4. Mapambano dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda yamenaki kwa Mange Kimambi tu.
5. Hivi wapinzani mnaungwa mkono na wananchi juu ya hoja yenu kuwa Rais Magufuli ni Dikteta uchwara?
Aiseeeee! Nawahurumia sana machadema. Nina hakika mzee wao Lowasa ambaye ndiye mgombea Urais wao 2020 si tu atashindwa kuongea bali atashindwa hata kuruka na chopa.
Lazima tuheshimiane.