Historia ya Nchi Yetu

Jan 3, 2017
11
38
HATUNA ZAIDI YA NYERERE?
_______________________________

Na #Mwenda ND,

Raiis John Pombe Magufuli (JPM) IJUMAA alinzudua mradi wa umeme katika Bonde la Mto Rufiji (Stigler's Gorge), katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na watu wengi kutoka sekta binafsi na serikalini, katika hotuba yake JPM alitoa maelekezo ya kulimega pori la Selous na kufanya kipande cha juu cha pori hilo kuwa Hifadhi ya Taifa, JPM aliendelea kwa kusema Hifadhi hiyo iitwe Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (hapa ndiyo hoja yangu ilipo hasa) kuenzi juhudi za Mwl Julius Nyerere katika uhifadhi!

Labda niseme tu kuwa, sina chuki na Mwl Julius Nyerere wala Mwl John Magufuli, bali ni kutaka tu kujua hivi nchi yetu hatuna zaidi ya Nyerere? Hatuna watu wa kuwaenzi zaidi ya Nyerere, mbona kila mahala ni Nyerere tu? Barabara, Shule, Vyuo, Madaraja, Mitaa vyote nk Nyerere, hivi hatuwezi kuwakumbuka na wengine japo kwa uchache tu, histi ya nchi yetu iko wapi? Kwanini ibebe mtu mmoja tu?

Mwl Julius Nyerere ndiye Rais wetu wa kwanza, pia ni mmoja ya viongozi waliopigania uhuru wa nchi hii, lakini kwanini tunamuenzi na kumpa heshima kubwa pekee yake? Nasikitika kwamba historia ya mashujaa wa nchi hii imekuwa ikisiginwa mno, kila mahala anatajwa mtu mmoja tu kwanini? Hatutendi haki...

Hivi Julius Nyerere alikuwa kiongozi wa kila kitu? Kwanini hatutambui michango ya watu wengine? Sikatai kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kwanza wa taifa letu huwa wanapewa heshima lakini heshima wanayopewa ni ndogo kuliko Mwalimu. Kwanini wakati walikuwa sawa na Mwalimu? Tena wengine walikuwa ni zaidi ya mwalimu lakini walimpa tu nafasi yeye!

Kwanini hatuandiki historia ya kuwatambua na kuwapa heshima wazalendo wengine kama tunavyofanya kwa Mwl Nyerere? Vizazi vyetu tunavirithisha nini hasa kama historia haisemi ukweli juu ya wale wote walioshiriki kupigania Uhuru wa nchi yetu? Tuna deni kubwa sana...

Ukiachana na Mwl Julius Nyerere na Rashid Kawawa tuna wazalendo wengi sana waliopigania uhuru wa nchi yetu kama vile Joseph Kassela Bantu, Abdulwahid Sykes ambao hawakuwa sehemu ya Serikali lakini waliipigania nchi, pia tuna Mawaziri wengi wa mwanzo katika Serikali mpya ya Tanganyika kama Sir George Kahama, Oscar Kambona, Amir H. Jamal, Paul Bomani, Job Lusinde, Chifu Abdallah Fundikira III, Azip Swai, Tewa Said Tewa na wengine wengi walioitumikia nchi hii kwa uadilifu mkubwa, lakini hatusikii wakipewa heshima kama Nyerere, kwanini?

Kule Afrika Kusini mbali na Nelson Mandela, watu kama Steve Biko, Walter Sisulu, Chris Hani, Oliver Tambo, Winnie Mandela, Askofu Desmond Tutu, Thabo Mbeki, Simon Mahlungu na wengine wengi wanapewa heshima kubwa sana kama Nelson Mandela anavyopewa, sisi shida ni nini hasa mpaka tuwasahau wengine? Leo unaweza kumuuliza hata Waziri kama anajua kuna mtu anaitwa Tewa Said Tewa alishawahi kuwa Waziri, atakwambia hajui!

Tunakwama wapi kama taifa kutambua michango ya watu kama hao waliodai uhuru wa nchi yetu licha ya kuwa walikuwa wanahatarisha maisha yao dhidi ya utawala wa kikoloni? Kwanini hatuwapi heshima wanayostahili kwa mchango wao kwa taifa?

Marekani ukiachana na Rais wa kwanza wa taifa hilo George Washington kupewa heshima pia bado kuna watu wengine wanapewa heshima sawa na Jenerali George Washington, wanaopewa heshima sawa na Washington ni pamoja na Thomas Jefferson, John Adams, Benjamin Franklin, Abraham Lincoln, pia mpaginia haki za watu weusi Dk. Martin Luther King Jr wanapewa heshima kubwa mno!

Kwenye noti ya $ 1 kuna picha ya George Washington aliehudumu kama Rais wa kwanza wa Marekani (1789-1797), kwenye $ 5 kuna picha ya Abraham Lincoln Rais wa 16 wa Marekani (1861-1865), kwenye noti ya $ 10 ipo picha ya Alexander Hamilton (1789-1795), huyu hakuna rais bali alikuwa Waziri wa Fedha wa kwanza wa Marekani na ndiye mwanzilishi wa Benki Kuu ya Marekani (Federal Reserve) na ndiye mtunga sera za uchumi katika utawala wa George Washington, vilevile kwenye noti ya $ 20 kuna sura ya Rais wa 7 wa Marekani Andrew Jackson (1829-1837), na kwenye noti ya $ 50 ipo picha ya Rais wa 18 wa Marekani Ulysses G. Grant (1869-1877), pia kwenye noti ya $ 100 ambayo ndiyo noti ya mwisho nchini Marekani ipo picha ya Benjamin Franklin.

