N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 6,825
- 9,533
Mapigano ya Tanga, ambayo wakati mwingine pia hujulikana kama Mapigano ya Nyuki kikosi "B", yalikuwa ni shambulio lisilofanikiwa la Jeshi la Uingereza chini ya Meja Jenerali A. E. Aitken lililolenga kuitwaa Afrika Mashariki ya Kijerumani (sehemu ya bara ya Tanzania ya sasa) wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia katika shambulio la Jeshi lililofanyika sambamba na shambulio jengine la kikosi "C" cha Uingereza karibu na Longido kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro.
Lengo la Mwingireza kuvamia akitokea upande wa Kenya ilikuwa kumwondoa Mkoloni Mjeremani kutoka Germany East Africa yaani Tanganyika au Tanzania ya sasa. Tanga ulikuwa mkoa muhimu wa ofisi za Ujeremani.
Hili lilikuwa shambulio la kwanza kabisa kwa ukanda wa Afrika Mashariki kufanywa na vikosi vya Uingereza na Wapambe wake "Triple Entente".
Lilishuhudia Waingereza wakishindwa na kudundwa na kikosi kidogo zaidi cha Askaris wa Ujerumani na askari wazawa wa Tanganyika waliojitolea wakiongozwa na Luteni Kanali Paul von Lettow-Vorbeck.
Ushindi wa Ujerumani kwenye bato hii na kwa kuzingatia ilikuwa ndo bato ya mwanzo kabisa ktk koloni la mjeremani...ilimwezesha mjeremani kujipanga kwa kuweka mazingira yatakayomwezesha kukichapa vema huko mbeleni kutetea koloni lake Tanganyika au Germany East Africa.
Baada ya hii ambush Mjeremani aliandaa vifaa vya kisasa vya mapigano kwa wakati huo(ikizingatiwa kwamba alikuwa na advanced war technologies kuliko wenzake sabu alikuwa superpower huko yuropa), vifaa vya matibabu, mahema, blanketi, chakula na idadi kubwa ya bunduki za mashine za Maxim ambazo ziliwaruhusu kufanikiwa kupinga uvamizi wa majeshi ya washirika kwa muda wote wa vita.
WIKIPEDIA