Hisia 8 hatari

Hisia 8 hatari

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138

Miongoni mwa vitu vinavyochangia kuharibu uhusiano wa kimapenzi ni hisia.Wapenzi wengi wameachana kwa sababu si kwamba walithibitisha ubaya wa wenzaoila walijijaza wenyewe hisia mbaya na kujikuta wamepoteza thamani ya kupenda.Hebu angalia hisia nane hatari ili uzikimbie mapema kabla hazijakuharibia penzilako.

1. NASALITIWA
Kuishi katika mapenzi huku ukiwa na fikra kwamba mwenza wako anakusaliti nijambo baya kwa vile huathiri msukumo wa ndani wa kupenda. Matokeo yakeutajikuta ukishindwa kutimiza wajibu wako kama mke/mume kwa sababu tu yakuendekeza hisia mbaya. Acha kuhisi, tafuta ukweli.

2. TUTAACHANA
Kuna wapenzi ambao wanaishi na mawazo ya “ipo siku tutaachana”. Wanafanya hivyoeti kwa kutafsiri mwenendo usioridhisha wa mapenzi yao. Kusema kweli hili nijambo baya kwani huondoa ari na kujenga ufa wa mapenzi.
Huwafanya wapenzi kubakia na wazo moja tu, la kutafuta sehemu mbadala yakwenda baada ya kuachana. Usiwaze kabisa kuachana hata kama mnagombana namwenzako kila siku.

3. SIWEZI MAPENZI
Baadhi ya wapenzi huwa na hisia kwamba hawayawezi mapenzi. Hata kamahawajaambiwa chochote kuhusu kutowatosheleza wenza wao faragha,hukimbilia kujihukumu.

Hujaambiwa kama umecheza chini ya kiwango, hofu ya nini? Usiwaze hivyo, kamauna lolote linalokufanya uwe na hofu muulize mwenzio.

4. NINA KASORO
Naamini mitaani wapo watu ambao huamini wana kasoro fulani ndiyo maanahawafikii viwango vya kupendwa kama wanavyohitaji. “Yaani mimi ningekuwa kamafulani ningefurahi sana lakini ufupi wangu ndiyo tatizo.”

Hizi ni hisia mbaya tu, kumbuka kuna wafupi wanapendwa ile mbaya. Jisahihishena epuka kujishusha hadhi kwenye hisia zako.

5. NITAMUUA
Miongoni mwa hisia mbaya kabisa kwenye mapenzi ni kufikiria kumuua mwenzako kwasababu yoyote. “Nikimfumania na mwanaume mwingine nitamuua.”

Mtu anayetawaliwa na mawazo ya aina hii anajiweka katika mtego mbayakisaikolojia wa kuja kutekeleza kile anachojiapiza hata kwa sababu ndogo.Usifikirie hivyo maishani mwako.

6. NIMEKOSEA KUCHAGUA
Usijihukumu makosa kwa sababu umeona mpenzi wako ana tatizo fulani. Fahamu kuwakasoro ni sehemu ya ubinadamu. Weka mikakati ya kumuongoza mwezio kulikokuhitimisha kwa mawazo kwamba ulikosea kumchagua. “Ningejua kama yuko hivinisingemchagua.” Usiwaze hivi!

7. HATUWEZI KUZAA
Kuna wapenzi ambao kwa kuishi miaka mitatu au minne pamoja bila kupata mtotohufikia kwenye fikra kwamba hawawezi kuzaa. “Mmm, mwaka wa nne umepita bilamtoto, nadhani sisi hatuwezi kuzaa.”

Kwa nini msizae? Hizo ni fikra zako, hamjaambiwa na daktari sasa iweje uwazehivyo? Jipe moyo kwani kuna watu walizaa baada ya miaka kumi, iweje ninyi wamwaka mmoja?

8. UNANIDANGANYA
Ipo aina ya watu ambao hata kama wakiambiwa wanapendwa sana, hukimbilia kusemana kuamini kuwa wanadanganywa. “Mmm unanidanganya.” Atasema hivyo licha yakuona mwanaume anavyojituma kumsotea na kumuonesha kila dalili za mapenzi. Hilini jambo baya, ukithibitisha kwamba unapendwa usihisi unadanganywa, utapotezabahati yako.

Namba 2 mmh!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
kujihisi muhimu loh kwani mmekutana meno 32 mdomoni utajiassure vp ww ndo umefika kuliko wote aliowaona,ukibweteka ndo utajikuta na manyoya kuku kaliwa.
 
kujihisi muhimu loh kwani mmekutana meno 32 mdomoni utajiassure vp ww ndo umefika kuliko wote aliowaona,ukibweteka ndo utajikuta na manyoya kuku kaliwa.
Hufanyi vyema Mkuu Asnam
 
Last edited by a moderator:
...ongeza na hii "wanaume wote ni sawa,baba mmoja mama mmoja"...
 