Huyu Benjamin Franklin hakuwa rais lakini ni mmoja ya watu muhimu katika historia ya Marekani, yeye ndiye aliyeijenga Pennsylvania na mmoja watu wa kwanza kuiunganisha Marekani kutoka majimbo (Vinchi vidogo-vidogo) 50 na kuwa taifa moja lenye nguvu. Huwezi itaja historia ya Pennsylvania bila kumtaja Benjamin Franklin, huyu alikuwa ni mwanadiplomasia mbobevu kweli kweli. Marekani haina Baba wa Taifa, wenzetu wana Mababa waanzilishi wa Marekani (Founding Fathers of the United States of America) ambapo watu 17 waliotoa azimio la Uhuru wa nchi yao huko Philadelphia wanatambulika kwa mchango wao huo mkubwa!

Kwanini sisi hatutambui michango ya waanzilishi wa taifa hili? Mtu kama Oscar Kambona ndiyo hakumbukwi kabisa katika historia ya nchi hii licha ya kuwa na mchango mkubwa katika kuleta Uhuru wa nchi yetu, mtu kama Mzee Edwin Mtei, Gavana wa kwanza wa Benki Kuu sidhani kama anapewa uzito anaostahili kwa kulitumikia taifa hili!

Wapo wengi waliopigania na kuitumikia nchi hii katika nyanja mbalimbali lakini hawapewi heshima yao na wala historia ya nchi hii haiwatambui, kama taifa tunapaswa kuandika historia upya, ili tusije kuhukumiwa hapo baadae na vizazi vyetu! #HistoriaTanzania
FB_IMG_1561754691913.jpeg
 
Wapo wengi waliopigania na kuitumikia nchi hii katika nyanja mbalimbali lakini hawapewi heshima yao na wala historia ya nchi hii haiwatambui, kama taifa tunapaswa kuandika historia upya, ili tusije kuhukumiwa hapo baadae na vizazi vyetu! #HistoriaTanzaniaView attachment 1165732
Mwenda,
Nimefurahishwa sana na makala yako.

Naomba nikueleze machache ambayo mimi binafsi nimekutananayo katika
uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika.

Hassan Upeka alikuwa katika jopo la uandishi wa historia ya TANU chini ya
Chuo Cha CCM Kivukoni.

Kwa kutambua kuwa historia inayotafitiwa na kuandikwa ilikuwa ni historia ya
TANU alileta mbele ya jopo lile ''notes'' za mahojiano aliyofanya na Abdul
Sykes
kuhusu TANU.

Jibu alilopewa na mwenyekiti wa jopo lile la Chuo Cha Kivukoni CCM ni kuwa
historia inayoandikwa haina uhusiano na Abdul Sykes.

Maneno haya kanieleza Hassan Upeka mwenyewe kwa kinywa chake.
Unaweza ukasoma historia ya Hassan Upeka hapo chini:

Nimeandika kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika kupitia maisha ya Abdul
Sykes
lakini kabla ya kitabu kuchapwa nilikuwa naandika makala za historia ya
uhuru wa Tanganyika.

Nikaandika makala, ''In Praise of Ancestors,'' katika gazeti likiitwa Africa Events
likichapwa London na Mhariri wake alikuwa Mzanzibari Mohamed Mlamali Adam.

Yale niliyoandika mle yalitofautiana sana na historia katika kitabu cha Chuo Cha
CCM Kivukoni ambacho kilianza na Julius Nyerere na kumalizikia na Julius Nyerere.

1564374824012.png

Toleo hili la gazeti lile lilikusanywa na ni magazeti machache sana yalipenya kuingia
sokoni.

Unaweza kusoma historia ya Africa Events hapo chini:

Pamekuwa na hofu ya kutafiti na kuandika historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika na
tatizo kubwa ni kuwa yeye mwenyewe Mwalimu Julius Nyerere kwa sababu fulani labda hakuipenda.

Matokeo yake ikawa ni kuwa na historia hii ambayo TANU inaanza na yeye hadi uhuru
ukapatikana na kwa nusu karne walichokijua wananchi ni hii historia ya Nyerere peke yake.

Kwa historia ya TANU vipi iliasisiwa na vipi Mwalimu Nyerere Baba wa Taifa alikuja kuwa
kiongozi wa TAA 1953 na kisha TANU 1954 ingia hapo chini:

Mkuu ndio maana nimeanzisha ule uzi angalau tuwatambue watu 100 walioipigania nchi hii na kuchangia maendeleo makubwa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni

Binafsi huwa nakereka sana mtu mmoja tu kuzoa credit za upiganiaji wa uhuru wa nchi hii wakati kuna wazalendo kibao ambao wanasahauliwa ama kutotambulika kwa makusudi kabsa, mtu kama John Rupia ama Paul Bomani yaani sijui kama ameenziwa kwa lolote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom