Siasa hizi sie tunazipigia debe mjini tu.
Na Mikoa yenye mihemko ya kisiasa Arusha,na Dar kwa wavivu wengi.
Ila huko Vijijini watu bado wana misimamo yao na wanaendelea na maisha yao.
Na ukichunguza UKAWA wengi ni vijana waliokata tamaa ya maisha wao wenyewe kwa uvivu wao.Na hii mbinu waliitumia saana CUF huku Zanzibar kuhamasisha wananchi juu ya Maisha bora mbadala wakichukua Dola.Sasa waulize leo hii hali ipoje na wamo ndani ya Baraza la maamuzi.Hahaha utacheka mpaka basi,sasa hivi ADC Hamad Rashid ndio anakuja kupiga msumari ule ule wa ahadi za CUF kuhusu vijana.
Siasa ni kama ugonjwa ambao watu tunaambukizana,yaani ukikaa na mtu fulani basi ukikutana na mwenzio basi maelezo yao yanafanana ila kwenye kuchambua hoja ndio shida sasa.Mtu anakuambia tu mie UKAWA au CCM.Ukimuuliza anakuambia maisha haya yameishanitosha,ukienda kwa undani anakula na kulala kwao na shule alikimbia.
Au mwingine anakila kitu ila mvivu kama yeye hakuna,anatamani kesho yaje mameli ya Kigiriki awe baharia.Political Science ni zaidi ya tunavyoijua kwa wana Siasa wa Tanzania.Na wanaisasa wana Target sana waliojikatia tamaa wao wenyewe.
Sasa watu mkiona pale watu wamejazana kwenye mikutano basi mnaona ndio idadi ya wanachama wenye nguvu,bila kujua upana na uimara wa chama chenyewe.