Sasa tufanyeje wakati kama huwazi hayo kwa mwenzako, yeye anakuwazia hivyo?
Bora kukaa bila kuoa tu maana majanga ni mengi sana ktk ndoa hasa za siku hizi tunapojidai tumestaarabika kumbe sifuri ndugu yake zero.
 
ndoa doa nikazi kweli kweli maisha haya huwa nayatafakari kwa mapana ila huwa nashindwa kufikia majibu kwa nini inakuwa hivyo
 
7. HATUWEZI KUZAA
Kuna wapenzi ambao kwa kuishi miaka mitatu au minne pamoja bila kupata mtotohufikia kwenye fikra kwamba hawawezi kuzaa. "Mmm, mwaka wa nne umepita bilamtoto, nadhani sisi hatuwezi kuzaa."

Kwa nini msizae? Hizo ni fikra zako, hamjaambiwa na daktari sasa iweje uwazehivyo? Jipe moyo kwani kuna watu walizaa baada ya miaka kumi, iweje ninyi wamwaka mmoja?

Hii hisia namba saba imewakumba wengi sana. Wenye imani za kidini hukimbilia kwenye maombi, wale wenzangu na mie hukimbilia kwa waganga wa kienyeji na wale ambao hawako huku wale kule saa nyingine hukimbilia kwenda kuzaa nje ya ndoa au kuikimbia ndoa kabisa!!!

Sina uhakika na sababu za matatizo ya kuchelewa kupata watoto kwa nyakati hizi za sasa, ila nimeona ni vyema kuwa makini na sababu yeyote ile ambayo itatajwa kwamba inachangia kukua kwa tatizo hili siku hadi siku. Kuzaa nje ya ndoa au kuikimbia ndoa mara nyingi si suluhu, bali huongeza machungu na hasira ndani ya familia.
 
hisia nyingine ni za kweli na pengine umethibitisha labda kwa kufuma mesej za mapenzi kwenye simu ya mpenzi wako.. sasa tutazikwepa vipi hisia za kusalitiwa ilhali dalili zipo wazi?
 
Mi kwa upande wangu ua NAJIEPUSHA kabisa na visababishi vya hcia mbaya ka vle CM YAKE,FKRA HASI,KUHOJHOJ,TAARIFA mf.kabla cjafika nyumban namtaarifu kuwa NAKARIBIA KUFIKA,,,,,,,,,,,,,,,,,,,N BORA NIJIDANGANYEDANGANYE TU KWAN NIKIJUA UKWEL ITANIUMA JAPO,,,,,********
 
Nimeamini wewe wewe kweli ni Joka...... Good thinking.
 
Hii hisia namba saba imewakumba wengi sana. Wenye imani za kidini hukimbilia kwenye maombi, wale wenzangu na mie hukimbilia kwa waganga wa kienyeji na wale ambao hawako huku wale kule saa nyingine hukimbilia kwenda kuzaa nje ya ndoa au kuikimbia ndoa kabisa!!!

Sina uhakika na sababu za matatizo ya kuchelewa kupata watoto kwa nyakati hizi za sasa, ila nimeona ni vyema kuwa makini na sababu yeyote ile ambayo itatajwa kwamba inachangia kukua kwa tatizo hili siku hadi siku. Kuzaa nje ya ndoa au kuikimbia ndoa mara nyingi si suluhu, bali huongeza machungu na hasira ndani ya familia.

..hapo kwenye red mkuu.... ni vyakula tulavyo... ndio chanzo halisi cha kutokupata watoto kwa wakati......au kuchelewa..
 
hisia nyingine ni za kweli na pengine umethibitisha labda kwa kufuma mesej za mapenzi kwenye simu ya mpenzi wako.. sasa tutazikwepa vipi hisia za kusalitiwa ilhali dalili zipo wazi?

..usipende kuchunguza simu ya mwenzio....pressure namba 1.....
 
na 1 na 2 ni majanga kila kukicha,,na huwezi kuacha kumhisi mwenzio wakati kuna vitu kabisa unaviona haviko sawa,,yani ukianza kuhisi vitu km hivyo maana yake kuna vitu vya chini chini vinaendelea,,muhimu kufanya uchunguzi kuthibitisha na sio kukurupuka km mwehu..na ushahidi unapokamilika ndo swala la namba 2 linapoingia kati..HAYA MAPENZI YA SIKU HIZI YANACHOSHA SANA HADI NAJUUTA KUYAFAHAMU..LOL:confused3:
 
Back
Top Bottom