Historia inayoumiza.!

Historia inayoumiza.!

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
202
Reaction score
1,588
Mwaka 2006 vijana watatu ndugu wa familia moja ambao walikua wafanybiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro pamoja na dereva taxi wao waliuawa kikatili na serikali ya CCM chini ya agizo la aliyekuwa Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Dar Abdalah Zombe.

Wafanya biashara hao ambao ni Ndg.Ephrahim Chigumbi, Sabinus Chigumbi ?Jongo?, Mathias Lunkombe waliuawa kwa kupigwa risasi na Polisi pamoja na derev wao Bw.Juma Ndugu.

Taarifa iliyotolewa na Polisi ilisema watu hao walikua majambazi hivyo wameuwa wakiwa wanarushiana risasi na Polisi. Lakini Tume ya Jaji Kipenka iliyoundwa kuchunguza suala hili ilibaini hawakuwa majmbazi bali wafanyabiashar wa madini.

Ripoti ya Jaji Kipenka ilonesha kuwa ndugu hao watatu walikua na fedha kiasi cha Shilingi Milioni 200 pamoja na aina mblimbali za madini. Polisi walipata taarifa hizo na hivyo wakaanza kutafuta namna ya kuwadhulumu.

Kamanda Zombe akaagiza wakamatwe, wakapelekwa msitu wa Mabwepande, wakafungwa vitambaa vyeusi usoni. Wakanyang'anywa fedha zote walizokua nazo pamoja na madini. Kisha wakapigwa risasi na kuuawa. Baada ya hapo Zombe akajitokeza na kudai ameua majamazi. Huu ni ukatili wa kiwango cha juu kupata kutokea katika historia ya nchi yetu.

Jaribu kufikiri vijana hawa walikua wanatafuta maisha kwa kufanya biashara ya madini ili watunze familia zao na kusomesha watoto wao. Lakini kwa tamaa ya fedha na mali wakauawa kinyama na kuporwa vyote walivyokuwa navyo. Mbaya zaidi wakaitwa majambazi.

Wake zao wakabaki wajane, na watoto zao wakabaki yatima, hawana baba wa kuwatimizia mahitaji yao tena, hawana baba wa kumuomba ada ya shule, hawana baba wa kumlilia wakiwa na shida, hawana baba wa kulipa kodi ya nyumba. Serikali ya CCM kupitia Jeshi la Polisi iliwaua baba zao kikatili na kuwapora mali zote.

Mbaya zaidi wakaitwa majambazi wakiwa tayari maiti na hawana uwezo wa kujitetea. Kinachoumiza zaidi ni kwamba serikal ya CCM iliyowaua haijui hatma ya familia zao. Haijuikama watoto wao wanasoma au wamekuwa machokoraa kwa kukosa ada, haijui kama wanakula au lah, haijui wanalipaje kodi ya nyumba, haijui lolote kuhusu familia hizi. Walipowaua wakaelekeza na familia.

Hata madini na fedha walizoporwa na Polisi hazikurudishwa kwenye familia. Badala yake familia zilipewa maiti wazike. Ukatili, ukatili, ukatili uliovuka mipaka wa serikali ya CCM na vyombo vyake vya dola. Halafu bila aibu wanajitapa kuwa Tanzania ni nchi ya Kidemokrasia. Kibaya zaidi watuhumiwa wa mauaji haya waliachiwa huru. Kuanzia Kamanda Zombe na wenzake. Hukumu iliyosomwa na Jaji Salum Massati ilionesha hawana hatia.

Jambo la ushangaza ni kusikia eti Kamanda Zombe amefungua kesi ya madai baada ya kuonekana hana hatia. Alifungua kesi mahakamani akidai serikali fidia ya Bilioni 3 eti kwa kusumbuliwa na kudhalilishwa na kupotezewa muda wake. Sijui hatma ya kesi hii iliuaje lakini haya ni maajabu ya 8 ya dunia.

Unadhani familia za marehemu zinajisikiaje zikiona Zombe analipwa hayo madai. Yani uwaue baba zetu kikatili, uwapore pesa na madini, kisha uwasingizie ujambazi, sisi watoto tubaki yatima, tumebaki wanyonge, hatuna baa wa kumlilia shida zetu, hatuna karo ya shule, hatuna kodi ya nyumba, halafu wewe uliyesababisha yote hayo unafungua kesi ya madai na unalipwa Bil.3. Hakika hata Mungu hawezi kuruhusu. Atashusha mkono wake kutoka mbinguni na kuiangamiza CCM na vibaraka wake. Imetosha.

