Historia ya kweli kabisa!!!

VPN USED2020OCTOBER28

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2011
Posts
1,505
Reaction score
677
Baba yangu alifariki nilipokuwa na miaka miwili hivyo sijawahi kupata mapenzi ya baba kabisa....na mama alinizaa akiwa sekondari miaka ya 80s .....kwa hyo nimekulia kwa bibi tena kijijini ...miaka ikaenda....nikaendelea ishi kijijini na niakaanza primary hukohuko kijijini..mpaka darasa la nne...ndipo upande wa baba wakaja nigomboa kutoka kwa bibi....nikaenda ishi na ba mkubwa.....tatizo halikuwa kwa ba mkubwa tatizo lili kuwa kwa mke wa dingi mkubwa ...kifupi alikuwa hanipendi kabisa kabisa mpaka ilifika nikikosea kidogo tu alinifokea sana tena sana mpaka aliwaamulu watoto wake wasiniongeleshe wiki nzima eti!!!! Niliishi kinyonge sana hapo tu nikiwa na miaka sita au saba.... Niliishi kama kuishi tu ...nilikosa mtu wa kumueleza kwakweli.... Maana nlikuwa najua kabisa bamkubwa hakuwa na muda wa kukaa na mimi kwa sababu alikuwa ametingwa na kazi... Ila najua kabisa alikuwa anajua kuwa mke wake ni mkali!!! Nikaishi kwa unyinge sana...nikifanya kosa kidogo tu inakuwa kama kosa la mwaka mzima!!! Nikiwa nasema nadhani walioishi maisha haya wanayajua kabisa!! Mengine siwezi simulia maana hakuna anayeweza amini kabisa!!!! Ikafika nikapata ujasiri wa kutoroka kutoka japo sikuwa na nauli kabisa...niliamka hasubuhi na mapema mwaka 1996 nikikuwa na shing hamsini tu ile ya noti nyekundu!!!! Kwa bibi mzaa mama nauli yake ilikuwa 1500 kipindi hicho..... Nilitembea kwa miguu nilipofika njiani mida ya saa sita mchana niliona gari ya abiria nikasimamisha....gari ikasimama ....konda aliponiona akapatwa hofu sana maana nilikuwa nimechoka ...akasema unaenda wapi!!!! Nikamjibu naenda kwa bibi ...akaniambia kwa bibi wapi.....nikamwabia kijijini huku machozi yakinilengalenga....na nkashindwa jieleza....akasema twende....... Basi ikawa hivyo..,... Nikafika kwa bibi mida ya usiku saa mbili..,. Bibi akalia sana pamoja na mamkubwa ......kwa sababu miaka hiyo kwa mimi kusafiri peke yangu ilikuwa ni hatari sana.....


Itaendelea
 
Utamu wa simulizi ukianza tu, mnaanza na ishu ya itaendelea, inafika mahala wasomaji tunakosa la kujifunza kwa kukata tamaa ya kuendelea kusoma.

Sijui waandishi / wasimulizi mnaambiana kufanya hivyo?!

Ahsante!
 
Labda alisema ataendelea ili ayaone maoni kama hayo yako, wasiwasi wangu ni asije kata tamaa akaacha kabisa kuendelea wakizidi kumshambulia wengine wakija. Mimi naacha kwanza hadi amalize. Kuna jamaa alikuja hivix2 yule wa 'baada ya chuo akahifadhiwa na mpenzi.... Akaja jibaba akaingia nae chumbani... Akafikia kwa mjumbe wa mtaa...' si mnamkumbuka alivyoshambuliwa? Sikumbuki kama aliimalizia ile simulizi.

Cc Miss neddy

Ahsante!
 
Kweli yule jamaa sijui kakimbilia wap! MTU kama hawezi kuleta story yake bas aache si lazimaa hi nitamalizia siipendii kweli wanatuacha na hamu tuu!
 
Hata part 1 hujamaliza mkuu...maana part1 huwa ndefu kidogo, wewe umefanya fupi!..
 
Eti unaenda wapi ukajibu. Kijijini
Dah
Ukirudi hebu tuelezee vizuri sio kwa mikato na kujichanya maelezo
 
Haya ya kuendelea kesho ndio tunayowafundisha Wadogo zetu uvivu wa kujisomea...nae utasikia nitajisomea kesho(uvivu)
 
Hapo kwenye nyekundu kama vile kuna chumvi kidogo,maana miaka hiyo hakukuwa na hiyo noti, bali sarafu.
 
Kabla hujaendelea punguza chumvi wakati unagombolewa ulikuwa la nne kufika kwa mammkubwa ulikuwa na miaka sita au saba so ulianza la kwanza na age gani enzi 80 huko?
Hii chai imegoma kuchemka.....

Ina maana alianza darasa la kwanza akiwa na miaka 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…