Hivi Aucho ataweza kurejea uwanjani kabla ya kukutana na Mamelod first leg?

Hii match kama Aucho hayupo namba 6 atacheza job halafu ukuta ni Mwamnyeto na Bacca
Mwamnyeto? Aisee unataka Mamelod wapate penati? Au Mwamnyeto achome? Mamelod wana kasi wale Mwamnyeto haiwezi ile kasi
 
Mshana Jr husema muda ni mwalimu mzuri kama asipoingiza ushabiki wa kiwaki kama ndgu yake ajuae vizuri mpira wa Tz ila zikija timu za kariakoo hujito akili, si mwingine ni Scars
 
Mi naamini Yanga anayo timu ya kushindana na Mamelody hata wao wenyewe wanajiuliza huko walipo namna ya kucheza nayo.

Simba sisi tukiongeza ubora kidogo angalau nusu ya ubora alio nao Yanga na tukichanganya na uzoefu wetu basi Ahly tunamtoa pale kwa mkapa kabla hajafika kwao.
 
Mi naamini Yanga anayo timu ya kushindana na Mamelody hata wao wenyewe wanajiuliza huko walipo namna ya kucheza nayo.

Simba sisi tukiongeza ubora kidogo angalau nusu ya ubora alio nao Yanga na tukichanganya na uzoefu wetu basi Ahly tunamtoa pale kwa mkapa kabla hajafika kwao.
Aisee. Kwamba Simba ili iweze kumfunga Al hly iwe na nusu ya ubora wa Yanga ndo unachomaanisha? Yaani hichi kiwango cha Simba cha sasa inatakiwa ipambane ifike angalau nusu ya ubora wa Yanga na ikifika hiyo nusu ya ubora wa Yanga Al hly anatoka kabla hata ya mechi ya marudiano. Kwa Analysis hii Mame atakula 5G nyumbani na ugenini. Yanga 10-0 Mame na Al hly ana bahati sana kuongoza kundi mbele ya Yanga maana inahitajika nusu ya ubora wake tu kumuadhibu.
 
Droo imepangwa na ni dhahiri shahiri, Yanga imekutana na timu ambayo hakuna timu anayetamani akutane nae. Mamelod ndio timu inayoogopwa na kila mmoja ila Yanga ndio imepangwa nao.

Ni vizuri kupimana ubavu na squad ya Yanga iliyokamili ila kama ikitokea kuna mchezaji wa muhimu kamiss basi ni bahati mbaya unaenda vitani ukiwa haujabeba silaha zako kamili lakini lazima ukapigane.

Je, Aucho atakuwa amerejea uwanjani? Yanga bila Aucho ina struggle sana ni roho ya Yanga iliyo bora.
haiwezekani,hatakuwepo
 
Vyura mmeshaanza kunena kwa lugha..

Niwakumbushe tu tabia moja kubwa ya Mamelodi, huwa hamuonei aibu yeyote anayesimama mbele yao, wale jamaa hawajui home wala away ni wanakukimbiza mwanzo mwisho popote pale...
 
Huwezi kucheza na Mamelodi kwa kutegemea mchezaji mmoja mmoja huwezi kufanikiwa, Yanga watacheza ki timu zaidi ili kurahisishia kazi.
 
Back
Top Bottom