MY TAKE;
Hii ndiyo serikali ya CCM isiyojali maisha ya watu wake. Inaua watu wasio na hatia na kuwasingizia kesi huku wakiwalinda wezi wa mali za uma. Kuendelea kuichagua CCM ni kuruhusu mauaji kama haya ya damu zisizo na hatia yaendelee nchini.

Kuchagua CCM ni kuchagua ukatili, kuchagua CCM ni kuchagua unyama, kuchagua CCM ni kuchagua uonevu wa raia na ukiukaji wa haki za binadamu. Mpe kura yako Edward Lowassa abadilishe mfumo huu kandamizi uliojaa uonevu kwa wanyonge.

Lowassa ndiye mtu pekee anayeweza kubadilisha mfumo na kutetea misingi ya haki na usawa kwa kila raia. Sema imetosha kwa kuinyima kura CCM kesho kwenye sanduku la kura. Mungu mwenyewe ametuletea mtu wa kuondoa uonevu huu, Mtu wa kutuondolea ukatili huu, Mtu atakayejali utu wetu, Mtu atakayetetea wanyonge dhidi ya tabaka tawala. Si mwingine ni Edward Ngoyai Lowassa. Mpe kura yako kesho akutumikie.!

#Change ni mimi, ni wewe, ni sisi. LOWASSA 4 PRESIDENCY.!
 
2006 lowassa alikuwa nani ndani ya serikali?
 
Waziri wa mambo ya ndani alikuwa nani vile?
 
Maamuzi sahihi na yenye busara. Kesho tareh 25 tunaanza safari mpya ambayo ilibidi tuianze miaka mingi iliyopita.

Nguvu ya Umma

M4C.
 
Tungeanza na waziri mkuu wa wakati huo na hapo hapo ndipo tujue yy kama pm alisolve vipi hili
 
Kaka umetisha mbaya,ila nilichelewa kuifungua maana heading yake haiku tempeting sana
 
Malisa,
Wakati mwingine uwe unatumia akili kabla ya kupost. Ulichokifanya ni upumbavu na upofu. Usirudie tena.

Wakati mauaji haya yanatokea mwaka 2006, wakuu wa serikali ya ccm Rais alikuwa JK, na Waziri Mkuu wake (msimamizi mkuu wa shughuli za serikali) alikuwa Lowassa.

Hawa ndo walikuwa vinara wa serikali ya ccm iliyowafanyia nao ndugu unayoyaita mauaji, uovu, ukatili na udhalimu.

Sasa baada ya kuwachafua hivyo. Lowassa ndio mgombea urais kwa kupitia chama chako pendwa cha chadema.

Umetutaka tusiichague ccm kwa maovu hayo. Lakini aliyeyafnaya maovu hayo, au aliyekuwa ba wajibu wa kuyazuia au kuwawajibisha wahusika huyu lowassa ndo anapeta huko chadema.

Hivi sasa unamkumbatia na kumkwepeshea kwa sababu hivi sasa ni mwanachadema mwenzio na unajiliza machozi ya mamba hapa mtandaoni.
Kamweleze Lowassa maovu yake na ya serikali yake aliyoisimamia.

Asante kwa kuwaonyesha watu jinsi alivyo muovu.
Umewaonyesha watu kwa nini wawachukie viongozi wadhalimu.
Umeomba wasiwachague..umewaomba wasimchague Lowassa.

Haya nenda kafurahi na upuuzi uliofanya.

Mwisho wa mahaba ni majuto.
 
Tungeanza na waziri mkuu wa wakati huo na hapo hapo ndipo tujue yy kama pm alisolve vipi hili

Waziri wa mambo ya ndani alikuwa nani?i hope hilo ndo ulitakiwa uulize kwanza kwa sababu jeshi la polisi liko chini ya wizara yake.I don't think if it was the matter to go that far,polisi wanaweza kujiongeza na kuacha udhalimu.
 
Hakika ww malisa umekaa kichonganishi sana
Hayo umeeda kyafufua iliiweje?
 
Back
Top Bottom