Hisia binafsi

Nolelo Nobert

Member
Mar 22, 2016
22
18
Ni jioni tulivu isiyokuwa na rapsha nyingi labda kwa kuwa ni mfungo Wa mwezi mtukufu Wa Ramadhan katika tafakari ya kawaida tu na kuwaza tu..labda naweza hata kukwaza wengine lakini nitaomba nisamehewe bure,
Nafikiria kawaida sana juu ya ubunifu Wa kubuni mambo mbalimbali yenye kutatua changamoto tulizonazo ilituendane na mahitaji ya mwanadamu..nawaza tena katika kubuni huku sisi tulioko huku Africa ..hatuna maarifa hayo na akili hizo ..hapana shaka jibu litakuwa tunazo lakini kwanini? Kila kitu kianzie kwa wenzetu hawa weupe ..mfano suala la teknolojia sisi ni mabingwa wakuwa consumers lakini hakuna jitihada zozote nasisi angalau tufanye ugunduzi Wa stuff ndogo ambazo hata wenzetu waweze kutumia kutoka kwetu...sina wakumlaumu yeyote juu ya hilo kwa maana kama mjadala utawekwa mezani najua fika watu watakuja na hoja kibao za utetezi juu ya hilo.Ningeweza kuzungumzia juu ya nyanja nyingi ambazo bado kama Africa na kama watanzania bado hatuwezi tukaja na ubunifu wenye tija Wa kutoa Huduma itayotatua changamoto lukuki zinazo tukabili..shida iko wapi? ni elimu ndogo tulizonazo au miundo mbinu ya kielimu ndio shida majibu yanaweza kuwa ndio au hapana, hapana shaka kuna wachache wamepata fursa adimu ya kupata elimu hiyo..lakini bado hawajatusaidia..shida hii Ina mizizi mirefu sana, kuichimba inahitaji system thinking ambayo inahitaji ijengewe misingi imara toka awali...kama wahenga wanenavyo..hakuna awali mbovu si vibaya kujipanga upya nakuanza awali mpya yenye tija..ni muda Wa kujitafakari kwa kila mmoja wetu na kuanza kufikiri zaidi(thinking beyond imagination) na sio kufocus kwenye easy to do! Hapo ndipo tutapatata watu bora zaidi wakutuvusha kwenye ulimwengu Wa ubunifu ambao wenzetu wameshavuka hatua kubwa.
"Imagination is more important than knowledge"
#Shabaha
 
Back
Top Bottom