Hivi atakuwa ananipenda au msanii tu?

Black African

Member
Oct 17, 2011
24
3
Kwanza kabisa wana JF,napenda kuwaarifu kwamba me ni member mpya kwenye hili jukwaa,naahidi tutashirikiana ktk kuchangia mada zile zitakazotumwa.Baada ya utangulizi huo,naomba kila mmoja kwa kutumia uelewa wake anieleze kile anachokifahamu juu ya kesi ifuatayo:-
Me ni kijana,miaka 22 kwa muda mrefu sasa nimetokea kumpenda msichana ambaye tulikuwa tukisoma wote kidato kimoja mpk tumetengana baada ya kufaulu na kila mmoja kusoma shule yake.Niliwahi kumtangazia nia, kwa mara ya kwanza alioverturn,kwa muda nikamtokea tena mara ya pili,mara kaniahidi nimsubiri kipindi cha mwezi 1 na nitegemee jibu zuri,kiukweli kwa miadi hiyo nilihisi kuwa hayuko tayari,hivyo sikumshitua tena wala na yy hajanigusia suala hilo ingawaje bado alionesha kunijali na kufurahia uwepo wangu.Ilifika kipindi fulani kama miezi 5 nyuma nikawa simuelewi kabisa,7bu kubwa ni kwamba kuna wakati anaonesha kujali wakati unafuata anaonesha kunipotezea amekuwa haeleweki,kumbe badaye nikagundua nilimuaproch akiwa ndani ya uhusiano,hivyo nikaamua kutodeal naye tena ila tu nilimuahidi kuwa nitaendelea kukaa naye kama mwanafunzi mwenzangu tu.Baada ya kauli hiyo wiki moja mbele nikaona mabadiliko kutoka kwake nikaanza kuona love message kwenye cm,nilimkataza asinitumie,nashukuru alitii amri ila hadi hivi sasa anaonesha kunijali,maana ninapomuhitaji kuongea naye hakatai,ninapomuagiza kitu ananitimizia yaani kiujumla amefanikiwa kuteka hisia zangu.Nataka nimfungulie ukurasa wa 3 ila nahofia kuwa mtumwa wa mapenzi,ila co siri nampenda na ninamuhitaji sana ila ndio hivyo simuelewi.Ahsanteni.
 
tulizan mwana ....hapa kibuti kipo nje nje...sasa lakufanya ni kupotezea tuu
 
unampenda muambie ww c mtoto wakiume bwana au?????? na kama humuelewi mpotezee asije kua anakuweka ktk mzani ww na huyo msela wake
 
sa ka ulikataa kutumiwa msg za mapenzi unachompendea ni nini???ngono???mana msg nazo huleta maana hata ka vidole ndo vimeandika
 
ooooooh, so sweet! amenikumbusha enzi zileeeee, unampenda mtu ila unaogopa ukikubali atakuona una haraka sana, na ukikataa moja kwa moja ataona huna interest, so unamkaribisha na kumfukuza at the same time.
Kijana, hiyo game anayo cheza ndio na yako pia. Fikiria yeye ndio kaanadika hivi:
kuna kaka aliwahi kunitongoza ila sababu nilikua katika uhusiano mngine nikampotezea. alikubali tubaki marafiki na katika urafiki huo nika devellop feelings kwake. nikamtumia message za mapenzi ila akanikataza na nikaacha. cha kushangaza ni kwamba nikisoma signal zake naona kabisa kua ana interest na mimi ila nashindwa kuelewa kwa nini hanitamkii. Jamani naomba ushauri, nifanyeje?
wewe kama wewe ungempa ushauri gani?
 
Nimekusoma,ila nilikataa sms zake huku nikiwaza ule ni mchezo wa danadana,sikuwaza kabisa kma atakuwa amedevelope feelings.
 
Umesema bado uko shule, MMU unafanya nini potea haraka sana! unastahili viboko we dogo!
 
Soma kwanza mapnz yanazingua sn sio raha wakati wote,utayakuta huko mbele ukishamaliza maliza masomo yako na akili itakuwa imekoomaa vya kutosha kupambana na hizo purukushani za mapenz na kuweza kufanya maamuzi sahihi!
 
Bado utaona mengi sana kijana. hasa siku utakapoanza kumchukia na kujilaumu
kumjua, huku ukiujilaumu saaaana, na bado huo hautakuwa mwisho
 
Wengi huwa wanashauri kuhusu kuzingatia masomo na kuachana na mambo ya mapenzi. kupenda sio kubaya ila nakushauri yafuatayo
1. jisomee vitabu kuhusu maisha safi ya ujana, urafiki mpaka uchumba vitakusaidia. hivi vipo aina tofauti na lugha nyingi, tembelea bookshop
2. Zingatia mafundisho ya dini kama angalizo la wewe kutokiuka maadili.
 
Back
Top Bottom