Hivi CHADEMA inastahili kuwa chama cha kidemokrasia?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
16,003
Amani iwe kwenu!

Katika pita pita yangu maktaba ya mambo ya utawala wa kisiasa "political governance"..huki nikifuatilia siasa za CHADEMA hii "mpya" chini ya yaliyokuwa magamba.Nimegundua ya kuwa kuna misingi ya kidemokrasia imekiukwa,ningependa tupatiane majibu ili tujisahihishe;

1.Je kipengele kinachozuia mwanachama kudai haki mahakamani pale anapohisi kuonewa kinaendana na misingi ya demokrasia?

2.Je uchaguzi wa kunyoosha vidole huku mwenyekiti Mbowe akitamba "nataka nione asiyenyoosha,ni mchawi!"..hii ilitokea siku ya kumuidhinisha Lowassa na Mashinji...je ni kweli hawa watu walipata asilimia 100 ya kura?

3.Tumeshuhudia Lowassa akijinadi kuwa ndiye mgombea wa CHADEMA 2020.Je hili limepata baraka ya vikao?..je katiba imempa ugombea wa kudumu?...Mbowe mbona unanyamaza,unamwogopa?...BAVICHA kazi yao nini katika kulinda chama?..je hili suala kwa muktadha wa demokrasia limekaaje?

4.Tukio lilifanywa kwa wagombea wa ubunge na udiwani chadema,Monduli..wote waliondolewa na kuwekwa vibaraka wa Lowassa....ninaweza nikasema Baraza la madiwani Monduli hawaamini katika CHADEMA bali Lowassa;Je hii kidemokrasia imekaaje?(maeneo mengi pia ilitokea)

5.Je hili jambo la kutopendekeza wenyeviti Laac,Pac...kwa sababu kuwa hawawezi,vilaza,limekaaje kidemokrasia?

6.Je kwa matukio hayo hapo juu, CHADEMA imegeuka kuwa chakima? (chakima:chama cha kiimla na malalamiko)

Nawakaribisha kujadili hoja hizo chache ili tufikie muafaka kuboresha vyama vyetu.

Tujikite kwenye mada na sio kelele.
 
Swali lingine je Mbowe ni kiongozi wa upinzani bungeni? Alichaguiwa lini na uchasguzi ulikuwa na wagombea wangapi na akina nmani? Je ulionyeshwa kwenye TV live? Na je taarifa zake zilisambazwa vyombo vya habari?

Kama haujafanyika Mbowe anajiitaje kiongozi wa upinzani bungeni?
 
Ongezea na Mwenyekiti wa CCM kupatikana hata kabla ya Juni. Hakuna uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM na wala hakuna mwanachama anayeruhusiwa kugombea. Demokrasia iko wapi?

Mzee Tupatupa

Anzisha thread yako ya hili hapa mleta maada kaleta INAYOHUSU CHADEMA.
 
Swali lingine je Mbowe ni kiongozi wa upinzani bungeni? Alichaguiwa lini na uchasguzi ulikuwa na wagombea wangapi na akina nmani? Je ulionyeshwa kwenye TV live? Na je taarifa zake zilisambazwa vyombo vya habari?

Kama haujafanyika Mbowe anajiitaje kiongozi wa upinzani bungeni?
Ni swali muhimu sana!
 
Kwa swali lako mheshimiwa hiki chama hakipaswi hata kuwa chama cha siasa, kwa kweli mheshimiwa kilipaswa kiwe Bank au SACOSS ili watu wakope na kurejesha marejesho.

Ngoja tusubiri.
 
Mimi nilikusa die hard wa chadema kipindi wako vizuri, lakini kimsingi kwa sasa chadema imepoteza dira, ukibadilishia gia angani ni dalili ya kukosa dira ya unapoelekea
Lazima tuulize maswali ili tujisahihishe.
 
Yote uliyozungumza hayana ukweli ndani yake na umeyazungumza kutokana na chuki uliyonayo ndani juu ya CHADEMA.....najiuliza tuu zanzibar, bunge kutokurushwa!!! Naona unauliza misingi ya demokrasia wakati hata watawala ndo wakiukaji wakubwa wa misingi!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yote uliyozungumza hayana ukweli ndani yake na umeyazungumza kutokana na chuki uliyonayo ndani juu ya chadema.....najiuliza tuu zanzibar, bunge kutokurushwa!!! Naona unauliza misingi ya demokrasia wakati hata watawala ndo wakiukaji wakubwa wa misingi!!
Mantiki ya maswali ni kulinda CHADEMA isiwe kama watawala,usikasirike mdogo wangu.Jikite kwenye mada.
 
Tukiangalia namna ya maswali ulivyoyajenga basi unaweza kugundua kitu....

Mbowe anajaribu kufuata maneno ya Gaddaf aliyoyazungumza akiwa Rwanda

Democracy is luxury life
 
Amani iwe kwenu!

Katika pita pita yangu maktaba ya mambo ya utawala wa kisiasa "political governance"..huki nikifuatilia siasa za CHADEMA hii "mpya" chini ya yaliyokuwa magamba.Nimegundua ya kuwa kuna misingi ya kidemokrasia imekiukwa,ningependa tupatiane majibu ili tujisahihishe;

1.Je kipengele kinachozuia mwanachama kudai haki mahakamani pale anapohisi kuonewa kinaendana na misingi ya demokrasia?

2.Je uchaguzi wa kunyoosha vidole huku mwenyekiti Mbowe akitamba "nataka nione asiyenyoosha,ni mchawi!"..hii ilitokea siku ya kumuidhinisha Lowassa na Mashinji...je ni kweli hawa watu walipata asilimia 100 ya kura?

3.Tumeshuhudia Lowassa akijinadi kuwa ndiye mgombea wa CHADEMA 2020.Je hili limepata baraka ya vikao?..je katiba imempa ugombea wa kudumu?...Mbowe mbona unanyamaza,unamwogopa?...BAVICHA kazi yao nini katika kulinda chama?..je hili suala kwa muktadha wa demokrasia limekaaje?

4.Tukio lilifanywa kwa wagombea wa ubunge na udiwani chadema,Monduli..wote waliondolewa na kuwekwa vibaraka wa Lowassa....ninaweza nikasema Baraza la madiwani Monduli hawaamini katika CHADEMA bali Lowassa;Je hii kidemokrasia imekaaje?(maeneo mengi pia ilitokea)

5.Je hili jambo la kutopendekeza wenyeviti Laac,Pac...kwa sababu kuwa hawawezi,vilaza,limekaaje kidemokrasia?

6.Je kwa matukio hayo hapo juu, CHADEMA imegeuka kuwa chakima? (chakima:chama cha kiimla na malalamiko)

Nawakaribisha kujadili hoja hizo chache ili tufikie muafaka kuboresha vyama vyetu.

Tujikite kwenye mada na sio kelele.
Nakuuliza swali kwanini umeitaja CHADEMA na kwanini aujavitaja. Vyama vinngine ukipata jibu pigia mstari
 
Back
Top Bottom